Nataka nirudi shule kwa ajili ya PhD mwaka huu

Nataka nirudi shule kwa ajili ya PhD mwaka huu

CHIEF MGALULA

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2009
Posts
1,193
Reaction score
915
Wadau nimeanza mchakato wa kuomba phd hapo IRA-UDSM.Najua kuna changamoto zifuatazo hivyo naomba mnipe namna yankukabiliana nazo;

1.Udhamini angalau kwenye utafiti tu.

2.Muda wa kumaliza...nitumie mbinu gani basi nimalize kwa muda muafaka.yaani miezi 36 kama inavyotakiwa.

3.n.k.

Asante
 
Wewe Ni bogus.
Spelling hujui........
PhD yenyewe hujui inavyoandikwa. Nadhani kaanzie dip. Pale CBE
 
Kwenye udhamini sina hakika sana labda jaribu kuomba mashirika yasiyo ya kifaida kutoka ktk nchi za ki-Nordic kama Norway au Denmark au Sweden kupitia balozi zao.

Kuhusu kumaliza elimu yako ya uzamivu(Ph.D) ndani ya wa kati vyuo kama Udsm au University of Nairobi(UoN) maana huwa wanashirikiana hakikisha unawa-push sana supervisors wako kila muda unawasumbua kuisoma kazi yako na angalau ujitahidi ku-publish paper mbili locally hapo hapo chuoni kwako miezi 18 ya mwanzo.

No offence, kama una kichwa kizuri nenda kasome University of Capetown (UCT) pale utamaliza ukiwa vizuri sana kichwani bila kubebwa bebwa na supervisors na wapo very strictly sana humalizi Ph.D bila ku-publish angalau paper mbili ktk international journals. Kitu ambacho vyuo vya Afrika mashariki kama Dar es Salaam, Makelele au Nairobi unamaliza tu kirahisi rahisi bila kuifanyia kazi yaani wanatoa Ph.D kama Masters bila hata ku-publish (through your unpublished thesis only). Ni Afrika mashariki pekee hapa ulimwenguni hasa hasa Tanzania si ajabu kumkuta mtu ana Ph.D ila hana chapisho lolote lile ktk international journals hasa hasa akisoma hivi vyuo vya mchangani nilivyovitaja hapo.😀
 
Yaani wewe mweupe kama theruji....unaadika kwa kuchanganya herufi kubwa na ndogo...yaani hata mtoto wa std 3 anakushinda..halafu unataka kuchukua fomu ya udiwani...
Wewe Ni bogus.
Spelling hujui........
PhD yenyewe hujui inavyoandikwa. Nadhani kaanzie dip. Pale CBE
 
Kitu ambacho vyuo vya Afrika mashariki kama Dar es Salaam, Makelele au Nairobi unamaliza tu kirahisi rahisi bila kuifanyia kazi yaani wanatoa Ph.D kama Masters bila hata ku-publish (through your unpublished thesis only). Ni Afrika mashariki pekee hapa ulimwenguni hasa hasa Tanzania si ajabu kumkuta mtu ana Ph.D ila hana chapisho lolote lile ktk international journals hasa hasa akisoma hivi vyuo vya mchangani nilivyovitaja hapo.😀
Mkuu mambo yanabadilika. Kwa SUA kwa mfano preferred mode of presenting results zako ni papers. Issue ni je umeplan kumaliza kwa muda gani? Muda ukiwa mfupi publishing inakuwa changamoto. Issue ya kumaliza kirahisi rahisi kwa sasa si kweli kwa chuo kama SUA.
Kitu cha msingi ni kuomba uwe na supevisory panel ambayo inajali kazi ya mwanafunzi kama kipaumbele vinginevyo utapoteza muda mwingi kusubiri feedback, hasa kama hao wakuu wana "majukumu" mengi pamoja na consultancies nyingi zinazo wanufaisha wao binafsi.
Na wewe mwanafunzi unatakiwa uwe sharp-unajituma ipasavyo na ujenge network yako.
 
Back
Top Bottom