Sijui uwezo wa betri mnalinganishaje, mimi ninaona Samsung kwa sasa wameboresha mfumo wa betri, cha msingi nunua original.
Kwa mfano, kama ni mtu wa kuchati kwa kadiri, yani unaingia na kutoka, unaweza kushinda kutwa nzima hujaichaji simu.Ninajua kuwa kuna simu zina uwezo zaidi ya huu, lakini kwa simu janja nyingi, kushinda kutwa nzima hujachaji ni uwezo mkubwa pia.
Samsung ni bora kwa kiasi fulani,ila ni ghali.Kama una hela zisizo na kazi,hasa ukizingatia kwamba vyuma vimekaza,nunua Samsung.Ila kama ni mtu unaejali pesa,nunua Techno.Ni nzuri tu,mimi ninayo Techno W4 sasa mwaka karibu wa nne huu, inadunda tu.