Nataka NIMSHITAKI BABA YANGU MZAZI....JE INAWEZEKANA?

Baba Matatizo

JF-Expert Member
May 5, 2011
334
64
Baba yangu hataki kutunza familia kabisaaa.vikao vyote vimeshindwa kumrekebisha.mdogo wanguw kafaulu kuanza shule ya kata.ada ni kianzio ni laki na nusu.mpaka sasa hakuna linaloendelea.pombe anakunywa kila siku.mshahara wake +
posho ni kama laki 7 kwa mwezi.NATAKA NIKAMSHITAKI USTAWI WA JAMII KWA KUSHINDWA KULEA FAMILIA NA KUTOMPELEKA MTOTO SHULE BILA SABABU.JE INAWEZEKANA KUMPELEKA USTWAI WA JAMII?NAOMBENI MAWAZO.
 
Na wewe si mkubwa tu baba matatizo! Saidia kumpeleka mdogo wako shule bana. Dingi keshakuwa cha pombe huyo!
 
Zungumza naye kwanza, ikishinfikana tumia wazee wenzake (baba mkuwa au baba mdogo) ikigonga mwamba peleka Ustawi fasta, mwehi huyo!
 
Jikakamue najua unamuogopa maana wazazi wengi wa kiafrika wanatumia ukali kama ngao ya kutorekebishwa na watoto.
Hakikisha siku hiyo hajanywa, usije mshauri hilo suala huku amalewa!
Najua kuna watu watasema walee wewe kwakuwa umekuwa sasa yeye hela yake atafanyia kazi gani? na kama bado anafanya kazi huyo ananguvu zake...atimize wajibu wake....wewe unuweza kuwa unasaidia kidogo....maana hata wewe unahitaji kuwa na watoto na mke nani atakutuzia?
 
baba mkubwa kashindwa.baba mdogo kashindwa.majirani na wazee wengine wameshinwa.mpaka nakuja hapa.tayari nishajaribu mbinu zote.za mwanzo
 
Baba yangu hataki kutunza familia kabisaaa.vikao vyote vimeshindwa kumrekebisha.mdogo wanguw kafaulu kuanza shule ya kata.ada ni kianzio ni laki na nusu.mpaka sasa hakuna linaloendelea.pombe anakunywa kila siku.mshahara wake +
posho ni kama laki 7 kwa mwezi.NATAKA NIKAMSHITAKI USTAWI WA JAMII KWA KUSHINDWA KULEA FAMILIA NA KUTOMPELEKA MTOTO SHULE BILA SABABU.JE INAWEZEKANA KUMPELEKA USTWAI WA JAMII?NAOMBENI MAWAZO.

Mpeleke tena haraka sana hilo linawezekana na utapata support ya kisheria haiwezekani yy kazi yake iwe kuzalisha tu then hataki matunzo,kuna sheria inambana mzazi ila wengi wetu hatuifaham hasa kwa suala la kusomesha hapo kitakachofanyika ni oda ya mahakama kwenda kazini kwake na kiasi flani cha mshahara kitakua kinakatwa ili kisaidia familia na yy atabaki na vijisent vyake kidogo vya pombe.
 
Nenda kwa bosi wake kwa siri ofisini kwake

Eleza tatizo hilo kwa ufasaha (hasa issue ya ada ya shule) ..usiongeze jingine tahadhari

Mwambie mwajiri akusaidie fedha ikatwe kwenye mshahara wa baba yako ipelekwa moja kwa moja shule

Toa ahaddi ya kupeleka riziti ya malipo..

itasaidia
 
Kwahiyo kuna thread huwa mnachaguwa, kuna za kujitoa akili na nyingine kama hii ndio unabeba akili zako unakuja nazo!!
 
kaka sina ajira kwa sasa.naishi kwa timing!

Kuna jamaa zangu mapacha baba yao alikuwa na tabia kama hizo. Siku mmoja wakamkamata na kumtia mijeledi ile mbaya. Mpaka leo kashika adabu tena yeye ndo kageuka kuwa mshauri mkuu. Chukueni hatua za mwanzo. Ikishindikana mnaweza kufanya kama hao mapacha.
 
sawa.ila hatua za mwanzo zimeshindikana zote.
 
Jikakamue najua unamuogopa maana wazazi wengi wa kiafrika wanatumia ukali kama ngao ya kutorekebishwa na watoto.
Hakikisha siku hiyo hajanywa, usije mshauri hilo suala huku amalewa!
Najua kuna watu watasema walee wewe kwakuwa umekuwa sasa yeye hela yake atafanyia kazi gani? na kama bado anafanya kazi huyo ananguvu zake...atimize wajibu wake....wewe unuweza kuwa unasaidia kidogo....maana hata wewe unahitaji kuwa na watoto na mke nani atakutuzia?

sawa mkuu.nakushukuru.
 
nenda kwa bosi wake kwa siri ofisini kwake

eleza tatizo hilo kwa ufasaha (hasa issue ya ada ya shule) ..usiongeze jingine tahadhari

mwambie mwajiri akusaidie fedha ikatwe kwenye mshahara wa baba yako ipelekwa moja kwa moja shule

toa ahaddi ya kupeleka riziti ya malipo..

Itasaidia

sawa nitafanya hivyo....
 
Back
Top Bottom