Nilichojifunza kutoka kwa Baba yangu

timeline

JF-Expert Member
May 19, 2015
458
2,396
Mambo niliyojifunza kutoka kwa baba yangu.
Naamini sisi wote hapa kuna mambo huwa tunajifunza kutoka kwa wazazi wetu yaani ( Baba na mama) na wengine hujifunza baadhi ya mambo kutoka kwa walezi wao.
Nianze kwa kuweka wazi mambo yafuatayo;-
1. Mara kadhaa katika ukuaji wangu nilidhani kwamba baba yangu hakuwa sahihi kwenye baadhi ya mambo.
2. Baba yangu alikuwa na taratibu ya kutupatia uhuru wa kueleza na hata kulalamikia baadhi ya maamuzi yake.
3. Miaka ya karibuni nimekuwa nikitafakari sana baadhi ya mambo ambayo nilijifunza kwa baba yangu na kugundua alikuwa sahihi sana.
4. Elimu ya shule inaweza kukusaidia sana kwenye maisha lakini elimu ya kijamii itakuepusha na mambo mengi.
5. Yapo baadhi ya mafunzo ambayo nimeendelea kuyafuata na baadhi nimeshindwa kuyafuata mara kadhaa.

Kwa sasa baba yangu ni ‘’retired officer’’ na ninashukuru kwamba yupo na afya njema kabisa.

Orodha ya mambo niliyojifunza kutoka kwa baba yangu-:
1. Hakuamini katika adhabu ya kudhalilisha ama uonevu.

Sisi kama watoto nyumbani tulikuwa tukifanya makosa mengi sana, tukiwa tunakuwa hasa umri wa kati ya miaka 7 mpaka 14 hapo. Baba alikuwa akituadhibu lakini hakuwa na adhabu za kudhalilisha, mara kadhaa angeweza kukuita na kukueleza ulipokosea na kukuacha uende mara nyingine alikuwa akikuita ndani na kukupatia adhabu yako na mara zote alikuwa akitumia bakora na sio kupiga makofi au mateke. Kuna siku kaka yangu mkubwa aligoma kuchapwa kwa adhabu ya kuchelewa huku akiwa na cheti kinachoonyesha alipita zahanati kwa ajili ya sindano za masaa, nilikuwa darasa la nne na kaka yangu alikuwa darasa la sita. Kesi ikawa kubwa na kaka yangu alirudishwa nyumbani na kutakiwa kuja na mzazi shuleni, ilipofika asubuhi tukatoka na baba kwa ajili ya kumpeleka shule kaka yangu na kwenda kusikiliza kesi. Tulipofika kulikuwa na majadiliano marefu sana na mwalimu, mwisho shule ikaamua kuwa kaka yangu achapwe bakora mbele ya wanafunzi kwa kuwa aligoma kwa jeuri mbele ya wanafunzi. Kaka yangu alikuwa tayari kuchapwa lakini baba aligoma na kuweka wazi kuwa kaka yangu hatachapwa kwa kuwa haoni kosa. Baada ya mivutano mirefu kaka yangu alirudi darasani, wiki mbili baadaye akahamishwa shule kwenda Shule ya msingi Boma. Nilikuja kugundua baadaye kuwa baba yangu haamini katika adhabu za kudhalilisha na za uonevu.

2. Tabia ya kuwa kusikiliza zaidi kuliko kuzungumza.
Tangu nikiwa mdogo moja kati ya sifa kubwa ya baba yangu ni kusikiliza zaidi kuliko kuzungumza. Huwa anazungumza mara chache sana na mara nyingi ni mwishoni baada ya kuwa umemamaliza kuzungumza. Nikiwa nakuwa hii ni moja ya tabia ambayo ilikuwa ikinichukiza sana. Mara zote niliona hii kuwa ni tabia ya kutokujali kwa kuwa mara chache sana alikuwa akikubaliana na kile unachokitaka. Kwa mfano inaweza kuwa unataka kwenda likizo kwa ndugu au jamaa, unaweza kuwa umepata ruhusa kutoka mama lakini baba akakataa na wakati mwingine bila kutoa sababu. Niliwahi kumuuliza sababu ya tabia hi miaka michache iliyopita nikiwa mtu mzima, alinijibu kwa kusema ‘’watoto ni wajanja sana, mara nyingi huwa wanaomba ruhusa ili wawe huru kufanya mambo mengine zaidi ya walichoomba’’.

3. Vikao vya familia

Tangu tukiwa wadogo ulikuwa ni utaratibu wa kawaida wa baba yangu kuitisha vikao vya familia yake (baba, mama na sisi watoto). Jambo kubwa katika vikao hivi ilikuwa kila mtu kueleza mahali ambapo ana tatizo, malalamiko na jambo lingine lolote. Jambo kubwa nilijifunza ni hali ya kila mtu kupewa uhuru wa kueleza na kufafanua tatizo lake ama pendekezo, hii imenisaidia sana kuwa na ‘uwezo mzuri wa kujiamini’’. Lakini pia kutoa uhuru wa mawazo kwa watu wengine kuanzia kwa mke wangu, watoto hata kwa wafanyakazi wenzangu.

4. Kuheshimu watu

Tumekuzwa na kufundishwa kuheshimu watu bila kujali wana hali gani katika maisha. Hili ni somo kubwa ambalo familia nyingi zimeshindwa. Baba yangu mpaka leo hii huwa anatwambia kuwa ‘’kuheshimu watu ni jambo la muhimu sana’’ hivyo ni tulizingatie.

5. Kutimiza majukumu ya kifamilia bila kutegemea kipato cha mama.

Wazazi wangu wote wawili walikuwa wafanyakazi (Wameshastaafu) kwa sasa. Nikiwa nakua mar azote nimemuona baba yangu akisimamia majukumu ya kifamilia bila kuhoji kuhusu mshahara wa mama. Sijui kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia lakini sikuwa kuona hata dalili za baba yangu kutaka mshahara wa mama utumike kwenye matumizi nyumbani. Nilipokuwa naoa, moja ya jambo aliloniambia ni kuwa timiza majukumu yako kama baba, ukihitaji msaada kwa mkeo basi iwe kwa lazima sana lakini epuka kutumia kipato cha mke wako kama hayupo tayari kufanya hivyo.

6. Kutoruhusu watoto kusoma shule za Bweni (Boarding School)
Kwa miaka ambayo mimi na ndugu zangu tuliosoma sekondari ilkuwa ni kawaida sana kwa wazazi kuwapeleka watoto shule za Bweni. Kipindi hicho shule kama Mwanga Secondary, Meta Secondary – Mbeya, Forest Seconday – Morogoro zilikuwa maarufu sana kwa watu wenye vipato vya kati kupeleka watoto wao. Mimi nilibahatika kuchaguliwa shule ya sekondari iliyopo mkoani Arusha kwa mshangao kabisa baba yangu alikataa nisiende huko. Na hivyo nikasoma shule ya Forodhani ambayo haipo kwa sasa. Nakumbuka kwa miaka ile shule za sekondari kwa O- level hapa Dar ilikuwa ni Azania Boys, Jangawani Girls, Kisutu Girls, Zanaki Girls, Kibasila, Pugu, Minaki na Forodhani. Nilikuja kugundua miaka mingi baadaye kuwa alikuwa akitaka tunakuwa karibu na kufuatilia maendeleo yetu ya kielemu kwa ukaribu tukiwa nyumbani. Katika naamini kwamba inawezekana mtoto akasoma boarding school na bado akafanya vizuri lakini baba yangu alihitaji tuwe nyumbani kila wakati.

7. Kuamua migogoro kwa haraka bila kuangalia athari kwa upande wake.

Nakumbuka nikiwa kidato cha kwanza baba alinunua shamba maeneo ya Buza Kanisani (Wakati huo Buza ni kijijini). Baada ya muda kukawa na mgogoro wa mpaka wa shamba, kijana mmoja alidai kwamba mpaka wa shamba la baba umeingia kwenye eneo lao akidai kuwa muuzaji wa eneo amekosea kuweka mipaka. Nakumbuka vizuri kuongozana na baba yangu kwenye kikao hiki cha usuluhishi, kilichofanyika chini ya mjumbe wa eneo hilo. Nakumbuka kikao kilipoanza mjumbe akamuuliza kijana aonyeshe mipaka sahihi ya shamba la familia yao, kijana akainuka na kuonyesha mipaka hiyo ikionekana kwa mipaka ya shamba la baba kwa eneo hilo ilikuwa ndani walau mita tano zaidi. Mjumbe akumuuliza baba yangu unasemaje, baba yangu akajinu akamwambia yule kijana ‘’weka mpaka mahali ambapo unataka mpaka uwe’’ jamaa akachomeka vipande vya miti, baba akamwambia kijana umeridhika sasa? Kijana akajibu ndio, mzee akamwambia mjumbe maliza kikao. Ilinishangaza sana shamba linamegwa kwa zaidi ya mita tano katika urefu wa mita arobaini na bado mzee anakubali? Miaka minne baadaye nikiwa kidato cha tano nakumbuka familia ya huyu kijana ilikuja kukiri na kurudisha kipande cha ardhi ambalo walidai kuwa ni lao.
Alikuja kuniambia baadaye kuwa hakuna haja ya kugombana na mtu kwa sababu ya ardhi. Kile ambacho umaweza ukakiacha ili ubaki na amani basi kiachilie maana amani ni bora zaidi ya magomvi na mali.

8. Kutotoza mahari kubwa

Familia yetu ni ya watoto wa kiume wawili na watoto wa kike watatu, dada zetu wote wamesoma mpaka level ya chuo. Wawili wana master’s degree na huyu mmoja ana undergraduate degree ni matumani yetu kuwa atafika mbali zaidi. Nikiangalia familia za ndugu wengine, mabinti wameozwa kwa fedha nyingi sana (Kiwango cha kuanzia Milioni 5 na zaidi). Lakini ilipofika kwa dada zangu baba alitaja mahari ndogo sana na nilikuja kugundua baadaye kwamba nia yake ilikuwa ni kutochukua mahari kabisa ila kwa sababu ya mila na ushauri wa wazee wengine ndio hawa shemeji zangu wakalipa pesa kidogo( sio zaidi ya laki tatu). Japo hawa shemeji zangu wanatoka katika familia ambazo zingemudu kulipa mahari hizi kubwa kubwa.

9. Usia wake katika ndoa.

Nakumbuka nilimwambia kuwa nataka kuoa miaka michache nyuma aliniuliza swali moja tu, huyo binti anakuvutia? Nikamjibu ndio. Akaniambia kuwa ukiachana na masuala mengine yote, mkeo anapaswa kukuvutia na kukupa hamu ya kuwa naye faragha. Akaendelea kusema kuwa iwapo kama hauridhiki faragha basi jua wazi ndoa haitakufurahisha hata kidogo. Hii imebaki kichwani mpaka leo na naona ukweli katika hili. Kama hakuna kuridhika kwenye faragha, ndoa inaweza ikabaki lakini mtaishi kwa mazoea na kufurahisha jamii. ‘’Exception katika hili ipo pale panapokuwa na changamoto ya kiafya baina ya wanandoa’’

Kingine ni kukaa mbali na wake za watu, huwa ananiambia hata mazoea tu hayafai.

10. Mtazamo wake kuhusu dini.

Nikiri kwamba tumekuzwa katika misingi ya dini na kufuata mafundisho husika katika maisha yetu. Baba yangu mara zote amekuwa akinisisitiza kujifunza na kuelewa kuhusu dini na kwamwe nisiruhusu kumuona kiongozi wa dini, mchungaji ama mtu yoyote yule kuwa daraja katika mambo ya kiroho. Huwa anasema sikiliza viongozi wa dini lakini tumia akili kufanya maamuzi.
Haya ni baadhi tu ya mafunzo kutoka kwa baba yangu.

Ni imani yangu kuwa sote tumejifunza vitu muhimu kutoka kwa wazazi wetu.
 
Thanks alot, ni mafundisho makubwa sana ili kuwe na mafanikio katika maisha.
 
Hongera mkuu acronomy kwa kulelewa na wazazi wazuri sana waliokuwekea mfano mzuri wa kuigwa na kukusaidia kuwa mtu bora sasa

Mengi mazuri nliyojiunza lakini naomba nikazie hasa swala laa kupeleka watoto boarding

Mkuu katika hili wazazi wako walikuwa sawa 100%

Boarding ni taasisi inayoongoza katika kuahribu watoto,eiza watoto kwa watoto wanaharibiana au wale ambao tunategemea watatwatunza watoto wetu wakiwa huko boarding,patrons,matron na walimu wenyewe

Sisemi watoto waliosoma day hawaharibiki,ila ukweli ni kwamba kuna utofauti sana kati ya mtoto anayeonana na mzazi kila siku na mwenye ukariibu na mzazi na yule ambaye anaonana na mzazi baada ya miezi mitatu mpaka sita.

Good lesson.
 
Hakika Baba yako ni mfano mzuri
 
Kwa kiasi kikubwa nafanana misimamo na kanuni za mshua tena karibia kote huko
Mi siamini kwenye kutumia kipato cha mke pia nachukia shule za bweni hasa single to the extent

Ila ambacho ningetofautiana na mzee ni hapo kwenye mtu kudhulumu kitu ambacho najua nina uhalali nacho hakika panachimbika
 
Mdingi alikuwa na hekima sana, pia nimejifunza kitu toka kwake hasa kwa kutopenda migogoro na kutojihusisha na habali za mshahara wa mke wake. Hali hii inasaidia kujua tabia za mke wako kama ni mbinafsi utamuona kwenye matumizi yake.
 
Back
Top Bottom