Nataka Nimshirikishe Mke Wake!!

Samehe 7 mara 70!! Fanya kama umepteza hivii hiyo hela na mungu atakuzidishia mara dufu!
 
Wanaume Tunalindana hata iweje, sasa wewe kumuhusisha Mke wake sio uanaume huo..

Cha kufanya jitaidi uonane na jamaa face to face umpe vidonge vyake kwamba anachofanya sio nawe una shida na hela uone atasemaje?

Ni bora kuhusisha marafiki wenzenu wa kiume wakamchane jamaa anazingua kuliko kumhusisha mke wake..

Wanawake hawatakiwi kujua mambo yote ya mumewe maana wenyewe tu hawajielewi. Achelewi siku kulianzisha na kuanza kumpiga madongo mumewe ana Kupa kopa kwa watu na kulipa halipi..

Kumwambia mkewe unakuwa ujamsaidia jamaa, wala kujisaidia mwenyewe zaidi ya kumdhalilisha rafiki yako wa siku nyingi..

Mda mwingine unafumba macho tu unasamehe.. Pesa kitu gani bwana, tunahonga sh ngapi kwa mwaka, Kunywa bia Bar, michango ya harusi etc..

ukweli mtupu...
 
japo sikubaliani na huo mfumo ila kunawakati unasaidia hasa pale mke anapokuwa anajielewa...ninamfano wa mzee mmoja akikopa au akifanyiwa kazi yoyote usipoenda kwa mkewe milele hela yako hutokaa upate. Lakini pia kwa upande mwingne mke hakuwepo siku mnakopeshana na pengne hajui hvyo kumshrkisha wakat huu ni kumbebesha mzigo usiomstahili..(chagua njia utakayopita ila chagua kwa busara)
 
Kama kweli ni rafiki yako kama ulivyosema huna haja ya kumdhalilisha kwa mkewe. Jiulize, kwani ukimwambia mkewe ndio hela zitapatikana???? Siku nyingine ukimsaidia mtu msaidie tu kwa kiwango kile ambacho hakitakuumiza incase mambo yake hayakwenda fresh kwa wakati.

Mkuu pesa ni pesa iwe nyingi au kidogo ukidhulumiwa zote zinaumiza sawa.
 
Watu wengi mliozaliwa kwenye fukuto la vyama vingi hamna uvumilivu hata kidogo...umeshamwita rafiki...umedeclare mmetoka mbaaaali na blah blah kibao..ulimsaidia kwenye matatizo (wakati mkewe akiongeza idadi ya wapiga kura) How come miezi mitano ukose ustahimilivu? Hebu kuwa mwanaume...
 
Absolutely mkuu unaeza usiamini miaka kama miwili bi mkubwa wangu alipata lidandas kazini akachukua kiinua mgongo chake na kuanzisha biashara ya kumsogeza maana yeye ndo baba ndo mama sasa kuna rafiki ake wa mda mrefu sana yaani walikua wameshibana haswa akampa mzigo wake wa kias kadhaa ampelekee sehem yule mama fedha kidogo tu ilimtoa imani akaitumia akawa hatak kulipa full kuzungushana mradi vurugu mechi, bi mkubwa alilamika jamani hadi huruma,cku zikapita miaka ikaenda ushoga ukafa akawa amesamehe hyo ela.kama unavosema malipo hapa hapa duniani juzi kat yamemkuta makubwa ya dunia na akawa hana msaada mwengine zaidi ya kwa bi mkubwa diiih bi mkubwa alimtolea nnje laiv bila chenga adi huruma ikaniingia nlijaribu kumbembelezea lakini wapi hili kila nkiliwaza naogopa sana kumdhurumu mtu mwenzangu!
unajua kwenye maisha, there is always NEXT TIME....mi naona achana naye we muache tu km ameamua kuingia mitini, ila naamini atakuja kukwama tena na bila haya atakutafuta..hapo sasa ndio umkumbushe hilo deni lako...pole sana mkuu.hiyo ni opsheni ya kwanza, ya pili mtishie kuwa utamwambia mkewe kuhusu suala hilo uone atafanyaje..
 
Sheria namba moja ya kukopesha siku zote unatakiwa kuikopesha hela usiyoihitaji..
 
Waungwana wamekupa ushauri mwingi wa busara, nachoongezea
mimi ni kuachana naye fanya kama umetapeliwa hiyo fedha ktk pilika pilika
zako mjini, kama ulipata moyo wa kusamehe nusu, na hiyo ilobaki samehe pia.
Pia kumbuka kudaiwa kunakera na kuna maelezo mengine kwenye simu
hayaeleweki usije kuta huyo jamaa yako kweli hari imekuwa tight sana kwake
kiasi kwamba siku mkikutana utamwelewa na kumwongeza zingine.
 
Back
Top Bottom