Nataka nikope Tsh milioni 10 SACCOS ninunue gari. Niambie uzoefu wako ulivyokopa pesa na kununua gari

kabunda88

JF-Expert Member
Nov 8, 2015
3,095
2,680
Wakuu mimi ni kijana tu under 35 yrs old kwa ajira yangu niliyobahatika nayo napata 1mil as take home, natamani sana kuwa na kigari changu cha familia maana nikipiga hesabu za elf 10 kila siku.

Za mishe za kuwapeleka outing wife na watoto wangu napoteza pesa nyingi sana mambo ya nauli ya Bolt, kwa sasa sina keshi ya kusema nitachukua ya kwangu kama 10 mil hapana ila kwenye kukopa hesabu zinakubali na kwa saving yangu kupata keshi yangu kama yangu itabidi kusubiri mitano tena.

Naombeni mnipe changamoto zitakazojitokeza baada ya kununua gari la mkopo hapo ukizingatia bado nimepanga, sijui kuendesha gari, sina leseni.

Thanks.
 
Ushauri wangu:

1. Nunua kiwanja cha 5m

2. Nunua gari ya 5m (utapata gari dogo lililopo kwenye hali nzuri).

Uiendeshe mdogo mdogo hadi umalize deni la kikoba.

Ukirudia mkopo wa pili, unajenga nyumba.(Size ya hiyo hela uliyokopa) uimalize uhamie.

Mkopo wa tatu uongezee na hela ya hiyo gari uliyonayo uagize gari zuri utakalo kwa pesa uliyonayo.
 
Wakuu mimi ni kijana tu under 35yrs old kwa ajira yangu nilio bahatika nayo napata 1mil as take home nataman sana Kuwa na kigari changu cha familia maana nikipiga hesabu za elf10 kila siku...
1,000,000 toa makato, toa gharama ya mafuta itakayobaki ndio utatumia wewe na hao wanafimilia wako. Kama kitakachobaki unaona kinawafaa endelea, kopa.
 
Wakuu mimi ni kijana tu under 35yrs old kwa ajira yangu nilio bahatika nayo napata 1mil as take home nataman sana Kuwa na kigari changu cha familia maana nikipiga hesabu za elf10 kila siku....

Kwanini usikope BANK? Saccoss wenywewe wanakopa BANK ndio wanakuja kukupa wewe, watakupiga na interest za ajabu, hiyo mili 10 unaweza kujikuta unarudisha milioni 70.
 
Upo Nyumba Ya Kupanga, Hujui Kuendesha Gari.

Unataka Kununua Hiyo Mashine Utagonga Wenzako Kazi Kubwa!

Chukua Millions 10 Tafuta Kiwanja Halafu Jenga Single. Baadaye Kiasi Kitakachobaki Ndiyo Uwaze Gari.

NB:: Pesa Ni Yako Mwisho Utakatwa Deni Mwenyewe, Amua Utakalo Ila Ukiwa Na Gari Utapata Heshma Huku Unaumia Taratibu
 
Maisha siku hizi yamebadilila sana, gari sio anasa tena now gari ni kama simu! Zile habari za kujenga kwanza huu sio wakati wake... Wapo watu wamenunua magari na badae wakajenga.

Mkuu wasikutishe! Vuta chuma mambo yatabalance tu ila kwenye uchaguzi wa gari ndio uangalie usije ukachukua chuma kitakachokutesa ila NUNUA GARI MKUU
 
Back
Top Bottom