Nataka Moyo wa hivi

Nataka Moyo wa hivi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,048
Reaction score
61,370
MOYO wenye AMANI na unaompenda MWENYEZIMUNGU hauna uadui ndani mwake na Wala hauna uadui na wengine.moyo wa kujitoa hautapeliwi kwa sababu uko MAKINI.Moyo unaoweza kujua ya kweli na ya UHAKIKA. Kuulanisha Moyo wako kutafungua milango yako ya fahamu na hatimaye macho yataona vizuri,masikio kusikia vizuri pua kunusa vizuri.

Moyo unaofanikiwa na kuridhikiwa Kiuchumi.Unakuwa na moyo mzuri mpaka umaskini kwako una kuwa Ni pambo kwako. Moyo wenye amani unaweza kuacha legacy na ukawa mtu uliyefanikiwa kutoka Tanzania yaani dunia nzima ikaja kutaka kwako maneno machache ili ipone kwa mfano matajiri watakuja kukutembelea na kutaka uwasaidie kwanini Wana pesa na hawapati usingizi au kwanini Wana kula vyakula na hawapati choo vizuri.

Huo moyo unaweza kuendesha vizuri mwili na mambo ya kiroho kiasi kwamba uwe Ni mtu wa kula kidogo kwa ajili ya uhai ukala chakula sahihi,ukaacha kuamini Kama uchawi upo Bali Ni ujinga wa Watu wachache wanaojisumbua wasio jua Nini maana ya mabadiliko ya kikemia waliokosa maarifa. Ukamcha MUNGU MWENYEWE ukaacha kuvuta sigara ukidhani Ni ufahari ukaacha kutoa mbegu kwa mkono kwani Kuna madhara Happ baadae ukaacha kunywa pombe ili isikupatie matatizo.

Utakuwa umejinasua kwenye mtego wa huu mfumo unaokata Kama mkasi unaoua Wengi sana karibia 70% ya Watu wananaswa kama samaki wanaliwa huku wametoa jicho.Moyo wenye amani una utambuzi hauna hofu unajua kabisa kifo Ni uhakika na Ni mwisho wa uhai kwa hivyo unajitahidi kuupa mwili kile inachohitaji kama ukitaka kukomaa BASI anaulisha madini chuma ambayo yapo katika mchicha.

Nataka Moyo wa kuweza kuongea mambo ya MUNGU muda wote ili niitafute hekima ambayo haitafutwi na Wengi na sio fedha ambazo zinagombaniwa na Wote.moyo wa kuniponya magonjwa haya yanayosumbua Watu Wengi.

JamiiForums-644317578.jpg
 
Back
Top Bottom