Nataka kwenda Zanzibar

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Ndugu zangu, nina mapumziko ya wiki mbili na sasa nimebakiza siku 6 tu. Ninataka kwenda Zanzibar kumalizia mapumziko yangu kwa muda wa siku 3. Pamoja nami, yupo shemeji/wifi yenu na mwanangu wa mwaka 1 na nusu. Mfukoni nimebakiwa na tsh 500,000(laki tano). Je, zitanitosha ktk mapumziko yangu huko Z'bar? Nategemea kufikia hotel na kufanya shopping ndogo ndogo. Mnaopajua vema, nielezeni. Kwa pesa hiyo, ninaweza kui-enjoy Z'bar?
 
hata kwa asiye pajua huko...kwa iyo nyomi ulioitaja hapo juu...HAITOSHI!...
 
Nataka kwenda Zanzibar lkn naogopa,
gari ya kwenye maji yaweza kuzama chin,
bora simba ale mimi c samaki jaman,
madumokii doi.
C maneno yangu yalikuwa ya Mr...
 
Sure thing. . .
Tafuta hoteli ambayo sio ghali sana (up to 70,000 a night) inayobaki ya usafiri (80,000), chakula, mizunguko kidogo na hako kashopping.
 
1. Nafuta hotel ya mjini ya stone town.
2. Shoping ndogo ndogo labda ununue halua, tende, ubuyu na spices lkn vitu vingine vingi bei ghali kwa hio hela uloitaja haitoshi.
 
Km anakaa siku 2 inatosha
BTW...Mzima BAGAH

mm mzima braza...hela bana iko kama ina mashetwani...ukichenj elf kumi mchana...jion hamna kitu...afu ndo wapo familia...tehe...zenj pabaya bana...aende akiwa fulu walet...maana!...
 
Last edited by a moderator:
1. Nafuta hotel ya mjini ya stone town.
2. Shoping ndogo ndogo labda ununue halua, tende, ubuyu na spices lkn vitu vingine vingi bei ghali kwa hio hela uloitaja haitoshi.

labda na tishet mbili za "jambo zanzibar" mwisho...
 
Kwani town taxi town trip ni bei gani? Hakuna lodge/hotel za bei nafuu kama tsh 30,000/day? Na bei ya vyakula minimum ni bei gani katika hotel za kawaida zisizo za kitalii.
 
Sure thing. . .
Tafuta hoteli ambayo sio ghali sana (up to 70,000 a night) inayobaki ya usafiri (80,000), chakula, mizunguko kidogo na hako kashopping.

watu mna hela ya kuchezea. Mimi natumia elfu10 hadi elfu15 kulala but yote hayo inategemea uwezo wako. Mi nikiwa nahiyo hela nitakesha bar nakunywa bia hadi asubuhi 50 elfu itakua haijaisha. maisha yalivyo magumu unampa mhindi 70000 akupe chumba cha kulala? mimi simpi. mwisho kabisa 20000/-
 
Kwani town taxi town trip ni bei gani? Hakuna lodge/hotel za bei nafuu kama tsh 30,000/day? Na bei ya vyakula minimum ni bei gani katika hotel za kawaida zisizo za kitalii.

Akifika achukue Hoteli za Malindi.. Zina kasuite ka-kishkaji,bei 50,000/-
Ni jirani na bandari na kituo cha polisi,na jirani na maduka..

Chakula sahani ni 4,000 kwa sehemu safi na reasonable... Jioni Forodhani panafaa kwa vitafunwa na kurelax..

Ila shopping.. Vitu ghali sana..bora watumie hiyo hela kwa ku-chillax tu!
 
watu mna hela ya kuchezea. Mimi natumia elfu10 hadi elfu15 kulala but yote hayo inategemea uwezo wako. Mi nikiwa nahiyo hela nitakesha bar nakunywa bia hadi asubuhi 50 elfu itakua haijaisha. maisha yalivyo magumu unampa mhindi 70000 akupe chumba cha kulala? mimi simpi. mwisho kabisa 20000/-

Vipaumbele vinatofautiana dubu.. Hata vipato navyo.. Na hobby nazo...

Wakati we unakunywa bia,mwingine pesa kama hiyo anatafuta demu,mwingine ananunulia bati au saruji,mwingine cheni ya dhahabu,mwingine Perfume,mwingine nywele..
 
We ushasema starehe yako pombe. . . wengine hiyo hatutumii kwahiyo tunafurahisha nafsi zetu kwa namna tofauti.
 
Vipaumbele vinatofautiana dubu.. Hata vipato navyo.. Na hobby nazo...

Wakati we unakunywa bia,mwingine pesa kama hiyo anatafuta demu,mwingine ananunulia bati au saruji,mwingine cheni ya dhahabu,mwingine Perfume,mwingine nywele..

Ni kweli. Hobbies zinatofautiana. Nakumbuka kipindi nikiwa Udsm nilikuwa kila nikipata boom nanunua atleast kitabu kimoja. Jamaa zangu walikuwa wakiniona mtu wa ajabu kidogo. Hata siku hizi, ofisin wananishangaa pindi ninapotumia karibu tsh 3000 kila siku kununua magazeti.
 
ww ni mnoko
 
Back
Top Bottom