Nataka kwenda Kenya Kutembea

Nyanya mbichi

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
3,716
2,215
Kam kichwa cha habari hapo juu nataka kwenda kumtembelea rafiki yangu Kenya .
Passport ninayo ,nina uwoga kidogo sijwahi kwenda nje ya Nchi, naomba muongozo napitia Mombasa.

Natakiwa kuwa na nini, Na nini sitakiwi kuwa navyo,maswali hapo uhamiaji.

Mwenye experience please.

.......update safari yangu ya Kenya.......

Namshukuru Mungu nimerudi salama safari yangu ya Kenya huko Malindi .

Niliondoka siku ya jumatano tar 2/3/ kuelekea kupitia Tanga border ya Horohoro-LungaLunga,tulifika Tanga Saa 13:02,safari ya border ikaanza nusu Saa baadae ,nilikua na mawazo mengi hasa suala la usalama wangu,alshabab hasa kwa kujitoa mhanga au wahuni wa Kenya wenyewe,kiukweli nilikua ninadhana mbaya kuhusu Kenya na Wakenya ingawa humu ndani kuna watu walinipa moyo sana na wachache walinivunja moyo.

Baada ya kupata utaratibu hapo border tukaendelea na safari mpaka custom ya Kenya inspection ikafanyika tukavuka SALAMA ila KONDAKTA akatupa tahadhari tufunge mikanda kwa kuwa tupo Kenya,na utaratibu wao asiefunga mkanda ndio mwenyekosa na sio dereva kama Huku Tanzania.

Tukafika Likoni kama by 18:00 tukavuka tukasubiria upande wa pili NAKUMAT hapo tulispend dk kama 50 gari yetu ikaja tukafika last destination Mwembe tayari ,nikafuata maelekezo ya mwenyeji wangu nikapanda tuktuk (BAJAJ) mpaka backstan Stand ya MALINDI,hapo nikakuta MAGARI [Matatu] kipanda au DALADALA hapa Tanzania machache ilikua kama 19:20 nikavuta subira maana abiria nilikua mwenyewe tu.

Dereva akachukua nauli kutoka kwa abiria kabla ya gari haijatoka (hakuna kondakta) express Matatu ilipofika Saa19:50 tulikua kwenye junction ya Nairobi,Malindi hapo Mombasa,safari ilianza dereva alikua vizuri seed na Makini ,nilikua na jirani yangu muongeaji sana nilikua nimechoka sana ila sikumujulisha mapema kama mimi ni mgeni ,nilimjibu niliyoweza kumjibu kwa kweli.Kwa kuwa alionyesha friendship tulivyofika Kirifi nikamuomba simu mwenyeji wangu afahamu nilipo bila hiyana nikamjulisha na ilipofika Saa 22:20 tulifika stage ya Malindi na yule jirani yangu alinikabidhi kwa mwenyeji wangu tukaenda nyumbani.

ilichojifunza:
1.Ferry hapo Likoni kuna vivuko vinne vyote vinafanyakazi
Kimoja cha MAGARI makubwa na Madogo,
Magari size ya kati na Abiria,
Magari Madogo na Abiria
Abiria tu.

2.Wanavuka bure hakuna malipo labda wenye magari kama wanalipia.

3.Huruhusiwi kupiga picha,nilipiga picha nikafuatwa na polisi wa ndani ya ferry akaniambia friendly kabisa kuwa sio ruksa kupiga picha.

4.Magari Yanatembea usiku kucha

5.Kuna ulinzi wa polisi na wanajeshi wakiwa na silaha njiani kila baada ya km kadhaa

6.Magari ya kwenda Nairobi wanakaguliwa abiria na mizigo yao

7.Wanapenda Wabongo sana na nyimbo zao wacheshi wengi wao watu wakujichanganya pia.

8.Pesa yao inathamani kuliko yetu,shilingi tano,kumi,ishiri inatumika.

9.Pikipiki na bajaji ni nyingi sana ,level seat kwa Matatu

10.Nakumat ulinzi wa kutosha sana inspection get la nje na mlango wa kuingilia ndani pia

11.Kupata laini kuna mchakato mrefu na ziko sealed,kama haiko sealed unashauriwa usinunue
 
Swali la msingi ni moja tu, passport basi!!
Mengine yatakua ni maswali ya nyongeza!!
 
Hutakiwi kuwaambia mlima Kilimanjaro upo kwenu,wakikuambia Olduvai George hiko kenya kwao na mwanadamu wa kwanza aliishi huko usibishe all in all i wish you a nice safari mkuu
 
Kam kichwa cha habari hapo juu nataka kwenda kumtembelea rafiki yangu kenya .
Passport ninayo ,nina uwoga kidogo sijwah kwenda nje ya Nchi naomba muwongozo napitia Mombasa .
Natakiwa kuwa na nini ? Na nini sitakiwi kuwa navyo,maswali hapo uhamiaji mwenye experience please.
we unaizomea samba au Yanga?!
 
Muhimu passport tu kuwa makini na Card ya njano km huna unapata hapo border buku tu km unaweza fatilia hata hapa home mengine utayajua kwenye border
 
Muhimu passport tu kuwa makini na Card ya njano km huna unapata hapo border buku tu km unaweza fatilia hata hapa home mengine utayajua kwenye border
Asante sana,mkuu Nashukuru sana sana card ya manjano ,acha niitafute iliko
 
Kam kichwa cha habari hapo juu nataka kwenda kumtembelea rafiki yangu kenya .
Passport ninayo ,nina uwoga kidogo sijwah kwenda nje ya Nchi naomba muwongozo napitia Mombasa .
Natakiwa kuwa na nini ? Na nini sitakiwi kuwa navyo,maswali hapo uhamiaji mwenye experience please.

Mbona unakuwa mwoga hivyo, Kenya ipo Afrika Mashariki hii hii na wanaongea Kiswahili.
 
Kam kichwa cha habari hapo juu nataka kwenda kumtembelea rafiki yangu kenya .
Passport ninayo ,nina uwoga kidogo sijwah kwenda nje ya Nchi naomba muwongozo napitia Mombasa .
Natakiwa kuwa na nini ? Na nini sitakiwi kuwa navyo,maswali hapo uhamiaji mwenye experience please.
Unaenda kutembelea OLDUVAI GORGE!?
 
Kam kichwa cha habari hapo juu nataka kwenda kumtembelea rafiki yangu kenya .
Passport ninayo ,nina uwoga kidogo sijwah kwenda nje ya Nchi naomba muwongozo napitia Mombasa .
Natakiwa kuwa na nini ? Na nini sitakiwi kuwa navyo,maswali hapo uhamiaji mwenye experience please.

Angalizo:
  • Huko Mombasa jihadhari, tumekuwa tunasikia mengi ya enzi za sodoma na gomora, uwe mwangalifu
  • Kenya wanatabia ya kujivunia vitu vya jirani zao, hivyo nawe wanaweza monopolize bila wewe kujijua
  • Nenda salama
 
Back
Top Bottom