Nataka kuweka umeme wa jua SOLA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kuweka umeme wa jua SOLA

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by LadySwa, Feb 29, 2012.

 1. L

  LadySwa Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2009
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wakuu karibuni 1 kampuni gani ni mabingwa wa kuweka umeme wa jua na kwa bei nzuri .2 Nahitaji taa 15,tv,redio na friji hii itagharimu sh ngapi?
   
 2. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Bei za Solar inategemea upo sehemu gani na solar yenyewe ya nguvu ipi!! zipo grade tofauti kwa matumizi tofauti. Mimi sina utaalamu nazo sana ila kitu kimoja ningekushauri katika kuweka taa wakati unatumia solar weka taa za grade A ama A++. hizi sijui kama zinapatikana hapa mjini kwetu. ila tu mimi nazifurahia sana kwani hazinyonyi sana umeme na matokeo yake unapata kutumia umeme mdogo kwa mwanga na kufaidika kwenye matumizi mengine. the same ukija kwenye mafriji na vyombo vingine vya umeme. Ila tu nikuonye bei yake sio ya chini. but kadri muda unavyopita it pays mkuu.
  Ngoja waje wale wataalam wa kudili na hivi vitu wachambue zaidi.
   
 3. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Kuna mwanajamvi engmtolera ambaye ansema anafanya biashara hiyo. Nilimtumia pm kuhusu suala kama lako lakini mpaka leo hajanijibu.

  Binafsi hata mimi nina madhumuni ya kuweka umeme wa solar kwenye nyumba yangu, maana inalipa baada ya muda. Uzuri ni kuwa tuna jua la kutosha sana na bei za vifaa vya solar zimeshuka. Ni jambo la busara kuweka solar hasa katika hali yetu ya Tanzania ambapo umeme hauaminiki na bei yake inazidi kupanda kila siku. Utumiaji nao wa majenereta ni mgumu kwa sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta, uchafuzi wa hewa na mazingira pamoja na kelele. Nawaomba wale ambao wana ujuzi wa matumizi ya solar hapa jamvini watuelimishe wengine kuhusu vifaa gani kwa mfano vinahitajiwa kwa matumizi tofauti ya umeme huo.
   
 4. Rashdind

  Rashdind Senior Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  chek na no. Hii 0763148588 kwa habar zaidi.
   
 5. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Dada,
  Kwa sasa nafikiri REX Investment ndo kampuni kubwa la mambo ya solar hasa kama uko DAR, nje ya DAR kuna vijana wanafanyakazi hizo na kwa bei nafuu. Kwa mahitaji uliyoyataja hapo juu itakugharimu around milioni 12 kama ukiwatumia REX investment. Kuna jamaa wengine pale Ubungo jengo la TRA/NIC karibu na Ubungo Hostel ndo walioweka Solar kwa babu Ambi kule Loliondo wao sijuwi gharama zao. Niliwahi kuwatumia email hawakujibu.

  Kwa kifupi ni kwamba gharama za solar ziko juu mno ukizingatia kuwa hazilipiwi kodi (Tax exempted). Nina quotation moja toka kwa Rex investment ingeweza kukusaidia kupata mwanga ila nimeshindwa kuiambatanisha hapa maana sikioni kile kitufe cha attachment. Nakutakia kila la kheri dadangu.
   
 6. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kuna jamaa wanaitwa umeme jua wako hapo ubungo milenium business park (karibu na kiwanda cha urafiki au mataa ya shekilango) waone kesho utapata jibu zuri. Nadhani wao gharama zao ni chini ukilinganisha na Rex. rex walinifungia umeme wa taa 6, TV na Radio miaka kama 5 iliyopita nilitozwa kama 2m na usafiri mpaka kijijini ulikuwa wangu. Kibaya ni kuwa system haijatengemaa mpaka leo. Kila nikiwambia wakawa wananiyeyusha mpaka warrant period ikaisha. Wakaniambia ninunue bettary nyingine nikabadirishe, nayo haikusaidia. Sasa hivi hakuna cha TV wala radio, ni taa tu. tena mtu akijifanya kuchaji simu muda mrefu, usiku mnalala giza. Kwa kweli customer care yao sikuipenda ndio maana nawachukia mpaka leo
   
 7. Mbaliche

  Mbaliche JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  gharama za sola zinategemeana. unapotaka ya kuwasha taa 15,tv na friji. inahitaji fundi aangalie ni taa ngapi za nje, na ngapi za ndani kati ya izo 15. tv ya aina gani atao tumia, size gani. vile2 friji. ndipo fundi atajua ni solar panel ya watts ngapi inatakiwa,bettri ya N ngpi inahitajika na inveter ya watts ngapi.
   
Loading...