Nataka kuweka kituo cha TV mwakani, ushauri tafadhali! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kuweka kituo cha TV mwakani, ushauri tafadhali!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mpeni sifa Yesu, May 25, 2010.

 1. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Waheshimiwa, habari za leo. kitu nitakachoongea hapa niko serious kabisa, na ninaomba wale wenye uelewa wanipe ushauri wao kuhusu hili.

  Nina mpango wa kujenga kituo cha Tv kuanzia mwakani, hilo ni wazo linalonisumbua muda mrefu sasa. kwasasa siko nchini, ila nitarudi home kuanza maisha ya home sweet home mwakani. kuna jamaa yangu alishawahi kunidokezea kuwa, ukitaka kuanzisha kituo cha tz Dar es salaam, kwasasa haiwezekani, ati unaambiwa "viwanja vimeisha", i am still ignorant hadi sasa, na bado ninafanya utafiti kabla ya kuingia kwenye iyo kitu, ndo maana nikaweka hili swali. hadi mwakani nitakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na kitu hicho bila shaka.

  hivi viwanja vinavyosemwa ni vya aina gani, na je, kama hivyo viwanja, sijui milango etc, vinahusuje kwa tv station za ki analogy na zile za digital...mainjinia tafadhali saidia hapa. JE, ITAWEZEKANA KUPATA NAFASI KUANZISHA KITUO HAPO DAR KWA SASA?

  pia naomba kuuliza, kisheria, taratibu zipi natakiwa kufuata A -Z kama kuna mtu anayefahamu hili. najua itabidi nimuone mwanasheria ili awe mwanasheria wangu kwa muda wote kuanzia kipindi hicho, na anaweza kunipa taratibu zote, isipokuwa ni bora kufahamu ili nijue kile mwanasheria atakachokuwa ananifanyia, nisiliwe hela mambo madogo pengine. nitashukuru sana kama nikipata mawazo yenu. asante.
   
 2. n

  nndondo JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Nakupongeza kwa mipango hiyo kabambe, kama ni social objective jamii inahitaji sand independent TV ambayo kwa sasa hakuna maana ukiangalia ITV labda walau lakini Mengi bado anajikomba kwenye system kwa hiyo kuna habari za muhimu kwa wananchi lakini kama zinaongelea udhaifu wa serikali yeye hataki kwa hiyo hazitolewi. Kuhusu viwanja inamaana masafa ama frequencies ambayo ni discretion ya Tanzania Regulatory Authority wameamua Dar basi sasa kumetosha mwenyekutaka aende mikoani. Hakuna kigezo chochote walichotumia kufanya maamuzi hayo zaidi ya ukiritimba wa kisiasa kwamba na mikoani kuwe na TV wanasahau kwamba hizo sio TV za serikali na za binafsi, bado sheria zao ni za state owned investments. Lakini kwa kuwa Tanzania yetu hii ya Rushwa hili lisikusumbua naamini ukiwa na kitu kidogo utaweza tu kupata. Hakuna mtu atakayekwambai A-Z kwa kuwa kwa nchi isiyokua na utaratibu na iliyotawaliwa na Rushwa procedure ziko flexible. La msingi na la kitaalamu ni moja, huwezi kuanzishiwa biashara na mtu wewe ukiwa umekaa nje huko unaagiza, hizo ni ndoto na udhaifu wa watanzania wengi waliokaa nje na kutegemea porojo na udanganyifu wa watu wanaojikomba kwa serikali wanaojiita diaspora, hawawaambii watanzania ukweli kwamba wao wamefanikiwa kwa connections ambazo ni very subjective wanawadanganyeni kwamba mkifika tu mambo poa opportunities kibao huku wakijua kabisa kwamba playing field haiko level na iko very subjective,negatively kwa wazawa. Nakusharui uje kwanza ufanye utafiti ukiwa hapa na kufanya hizo hatua za mwanzo wewe mwenyewe, wapambe watakumaliza ama mtagombana kwa sababu ambazo ni genuine.
   
 3. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  actually, nina uchungu sana na tz, na sitakujakuwa na wazo la kutafuta uraia mwingine nje..hivyo narudi home. nashukuru kwa ushauri kuwa itabidi nisiwe mbali...kitu yenyewe itakuwa mkononi mwangu, and nitakuwa bongo muda wote. cha kushangaza ni kwamba, ina boa sana mtu kwenda kuanzisha tv mkoani, selikali yenyewe imeshindwa kuweka hata dodoma tu, inang'ang'ania dsm...kipenda roho kwangu ni kwamba mikoani ingekuja kusambaa tu badaye, ila makao makuu yawe dsm ndo ulaya ya tz bila upinzani.....maadam ni independent, napenda iwe Dsm tu, na si mkoani, huo ndo uliuwa uchaguzi wangu binafsi. i hope God will make it.

  kwahabari ya rushwa, hicho ndio kitu kigumu sana kwangu kufanya, na ndio kinachonisumbua...huwa sitoi rushwa kabisaaa, kwangu ni dhambi na mwiko hata kama ingeruhusiwa vipi na selikali. hivyo nitakuwa mvumilivu kufuata taratibu hata kama zitachukua miaka kadhaa. naamini kwa Mungu yote yanawezekana, hata bila rushwa.
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hongera mtumishi, nakutakia yote mema. natamani ningekuwa nafahamu hayo mambo ningekwambia, lakini mimi pia ni ignorant wa issue hizo. by the way, nimependa signature yako. Mungu akubariki sana.
   
 5. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2010
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Mimi ningekushauri ufungue hio TV popote pale nchini na isiwe tu Dar....maana sio sababu ya TV lazima uiweke Dar...kama unavyodai kuwa una uchungu na TZ basi popote pale nchini panakufaa besides Dar imejaa
   
Loading...