Nataka kusema Happy mother's day, lakini...

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,645
2,000
Nataka kusema "happy mothers' day" lakini napata kigugumizi.

Mama halisi ni wachache sana na ni wazee sana (miaka 60+) hata ujumbe wangu hawatausoma wala kuusikia.

Hawa wa siku hizi siyo akina mama ni WANAWAKE WENYE WATOTO. Mama gani huyu;--

1. Hataki kumnyonyesha mtoto kuogopa matiti yatalala?
2. Hajawahi kumbeba mtoto mgongoni akapandikiza upendo kwa mtt kupitia joto na jasho?
3. Anavaa vinguo vifupi kiasi kwamba mtt anaona masinema ya kikubwa kila mara?
4. Amejipulizia mipafyume na kujipaka mafuta hadi ananuka badala ya kunukia? Inamharibia mtt uwezo wa kunusa na kutambua kupitia pua.
5. Yuko bize kutoa koments kwenye magroup ya Whatsapp mtt akilia h/girl anaambiwa ampe matoi.

Akina mama wanatoweka duniani kwa sasa. Ni bidhaa adimu. Ni endangered spicies.

Tusaidiane kuwajenga akina mama katika familia. Umama siyo kuzaa ni zaidi ya kuzaa.
 

MimiT

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
602
500
Kama umeoa na hizo sifa zote hapo anazo mkeo pole sana.
Mengi uliyoyasema yana ukweli.
 

nra2303

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
2,738
2,000
Nani kama mamaaaa aaaaaah*2 (Cristian Bella voice)
Uliyosema mdau hapo juu ni kweli na hili linasababishwa zaidi na malezi mabovu na utandawazi. Akina mama wanatakiwa kuwafunda mabinti zao miaka nenda rudi na sio wasubiri mpk siku ya kichen party au baada ya kuolewa.Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi.
 
Top Bottom