Nyetk
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 1,648
- 1,696
Leo ni siku ambayo duniani kote tunawakumbuka na kuwaenzi mama zetu. Sote tumezaliwa na mama zetu. Hata kama wapo wachache ambao kwa bahati mbaya, kwa sababu hii au ile hawakuwahi kuonja upendo na mahangaiko ya mama zao, lakini ukweli wa jumla ni kwamba yako mambo ambayo bila mama zetu yasingefanyika, kubwa ktk hayo ni kutubeba tumboni hadi tukafikia umri wa kuwa tayari kuwa hai bila kuwa matumboni mwao.
Malezi yanaweza kuyafanywa na mtu yeyote mwenye mapenzi mema, lakini “role” ya mama (mzazi au mlezi) kwa mtoto ni “indisputable”. Sisi tuliozaliwa na kukulia vijini nyakati hizoo hili ni kweli Zaidi. Naomba wana JF wote muungane nami:
1. Kumpongeza mama yangu mzazi Dorotea na mama zetu wazazi na walezi wote
2. Kuwaombea pumziko la Amani mama waliotangulia
3. Kuwatia moyo mabinti wanaoogopa majukumu ya kuwa “mama”
4. Kuwasamehe akina mama waliofanya makossa makubwa ya umama kwa watoto wao
5. Kulaani vitendo vilivyo kinyume na hurka sahihi ya umama kama utoaji mimba, kutupa na kutelekeza watoto, nk.
6. Kulaani akina baba wanaowatesa, kuwatumikisha na kuwatelekeza mama wa watoto wao
7. Kulaani watoto waliowatelekeza wazazi wao, hasa mama zao
8. Kulaani serikali zote duniani zisizoweka mipango sahihi kwa ajili ya afya na ustawi wa mama na mtoto, na
9. Kila mtu ampongeze mama yake hapa kwa kumtaja jina
Kila ifikapo Jumapili ya pili ya mwezi Mei, mataifa mengi duniani husherehekea Siku ya Mama.
Ni siku ambayo inamkumbusha kila mmoja wajibu wake kwa mama yake. Kwa wale ambao mama zao wametangulia mbele za haki, huitumia siku hii kuiwaombea na kuwashukuru kwa kujitoa kwao kuwalea watoto wao.
Kila mmoja hutafakari namna mama yake alivyomleta duniani, kumtunza, kumlea, kumlinda, kumsomesha na hata kumfanya awe hivyo alivyo leo.
Mama ni mwalimu mkuu katika makuzi ya mtoto. Wakati mama akifanya hayo yote, wapo baadhi ya watoto wakishakua na kuanza kujitegemea huwa wanamsahau mama.
Upo usemi kuwa mama anaweza kuwa na watoto wanane, akawalea na kuwasomesha wote kwa usawa lakini anapozeeka, watoto wale hushindwa kumtunza mama yao vile inavyostahili huku kila mmoja akimtegea mwenzake.
Wengi wamewatelekeza mama zao vijijini. Wanavutana nani awajibike kwa ajili ya mama yao wakati yeye alifanya kwa upendo. Bila shaka mpaka leo hii akisikia habari za kuhuzunisha za watoto wake, huchukua jukumu lake kwa kuwaombea.
Wapo kina mama watu wazima wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini, watoto wanarushiana mpira kila mmoja akimtaka mwenzake abebe jukumu la kumhudumia.
Katika kipindi cha wiki nzima, mtoto anaweza kwenda mara moja tu kumtazama mama yake huku akiwalazimisha wenzake nao waende.
Lakini mama alimlea kila mmoja kwa kuwa mlinzi wake saa 24 kwa miaka yote mpaka akafikia umri wa kujitegemea.
Tunapaswa kuadhimisha siku hii kwa kujiuliza maswali! Umemfanyia nini mama yako, yupo wapi na je, anapata mahitaji muhimu wakati huu ambao wewe umeanza kujitegemea?
Lusia Mwakalinga anasema siku zote ana hakikisha mama yake anapata mahitaji muhimu kwa kuwa umri wake mkubwa.
“Mama yangu ni kama mtoto wangu wa kwanza, nikilala, nikiamka katika vitu vinavyonijia kichwani na yeye yumo,” anasema Mwakalinga.
Kumbuka mama yako ni zaidi ya kumpa zawadi na mahitaji mengine, hata kumjulia hali ni sehemu ya kumtunza.
“Hivi nilivyo na nitavyohitaji kuvipata, vimewezekana kwa sababu ya mama yangu,” Abraham Lincolin

Happy Mother’s Day!
NANI KAMA MAMA?