Kwa kweli hofu niliyoipata wakati naenda kupima Ukimwi miaka 5 iliyopita ni zaidi ya ile niliyoipata utotoni nikiwa na Aka kama 6 hivi nilipopata taarifa kwamba nitahitajika kwenda kukutana na mkasi kwa ajili ya kutoa ngozi kwenye Mtwangio wangu...Ilikua ni kwa Kairuki na ndio kwanza nilikua nimepata ajira yangu ya kwanza hapa town HR wa hiyo Company (ni ya kigeni) akasema anahitaji FULL MEDICAL CHECK-UP REPORT kufika hospitali nikapima kila kitu ila Ngoma nikaacha ...nikarudi faster kwa HR nikamkabidhi na kwa vile muda ulikuwa umekwenda ikabidi nisepe Maghetoni kupumzika.Kesho asubuhi HR huyo akasema kuna kitu cha muhimu kuliko vyote nimesahau hehehe Kupima NGOMA..nikazuga zuga pale job weeee mwisho nikapiga moyo konde maana hata Comfirmation Letter nilikua sijapatiwa.Ikabidi nirudi kwa Kairuki kufika nikaambiwa vp unahitaji ushauri wa DR kwanza kabla ya vipimo nikajibu hapana Basi wakanipima nikawa nasubiria jibu kwenye benchi....Mara yule jamaa wa Maabara huyo na vikaratasi anasoma majina akaita Rural Swagga....x9 hivi mimi kimyaaa ...nikanyanyuka nikaingia Bar flani hivi ipo nyuma ya Kairuki Buddha Blue nikapata kinywaji kuweka Ubongo sawa kumbe ndio kwanza nazidisha feelings .....nikakumbuka Game zote nlizocheza kuanzia O level mpaka University....Ila pombe noma nikajisemea potelea mbali watu wangapi nawajua wana Mdudu na wanakula Gudtyms to the fulest.:clap2:Basi nikarudi moja kwa moja mpaka Kairuki nikaulizia majibu yangu...Jamaa akauliza tena vp unahitaji kumuona DR kabla ya kupata majibu nikasema hapana Basi jamaa akafunguka akanipa hongera kwamba niko safi kabisa...Nakumbuka nilikua sijawahi panda Teksi kwa muda mrefu ila that day nilipanda Tax mpaka job nikampatia HR majibu yake....From that day nimepunguza kama si kuacha kabisa Ngono zembe.