Nataka Kuoa Nifanyeje

Katika Masha yngu nimetokea kuchukia Anasa tena sana. na kipindi hiki nimefikia umri ambao nilazima niowe...nimemaliza masomo kazi sina. nimehangaika sana..ila huu huangaika nipate chochote na ninachopata kinanitosha mimi mwenyewe binafsi. naombeni ushauri nifanyeje?

Kama unafeel kuoa oa tu, akili mbili sio moja my broda! mtasaidiana tu, ila kumbuka wewe ni kichwa na unatakiwa kujiandaa hivyo sio kutegemea fadhila za utakaye muoa.... go for it my broda go go go
 
Kuoa siyo pesa, omba Mungu akupe mke mwema mnayependana, kuheshimiana, kuvumiliana wakati wa hali zote furaha, shida. Usisahau kumshirikisha Mungu kwenye hili jambo maana ni gumu kupata mke mwenye roho ya utu, unyenyekevu. Wengi wakisikia huna kazi watakukatisha tamaa sana, ila kuonekana unaendesha gari zuri, unaamka alfajiri kuwahi foleni kwenda kazini ndiyo sifa au umaarufu wa kukupa kibali kuoa la hasha!

Amka zako mapema weka mchicha wako kwenye toroli anza kutembeza mchicha ni kazi nzuri/kipato kizuri kishicho na masimango, limit ya kufanya kazi nyingine. Nakushauri kama una mchumba endele ana process zako za kuoa. Ikikaribia tu PM tukuchangie upate mke msaidiane kwenye shida/raha zanu

Mungu akupe hekima na muongozo mwema kwenye hili swala lako la kuoa.
 
Katika Masha yngu nimetokea kuchukia Anasa tena sana. na kipindi hiki nimefikia umri ambao nilazima niowe...nimemaliza masomo kazi sina. nimehangaika sana..ila huu huangaika nipate chochote na ninachopata kinanitosha mimi mwenyewe binafsi. naombeni ushauri nifanyeje?

hivi suala la kuoa/kuolewa ni lazima?!
Kwanini uoe wakati unajua mazingira yako ya kiuchumi hayajakaa vizuri?
Sidhani kama umri mkubwa ndio iwe sababu kubwa ya wewe kuoa.
Jipange kwanza.
 
oa mambo ya kufikilia mtakula nini mtavaa nini anajua mungu mwenyewe kama wew hulali na njaa na mkeo atakula hicho hicho
 
Katika Masha yngu nimetokea kuchukia Anasa tena sana. na kipindi hiki nimefikia umri ambao nilazima niowe...nimemaliza masomo kazi sina. nimehangaika sana..ila huu huangaika nipate chochote na ninachopata kinanitosha mimi mwenyewe binafsi. naombeni ushauri nifanyeje?

...Unamuamini Mw'Mungu?

kama unaamini, wewe oa tu. Milango ya heri itafunguliwa.
Mke, watoto, kila mmoja kaandikiwa riziki yake.

Tunajikwaza wenyewe kwa kuhofia kesho itakuwaje ilhali siku hazirudi nyuma.
Piga moyo konde. Chumbia, oa, na fanya kila jambo kwa kadri ya uwezo wako.

Kila la heri.
 
kwa maelezo yako unataka kuoa ama kuolewa

Katika Masha yngu nimetokea kuchukia Anasa tena sana. na kipindi hiki nimefikia umri ambao nilazima niowe...nimemaliza masomo kazi sina. nimehangaika sana..ila huu huangaika nipate chochote na

ninachopata kinanitosha mimi mwenyewe binafsi.

naombeni ushauri nifanyeje?

ushauri gani unataka nini kama kinakutosha mwenyewe mwenzako wa nini na kama si hivyo uoni wataka utoshelezwe weye??
 
Una tembo card master card? lol. Oa tu mwaya ila mshirikishe sana Mungu ili akujaalie mke mwema atakayekubali kuanza na wewe from the scrach. Ila mkitoka usije ukam damp! Kila la kheri brother.
 
Kajisemea Saida Karoli, mapenzi kizunguzungu.

Haya wewe oa tu sasa hivi, ila kama haujawa tayari ndo utajua matumizi ya neno Talaka.
 
Mkuu huu mpango wakuoa bla kujpanga mara nyingi unazfanya ndoa zwe ndoano.
mwanamke kaumbiwa kutunzwa kwa malazi,mavazi,makaz nk.
nafkir ni vzuri ukijpanga katika jinc utakavyoweza kutoa hzo huduma kabla haujaamua kuoa.
zaid kila la kheri
 
Katika Masha yngu nimetokea kuchukia Anasa tena sana. na kipindi hiki nimefikia umri ambao nilazima niowe...nimemaliza masomo kazi sina. nimehangaika sana..ila huu huangaika nipate chochote na ninachopata kinanitosha mimi mwenyewe binafsi. naombeni ushauri nifanyeje?
Omba wazee wakupeleke jando
 
Kama hauko tayari subiri mkuu kamasi lisije likakutoka kwa kushindwa kutimiza majukumu. Ndoa inaleta mambo mengi kama unaishi chumba kimoja utahitaji kuongeza viwe viwili maana muda c mrefu j au kay atazaliwa nae atahitaji yaya ambaye hamuwezi kulala nae rum moja. Usiwasikilize hao wanaoleta habari za mungu kupanga ishu ni kusababisha tu na kuMake kipato bila hivyo life itaendelea kuwa chenga tu..
 
Cha kufanya, kapite kwanza viungo vyote kama vinafanya kazi.

Katika Masha yngu nimetokea kuchukia Anasa tena sana. na kipindi hiki nimefikia umri ambao nilazima niowe...nimemaliza masomo kazi sina. nimehangaika sana..ila huu huangaika nipate chochote na ninachopata kinanitosha mimi mwenyewe binafsi. naombeni ushauri nifanyeje?
 
mmmmmmmmmh we kaka mbn kama unajiongezea matatizo hebu vuta subra kwnz plz "mvumilivu huwa mbivu"
 
Kuoa hakuna fomula wala muda,ni vitu vinakuja vyenyewe tu ndugu, watu kibao ukiwauliza walipanga waoe lini watakuambia nilipanga nioe mwaka,au kipindi flani nikajikuta nimewahi kabla ya nilivyopanga, mwingine nilichelewa tofauti nilikuwa nimepanga . Mi mwenyewe niliwahi tofauti na nilivyokuwa nimepanga. Hivyo ikifika huo wakati mkuu utakuta umeoa tu aotomatically, haiitaji ushauri,tena ikifika hutasikiliza la mtu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom