Nataka Kuoa Nifanyeje

Mkulima1

New Member
Apr 26, 2011
3
1
Katika Masha yngu nimetokea kuchukia Anasa tena sana. na kipindi hiki nimefikia umri ambao nilazima niowe...nimemaliza masomo kazi sina. nimehangaika sana..ila huu huangaika nipate chochote na ninachopata kinanitosha mimi mwenyewe binafsi. naombeni ushauri nifanyeje?
 
  1. Naomba kujua umri halisi, hiyo ina determine sana kuweza pewa mawazo yatakayo kulenga. Mana kufika umri wa kuoa ni perspective ambayo wanajamii wanaangalia factors kibao mpaka mtu kuambiwa sasa ni umri wa kuoa; mwingine anakua 27, labda 32 or even 40. Hivyo kwa mawazo yangu ningeomba utaje umri.
  2. Usichanganye anasa na kua na girlfriend/boyfriend. Kuna watu hawapendi kabisa anasa na wana watu wao wa karibu ambao wamesomana na wamezoeana kwa mda mrefu to the extent hata mmoja wao (awe wa kike/kiume) akikwama au kuachishwa kazi wanapeana support mpaka mambo yanaporudi katika msatari tena.
 
Katika Masha yngu nimetokea kuchukia Anasa tena sana. na kipindi hiki nimefikia umri ambao nilazima niowe...nimemaliza masomo kazi sina. nimehangaika sana..ila huu huangaika nipate chochote na ninachopata kinanitosha mimi mwenyewe binafsi. naombeni ushauri nifanyeje?
Kama unahisi uko tayari kuoa basi ndio wakati wakuoa yenyewe huo. Ila mtakula nini ndugu yangu? kama unacho kipata kinatosha kwako mwenyewe basu hakikisha utakae muoa awe na pato linalo mtosha yeye na ikibidi liwe juu zaidi ili mweze kusave angalao kitu chochote kwa ajili ya mtoto. Usichoke kutafuta kuboresha hilo pato lako na pia ongea vizuri na potential wachumba waijue hali yako ya kiuchumi.
Good luck!
 
Usioe kwasababu unataka kuoa...oa kwasababu umempata unaetaka kumuoa!!

Mpaka umeomba ushauri hapa jua kwamba hauko tayari!!
Japo sijajua umri wako naomba nikwambie kwamba huna sababu za kukimbilia kuoa kama bado hali yako haisupport kua na mke.Jua kuoa kunazaa familia...sasa ukikimbilia kuoa huku hata banda la kukaa linasumbua utaipa hiyo ndoa ''DOWNS '' nyingi mapema !!Jiweke sawa kihali na kifikra huku ukitafuta mchumba kama bado hujapata...ukiwa tayari hutohitaji ushauri wetu..mwenyewe utajua wakati umefika na hali inaruhusu.
 
Utaoaje na huna kazi?? Unatafuta matatizo wewe?? Wanawake wa raha na shida wameisha, wamebaki wa RAHA tu! Jipange sawa, sawa!
 
Subiri kama unaona bado kipato ila ningependa pia kukujulisha tu kuwa hata wale mashoe shiner na wabeba mkokoteni wana familia zao na wanajitahidi kile kidogo sana wakipatacho kugawana na wanafamilia zao. kwa hiyo naamini kama umekamia kuoa utayaweza tu, ila huna haja ya kukimbilia huko ki hivyo Unless your above forty
 
Tukiwa JKT kuna adhabu tulikuwa tunapewa ya kunyoosha mikono mbele kisha unakunja na kukunjua ngumi,maumivu yake ni balaa.Sasa wakati wa kukunja na kukunjua vidole maafande walikuwa wanatulazimisha tuimbe 'matatizo njoo,matatizo njoo,matatizo njoo......'wakimaanisha eti hayo maumivu tumeyakaribisha wenyewe.Mkulimaone tafakari.
 
Nalo wazo,Tembo mastercard unayo?
Hivi hili tangazo mbona huwa lina maana ndogo sana? kwa bank kama ile ilibidi wawe na tangazo lililoenda shule, ina maana watu wote kuoa lazima wawe na pesa? au mabinti waolewe sababu ya kitu fulani, nahisi watu wa marketing wanabidi waliangalie upya. ni mawazo yangu tu
 
Katika uhalisia CRDB walichemka sana,ndiyo matatizo ya kuiga matangazo mobile phones service providers.
 
mimi ninachoona unaweza kuhangaika mpaka ukafa hujafanikiwa kupata unachotaka kupata, inamaana hutaoa?????????

huwezi jua lbd mke utakaye mpata atakuja na baraka gani.

ila kbl hujafanya hivyo VAA NAIVERA UMUULIZE BWANA!!! NAYE NI MWAMINIFU ATAKUJIBU LA KUFANYA
 
Utaoaje na huna kazi?? Unatafuta matatizo wewe?? Wanawake wa raha na shida wameisha, wamebaki wa RAHA tu! Jipange sawa, sawa!

Oa bwana watu wasikukatishe tamaa, mtagawana kilichopo, kwani unayemwoa si atakuja kula alichokuwa anakula kabla hamjakutana? Au unataka kuoa goal keeper? Ndoa ni kusaidiana. Na maisha yote huanzia chini, na atakayekukubali wakati huu ndiye mwanamke wa maisha yako. Usisubiri hadi uwe na nyumba na gari.
 
Katika Masha yngu nimetokea kuchukia Anasa tena sana. na kipindi hiki nimefikia umri ambao nilazima niowe...nimemaliza masomo kazi sina. nimehangaika sana..ila huu huangaika nipate chochote na ninachopata kinanitosha mimi mwenyewe binafsi. naombeni ushauri nifanyeje?

Mkuu, kuoa/kuolewa siyo anasa. Ndoa siyo mialiko tunayopeana na gfs wetu kwenye hotel, au sehemu za starehe na jioni mtu anarudi kwao. Ndoa ni zaidi.
Mkuu oa kama umri umefika na unae unayempenda. Hiyo haitakuwa anasa ila itakuwa ni baraka toka kwa Mungu.
Wengi wamefanikiwa sana wakiwa kwenye ndoa zao, na mbaya zaidi wengi wakifanikiwa wanawasahau wake zao.
 
matangazo mazuri yapo bank M bana..utafikiria mara elfu ujue ana maana gani..i love them,plz crdb do something

Hivi hili tangazo mbona huwa lina maana ndogo sana? kwa bank kama ile ilibidi wawe na tangazo lililoenda shule, ina maana watu wote kuoa lazima wawe na pesa? au mabinti waolewe sababu ya kitu fulani, nahisi watu wa marketing wanabidi waliangalie upya. ni mawazo yangu tu
 
matangazo mazuri yapo bank M bana..utafikiria mara elfu ujue ana maana gani..i love them,plz crdb do something
Mimi niliishajiuliza mara nyingi sana hawa M Bank matangazo yao wanatengeneza wapi maana yanavutia na pia creativity ni nzuri sana
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom