Nataka kununua TECNO C8 CAMON

mnyongeni

Senior Member
Dec 6, 2011
141
24
Kuna simu mpya naziona madukani ni za tecno c 8. Vipi ubora wake? Nilichovutiwa zaidi ni uwezo wa camera 13 Mega pixel. Na bei nimezunguka naambiwa hata 280,000 napata. Naomba wanayoijua vizuri tuidiscus uzuri wake na madhaifu yake. Pia vipi kuhusu tecno c5 na boom 7?. Pia kuna simu nyingine bora zaidi naweza pata kwa bei ya 250000 - 300000?.
 
Kwa kifupi hapo simu mzuri kwa hizo ulizotaja ni c5 ambayo inatumia 4g 3g na 2g
Hiyo c8 inatumia 3g Na 2g tu
Pia kuhusu ubora zote zipo sawa
 
Attachments

  • 1456069924230.jpg
    1456069924230.jpg
    39.1 KB · Views: 115
ongeza kidogo kuna watu wanauza lg g2 humu kwa around 350,000

kama huwezi kuongeza subiria kidogo xiaomi redmi 3 itatua muda si mrefu kenya ni powerfull kushinda simu yoyote utakayopata kwa bei hio.
 
Kuna simu mpya naziona madukani ni za tecno c 8. Vipi ubora wake? Nilichovutiwa zaidi ni uwezo wa camera 13 Mega pixel. Na bei nimezunguka naambiwa hata 280,000 napata. Naomba wanayoijua vizuri tuidiscus uzuri wake na madhaifu yake. Pia vipi kuhusu tecno c5 na boom 7?. Pia kuna simu nyingine bora zaidi naweza pata kwa bei ya 250000 - 300000?.
kwa tecno mp13 hapo kiuhalisia itakuwa mp2.kama vipi linganisha picha yake na picha iliyopigwa na galaxy s4 ambayo ndio ina mp13 utaona tofauti kubwa sana
 
Achana na hizo simu mkuu..ongeza pesa kidogo upate simu nzuri
 
Mkuu ushauri wako ni wabusara sana lakini wakati mwingine mtu huangukia kununua tecno na simu zenye hadhi sawa na tecno kwasababu ya upatikanaji wa simu ambazo wengi mnashauri humu jukwaani changamoto ni kwa wafanyabiashara wetu wa tz hasa sisi wa mikoani utakuta unapitia karibu kila duka simu yenye thamani kidogo ni tecno ndio wamezijaza na makampuni mengine yasiyojulikana sasa unakuta zipo simu nzuri zenye bei sawa na uliyo nayo lkn unaipata wapi hilo swali la kwanza ukibahatika kuipata basi huipati kwa bei uliyodhani unakuta ipo juu na hasa kwenye maduka haya ya mitandao ya simu.
Kwahiyo wakuu si kila mtu unakuta alipanga kuwa na simu yenye ubora mdogo bali na soko nalo lina mlazimisha mtumiaji kununua bidhaa za namna hiyo.
 
Tecno ni simu fake! Kainunue at your own risk!
Natanguliza pole kwa sababu unaweza ukawa bado mjinga yani ujaelimika kujua neno fake na low quality, tecno sio fake inaweza kuwa ni low quality kwa baadhi ya model fulani ya matoleo yake
 
Kama kuna mtu ana simu tajwa aniuzie. Iwe kwenye hali nzuri kwani namnunulia mtu zawadi. Bei niliyojipanga nayo ni LAKI NA NUSU (150,000/=) TU...
 
Tecno ni simu fake! Kainunue at your own risk!
Kukariri majina ni kubaya sana, kwahiyo ukikutana la Samsung, Lg nk hizo ndio original. Angalia sana utakuja ulizwe mjini kujifanya unajua.
Hujui hata kutofautisha fake na low quality.
 
kwa tecno mp13 hapo kiuhalisia itakuwa mp2.kama vipi linganisha picha yake na picha iliyopigwa na galaxy s4 ambayo ndio ina mp13 utaona tofauti kubwa sana
Camera ya C8 ni 13MP hata kama quality yake haifikii samsung au sony ya 13mp lakini bado huwezi kulinganisha na camera yoyote ya 2MP.

Kama umeitumia hii simu inatoa picha nzuri kuliko lumia 535 yenye 5MP
 
Kuna simu mpya naziona madukani ni za tecno c 8. Vipi ubora wake? Nilichovutiwa zaidi ni uwezo wa camera 13 Mega pixel. Na bei nimezunguka naambiwa hata 280,000 napata. Naomba wanayoijua vizuri tuidiscus uzuri wake na madhaifu yake. Pia vipi kuhusu tecno c5 na boom 7?. Pia kuna simu nyingine bora zaidi naweza pata kwa bei ya 250000 - 300000?.
Camera ni nzuri, screen size inaridhisha, ina flash mbele na nyuma. Speed na ram ni nzuri.

Weakness;
Sound quality sio njema, headphones si quality.

Ni bora kuliko kununua simu used ya toleo la zamani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom