Nataka kumuoa huyu single mother

Nataka kumuoa huyu single mother

Uko naye kwa miaka miwili mkiwa hohe hahe sasa mmenyanyuka hadi kuwa na upande mzima wa nyumba bila shaka naye kachangia sana. Yuko vizuri kwenye yale majambo yetu. Ana akili za kimaisha za kukuhimiza ununue kiwanja. Za kuambiwa CHANGANYA NA ZAKO!
Nimeshamfanyia visa vya kila aina ili anichoke lkn naona ameniganda tu. Haniombi ela na hana usumbufu wa kijinga, ananipa uhuru ninaoutaka.

Anajiheshimu na ananiheshimu na kwenye uwanja wa futi sita yuko vizuri ile mbaya, anajua kuifinyia kwa ndani

Nina miaka miwili naishi nae lkn sijawahi kwenda hata kujitambulisha kwao. Tulianza maisha ya kulala ktk kigetto tu chenye kagodoro tunatandika chini mpaka sasa tumepanga upande mzima wa mjengo na kuna kiwanja amenihimiza nikinunue tuanze ujenzi..

Kasoro pekee ni single mother, mtoto wake yupo analelewa na bibi wa upande wa baba. Msela aliyemzalisha hana mishe ya kueleweka anapiga debe stendi, ni dizaini ya wale wana wanaovaa majinzi ya kuchanika chanika na kunyoa viduku. Anadai walishaachana..

Wazoefu mliooa single mothers njooni mnipe muongozo..
 
Kwa Mimi jibu langu bado ni no
Usioe single mother
Mateso yapo mbele
 
Kwa Mimi jibu langu bado ni no
Usioe single mother
Mateso yapo mbele
Yeyote utakaeoa mateso yapo mbele, so kama huyu walau ana vigezo vingine hasa akili ya maisha, mi nadhani jamaa aoe tu. Unaeza oa ambae sio singo maza lakini ni kicheche hatari na akili ya maisha hana.
 
Ushaishi na mwanamke miaka miwili, halafu bado hujui kama upo tayari kumuoa au lah!

Nigga, what's wrong with you!
 
Mapenzi ni ya wawili. Fata moyo na akili yako inavyokwambia mkuu.

Wife material ndio hawa hawa wanaotuzunguka, hakuna wengine.
 
Hakuna bi mkubwa anayependa kijana wake aoe single mother. Nafikiri wanajua nini kinaweza kutokea mbeleni ndio maana wanapinga
 
Kiongozi swala la mapenzi linauwanda mpana sana. Amani ya moyo wako inasamani sana kuliko ushauri utakaopewa humu. Hakuna mahali sheria ilipitishwa kwamba ukimkuta binti anamtoto basi hafai kwa ndoa! Kama anakisi zifa na tabia unazoitaji muoe tu mkuu wanawake wanamna hiyo Mungu anakuletea mara moja tu.
 
Nje ya mada: Hilo jina lako limenifanya nicheke kwa nguvu sana nikakumbuka ile video😂😂😂😂
Nilikuwa sijalisoma jina lake nimecheka kwa sauti, mangi hanyanyuki na kwa msimamo wa huyu jamaa single mother ataisoma namba.
 
Back
Top Bottom