Nataka kumuoa huyu binti ila tabia zake zinatetemesha sana

Bado anapambana kukupenda uenda akili inataka ila moyo wake kihisia unagoma anakukubalia kuhusu kukuzalia,kuishi nk na wewe akiamini uenda akizaa au kuishi na wewe anaweza jenga upendo wake kwako tatizo moyo wake umegoma hapo anapitia wakati mgumu.

Nb: hiyo inaitwa anayenipenda simpenda.
 
Huyu bibie amakufaa sana.

Muoe huyo bibie anakufaa sana. kila mtu na mapungufu yake hawez kukamilika 200%

Kama vyote ulivyotaja anafanya mi naona iko sahihi hilo la kutokutafuta ni ishu ndogo kwa sisi tunaotafuta ndoa.

Hao wanawake uwa wanaambiwa ni mwiko kujipendekeza kwa wanaume labda ndo kinachomsumbua.

Hata wangu nae alikuwa na tatizo kama hilo ila niligundua wazazi ndo wanaongea nao kuwa, mwanaume si mtu wa kutegemea labda ndo anahisi akijipendekeza sana mwishowe utamuacha.

Ila kwangu huko sahihi atabadilika si ishu ya milele hiyo
Sawa mkuu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mtoa mada ukisema anakupenda na hakutafuti mpaka umtafute yeye unakuwa unamaanisha nini hasa, tuambie nikitu gani kinakuonesha anakupenda ikiwa hakutafuti ???

Nafikiri Kuna haja ya kuanzishwa mitaala ya kufundisha mahusiano shuleni.

Nikupe maana ndogo ya MAPENZI, mapenzi ni hisia yaani mtu kumuweka akilini tunaita moyoni, ukimpenda mtu akakaa moyoni kweli Kuna matokeo yanayojionesha/jitokeza nje automatically moja wapo kumpa ATTENTION.

Mtu unayempenda kweli haijalishi cheo chako, ubize wako, tabia yako nk lazima umpe ATTENTION kama kumtafuta kwa simu (Call/texts), kutaka sikia sauti yake, kumpa kipaumbele nk na haya ndio mapenzi yenyewe sasa wewe unasema hakutafuti HOW COME mtu awe na hisia na wewe asikutafute.

Mimi naijua saikolojia ya mapenzi, Mimi binafsi nikimoenda mwanamke kutokumtafuta inakuwa adhabu kwangu yaani inapita siku inaisha nalala bila kumoigia au kum-text Kuna kitu Kama kinanifurukuta moyoni siwezi na ikipita siku 4 mujawasiliana unaanza kuona upweke na hii ndio inakuwa kwamtu mwenye hisia na wewe Sasa wewe unasema eti anakupenda lakini hakutafuti NIgga you need to learn what's is mapenzi aise.

Relationship:
tunakuja kwenye mahusiano, mahusiano ya kiplmapenzi ni kitu Cha wawili lazima energy itoke kwa wote wawili kuhakikisha penzi Kama chombo kinaenda ukiona unamtafuta wewe tu yeye hakutafuti hio ni SHOBO na sio mapenzi RAI yangu kianzia Sasa jitamkie mwenyewe kuwa "Mimi ni mjinga na sitafanya tena huu ujinga" ukitoka hapo weka deadline ya week moja Kama ujaona text/call yake futa namba zake na penzi liwe limeishia hapo.

Usije mwambia mwanamke asiyekutafuta muyajenge eti kwanini hunitafuti mpaka nikutafute Hilo ni suala la kihisia zaidi na huyo Hana hisia na wewe Kama mpenzi wako hakutafuti hakupi ATTENTION nini maana ya mapenzi sasa mapenzi ni unatoka kazini stress zimejaa unaona text imeingia 'mambo my' kichwa kinaanza kupoa Moto stress zinashuka Sasa wewe kushusha stress mpaka u-hustle INSANE.

Kuwa mwanaume mzee u deserve better unahitaji kuambiwa
"umemkaje baby"
"kazi zinaendaje"
"usisaau kula eeh"
"ukifika salama niambie"

Sasa Kama mimi nipo single nakosa hizo packge na wewe upo kwenye mahusiano tunatofauti gani mzee kumbuka kuingia kwenye mahusiano Kuna RISK umeingia kutongoza, kumpa mtu attention, kuwa tayari kutoa pesa ukiomba Sasa unapata Nini.

Wanaume ATTENTION ni kitu Cha thamani sio tunampa kila mwanamke Kuna wanawake wanakesha na kuomba kupewa attention ile Hali tu ya kuwa Kuna mtu anamlenda, anamjari, anampa kipaumbere nk hili mwanamke kupewa attention huyo mwanamke Hana sifa ya kupewa attention unachofanya si misingi ya kiume mpe attention anaye deserve kupewa attention.

Mzee tafuta mwanamke achana na huyo mtu haraka inatosha ujinga uliofanya ujinga ni malamoja lakini Mimi nishakwambia Sasa acha.
Sawa mkuu.. nitaacha ndugu yangu.. na hapo ndipo ninapo jiuliza kwanini anipende alafu akilini mwake sipo yani na fikiria sana, alafu kingine ni kwanini haniombi hela kabisa yani haombi hata iwaje sasa kweli patakua sawa hapa.

Au kunamtu anaye muhudumia nakumliwaza

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Jaribu kumuambia kuhusu tabia yake kwamba haufurahishwi nayo then subiri utekelezaji wake
 
Habari ndugu zangu,

Katika kundi la wanawake zangu kadhaa wa kadha nilionao, nimejikuta nimeangukia kumpenda binti anayetokea na kukulia maeneo ya Mlima Meru huku Arusha ndugu zangu.

Nipo nae kwenye mahusiano ya wastani lakini nimejikuta moyo unanisukuma sana kumuoa ila nikikumbuka mienendo yake na choka kabisa.

Yupo hivi ndugu zangu.

1. Ni binti mwenye umri wa miaka 23-25 na nimlokole haswa ila aliwahi kuwa na mahusiano ya kavunjika anasema mwanaume alimuacha tuu bila yeye kujua sababu ni nini, japo aliingia kwenye mahusiano mengine jamaa wazazi wakazingua na baadae mimi hapa ninae songa naye ndugu zangu.

2. Anapoabudu pana umbali wa si chini ya kilometa kumi kutoka anapoishi , japo huko kuna nyumba za ibada ila ndiyo hivyo.

3. Wazazi wa huyu binti waliwahi kumkataa mwanaume aliyetaka kumuoa huyu binti hapo nyuma kutokana na sababu binafsi za wazazi wake binti.

4. Wakati naanza nae mahusiano alionyesha kutokuniamini na baadae akaamua kukubaliana na mimi nikamuweka rasmi kwenye list yangu.

5. Hanitafuti kabisa mpaka ni mtafute mimi na nikisema nipige kimya tunaweza maliza hata mwezi ndugu zangu, yani ni ukweli usiopingika hanitafuti kabisa labda nianze kumtafuta mimi na siyo vinginevyo.

6. Alishawahi kuniambia mimi ndiye mwenye maamuzi ya kumuoa au kutomuoa maana yeye hajui nawaza nini kichwani mwangu.

7. Alishawahi kunambia ghafla tu hataki tena nyumbani kwao ili aje tuu geto tuanze maisha japo nilimjibu kuwa atulie asiwe na haraka nataka kumuoa hivi karibuni kwa kufata taratibu husika na halali ila baadae aliniambia alikua ananipima tuu.

8. Aliwahi kuniita majina ya mahaba mara moja tuu ila tokea hapo hajawahi niita tena kwa namna yeyote ile. Yani ikitokea tumewasiliana inakua ni kama kusalimiana na mpita njia tuu yani.

9. Hajawahi kuniomba Hela kabisa binti wa watu wala chochote kile huu ni ukweli na waambieni.

10. Yupo tayari kuwa mke wangu ila naona ni mgumu sana asee ikitokea nimesafiri anaweza asinitafute hata mwaka eti, kwajinsi tu alivyo kama mimi sitomtafuta wa kwanza.

11. Yupo tayari kua mama wa watoto wangu.

12. Yupo tayari kuishi maisha yoyote yale kwa mujibu wa maelezo yake na jinsi alivyo alivyo tuu ukimuona.

13. Hawezi kuvaa suruali au nguo yeyote fupi kwake hataki kabisa anapenda kuficha sana mwili wake.

Ndugu zangu nishaurini hapa nioe au niendelee kuongeza namba ya wanawake nilio nao wakuu maana naona kabisa hapa nikioa na ikitokea nimesafiri sijui kama atanitafuta huyu hatakujua huko nilipo naendeleaje kama mimi nisipo mtafuta.

Asanteni wakuu.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Huyo hajaokoka,kajificha kwenye kichaka Cha kuokoka.
.Binti aliyeokoka seriously hawezi kusema anataka kuja kwako muishi pika pakua.
 
MZALISHE MTELEKEZE AONGEZE LIST YA MASINGO MAZA... Sio kila mwanamke anafaa kuolewa wengine tuwachezee tu...
KATAA NDOA UISHI KWA AMANI UIMARIKE KIUCHUMI
 
Huyo ni wife material. Usiacha dhahabu ipite. Hao wanaokutafuta, hawakutafuti peke yako, wanajaribu huko na kule,: Yaani hawajatulia.
Huyo kajiwekea ulinzi asijitegemee kwako sn ili hata ukimtema asiweweseke. Ila huyo ndio anafaa, vitu vingine utamfundisha akiwa ndani, hao ni watii; na ni bidhaa adimu. Utakujanishukuru baadae.
Boraa wee umuambiee.
 
Sawa mkuu.. nitaacha ndugu yangu.. na hapo ndipo ninapo jiuliza kwanini anipende alafu akilini mwake sipo yani na fikiria sana, alafu kingine ni kwanini haniombi hela kabisa yani haombi hata iwaje sasa kweli patakua sawa hapa.

Au kunamtu anaye muhudumia nakumliwaza

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kheeeeeh? Angekua anaomba pesa ungeona mdangaji, haombi bado ni tatizoo, duuuh binadamu bhana
 
Ngoja azubae mwishowe atapata kunguru wa Zanzibar
Mtoa mada nimechungulia nyuzi zako mbalimbali, nimeona unateseka sana na wanawake.

Unasema kuwa hakuombi hela, je huwa unajiongeza na kumpa hela? Au unakula buyu tu.
 
Back
Top Bottom