Nataka kujitegemea nahofia hatima yangu

Nov 23, 2020
58
96
Nataka kuondoka nyumbani sina pakuanzia

Nahitaji kujitegemea wandugu mwenye connection ya kazi yoyote anipe sichagui kazi yoyote nipo tayari

Nina umri 24
Nipo. Mkoa Tanga
Nina diploma ya electrical engineering

Nafanya kazi yoyote ile nipate angalau mtaji wa kuanza kujitegemea.

Mawakala wa kazi karibuni pia
 
Hongera kwa kulifikiria hilo, ila hatua ya kwanza ni kuondoa hofu na kuwa tayari kujisimamia wewe mwenyewe.

1. Kaa andika vitu ambavyo ni muhimu kwanza katika kuanza kwako kupanga

(godoro lolote ilimradi liwe ndani ya uwezo wako hata ukiweza mkeka ni sawa,

Jiko (unaweza kuanza kutumi mafiga kutegemeana na eneo ulilopo kama kuni zinapatikana ili kuepuka gharama za mkaa au gesi kwa mwanzoni)

Vyombo vile muhimu

Kiufupi focus kwenye mahitaji ya kula na kulala tu suala la kuvaa achana nalo.

2. Piga gharama za kodi kwa miezi sita na usichukue chumba cha gharama 10k, 20k, 30k najua huwezi kosa (ndani ya muda huo utakuwa umeongezeka upeo wa kufikiri hivyo utakuwa nafasi nzuri kuendelea kupambana kama kweli unamaanisha)

3. Tafuta kazi yoyote acha kufikiria sana kuhusu professional yako, yaani ukipata kazi ya professional yako sawa, usipopata fanya kazi yoyote (tembea mtaani)

Unaweza shirikisha ndugu au jamaa wa karibu kuhusu malengo hayo na yeyote atakayeguswa anaweza kusaidia chochote na kikakusaidia kuanza, jambo la msingi ni uanze wewe kupambana itakuwa rahisi wao kushawishika kukusaidia.

Ukifanikiwa kupata hiyo pesa ya kodi na kununua au kupata vitu muhimu vya kuanzia, ondoka nyumbani na uende ukapange na usiangalie nyuma kujiuliza sasa nikishapanga na pesa ikaisha nitaishi vipi, ONDOA KICHWANI HILO.

Mwanajeshi ukishafika uwanja wa vita, choma boti zote na uwe na mawili tu, KUSHINDA AMA KUFIA VITANI na huwezi kusjindwa kama una nia ya dhati kupambana.

Mpaka hapo sasa uwe na hekima ya kupanga maisha yako na kufikiria namna gani unaweza fikia malengo yako mengine katika maisha, ila cha kwanza toka kambini (kwenu), ingia vitani (kapange ujitegemee).

Nakuhakikishia Mungu atakukutanisha na watu ambao watakuwa ni daraja la kufik huko unakotaka.

Kitu cha kwanza ni kujitoa.

Kama huna moyo wa kujitosa na kutumia ushauri huu tafadhali endelea kukaa nyumbani ukisubiri kazi yenye mshaara mzuri.

Ila kama una nia, TOKA NENDA KAPAMBANE, nina umri kama wako na nina familia nalea na chuo sikumaliza nategemea kurudi na kujisomesha mwenyeweila nilijilipua na sasa najiona MWANAUME KWELI.
 
Kama ni technician nadhani unaweza kuwa unawafahamu wakandarasi wa umeme (Electrical Contractors) hapo Tanga ambao huwa wanakuwa na kazi za wiring unaweza kuwatafuta ukapata hata kibarua.

Kuna mafundi pia ambao sio wakandarasi ila wana majina (kazi). Pia unaweza kuwa ukiona nyumba inajengwa unamtafuta mwenyewe unamwambia uwezo wako wa kufanya wiring kidogo kidogo unatengeneza jina hutakuwa unakosa hela za kukuwezesha kujitegemea.
 
Kama ni technician nadhani unaweza kuwa unawafahamu wakandarasi wa umeme (Electrical Contractors) hapo Tanga ambao huwa wanakuwa na kazi za wiring unaweza kuwatafuta ukapata hata kibarua.

Kuna mafundi pia ambao sio wakandarasi ila wana majina (kazi). Pia unaweza kuwa ukiona nyumba inajengwa unamtafuta mwenyewe unamwambia uwezo wako wa kufanya wiring kidogo kidogo unatengeneza jina hutakuwa unakosa hela za kukuwezesha kujitegemea.
Niunganishe mkuu
 
Back
Top Bottom