Nataka kujinyonga kwa kukosa kazi

Nataka kujinyonga kwa kukosa kazi

Mwimbo mpya wa mwana FA...silalamiki sina viatu wenzangu hawana miguuu...sikiliza vizuri..msomi gani akili inawaza maroroso
 
Mkuu ushajinyonga?nimecheka eti.ukute hiyo kozi yako ya kibitoz !ila usijali sikuhizi hata kujiokotea machupa tu ajira tayari! Tatizo mnachagua sana wasomi nyie!!
 
Mtoa mada ananipa asubuhi ya furaha leo,nimecheka sanaaa! l wish tungekutana jioni nijaribu kukuunganisha na

mataita wa mujini wakupe kazi,wakati huo tunapata juice bariidi,nitakwambia imewekwa sumu ya panya then nione reaction

yako!! maneno tu hayo ya kukata tamaa,chezea kufa wewe!!

Usikate tamaa,pambana ndg!
 
Tafuta VCD ya kwaya ya kinondoni revival kuna wimbo unasema ''usijiua kaka,ooh mwambie Yesu'' ukimaliza kusikiliza leta mrejesho hapa.
Na mimi nakushauri usijiue.Mimi nilimaliza zamani kidogo nimejenga miaka ya karibuni na kununua gari
hakikisha ndoto zako zisiwe zile za kwenda mwezini kwa miguu.kuwa na ndoto zinazotekelezeka,lkn ukidhani kusoma ni kuwa na nyumba kubwa na gari zuri kirahisi rahisi,utajiua kweli.Tulia tafuta vikazi vidogo vya kukupa nauli ya kutafutia kazi kubwa.Usidharau kazi kisa una degree itakugharimu maisha,jishushe na MUngu atakuinua.ni hayo.
 
Uliona wapi anayejinyonga anatangazia uma wewe?. Kukosa ajira si mwisho wa maisha na maisha lazima ujue ni ups and downs hyo ni down yako ups itakuja tu ntumainie Mungu.tofauti tu hapa ni kiwango cha uvumilivu na mind set yako bila kuajiriwa huwezi kuishi?
 
Kama unatafuta ajira zipo hapa duniani,ahera hakuna ajira yoyote.Umewaza ujinga kama watu wapumbavu.Ushauri wangu ni kwako ni kwamba mrejee muumba wako maana yeye ndiye akupae nguvu za kupata utajiri.
 
Back
Top Bottom