kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 17,349
- 21,449
Ndugu wakazi wa Dar,
Nataka kuja kutembea Dar lakini bado nina wasiwasi na zile tabia za kale bado zipo au zimekoma, za watu kugombania mabasi na kuingilia madirishani,polisi feki kukwambia wanatafuta namba za pesa zilizoibiwa,kanyaboya au jitu kuvaa vizuri na mafaili lakini mchana kutwa wapo pale posta ya zamani wamezunguka sahani ya kashata na kahawa,wale wasanii wa kukuchora wewe ulivyo,yale majihuni ya kuibia watu mifukoni kwenye daladala je wamebadilika,naogopa kipindi cha kutalii kwenye hayo mabasi nisije kosa nauli ya kurudi kijijini kwetu.