Nataka kuitembelea China

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Ni shauku yangu kufanya hivyo! Ikimpendeza Mungu, nitaenda huko mwakani.

Lengo la safari ni utalii wa kuangalia fursa za kibiashara, hasa bidhaa zinazopatikana kwa wingi huko zinazohitajika sana Tanzania. Na, kama wasemavyo, "mwenda bure si sawa na mkaa bure", huenda katika hiyo ziara, nikabaini bidhaa ninazoweza kuzipeleka huko kutoka Tanzania.

Ingawa najua China ni kimbilio la wafanyabiashara wengi wa Tanzania, naamini nikienda mwenyewe huko kunaweza kuniongezea "kitu" cha ziada katika kufanya maamuzi ya bishara ya kufanya. Nimelenga kufuatilia upatikanaji wa bidhaa zifuatazo:
1. Nguo

2. Simu

3. Computers - laptop na desktop

4. VIFAA vya electronics kama redio, tv, n.k.

5. Vifaa vya umeme

6. Furnitures

7. Vifaa vya ujenzi.

8. Stationaries

9. Mapambo

10. N.k.

Sijawahi kwenda huko, wala kusafiri nje ya bara la Afrika.

Pamoja na hayo, ninakusudia kusafiri peke yangu bila kuwa na mzoefu wa "kunishika" mkono. Naamini kufanya hivyo kutaniongezea kujiamini zaidi.

Naomba kuuliza kwa wazoefu mliomo humu jukwaani:
(A). Kuna usumbufu wo wote kwenye upatikanaji wa visa?

(B). Ni maeneo gani muhimu kuyatembelea kwa mtu anayetaka kufanya ziara kama hiyo?

(C). Safari kama hiyo inaweza kugharimu kama kiasi gani? Tiketi ya ndege (economy class), malazi kwenye hoteli za kawaida (siyo za kifahari), chakula, na mizunguko ya hapa na pale ndani ya China kwa muda usiozidi wiki moja. Napaswa kuwa na alau milioni ngapi kwa mahitaji ya safari nzima kutoka Tanzania hadi China na kurudi Tanzania?

(D). Shirika gani la ndege linatoa huduma nzuri?

(E). Hali ya usalama ikoje kwa wageni? Kuna tatizo la ubaguzi wa rangi?

(F). Ni maeneo yapi yanatembelewa zaidi na Waafrika wengi, hasa Watanzania? Kwa nini?

Nitafurahi nikikutana na Watanzania huko, au alau watu kutoka East Afrika.

(G). Ushauri mwingine wo wote ufaao!

Asante🙏
 
Kila la kheri na safari NJEMA!
 
Back
Top Bottom