Nataka Kuishi Masaki

Nataka Kuishi Masaki

Mungu akutangulie kwenye kutimiza ndoto zako Mkuu. Ukipenda kuishi Masaki au Osterbay jipange. Viwanja vinapatikana kwa kuwavua watu andaa 1- 3 Billion. Nyingi ya Nyumba zamani zilikuwa za Serikali lkn ziliuzwa kwa Watumishi enzi hizo wengi wao kwa sasa wanastaafu au wamestaafu hivyo wanavuliwa sana. Wengi pia walishauza, ingawa wakati serikali inawauzia kuna kipengele kwenye Mkataba kilizuia kuuza nyumba hizo.
Kuhusu Nyumba za kupanga Masaki zipoo kuanzia BnB, Bungalow, Apartment nk nk ispokuwa kodi jipange kuanzia 2.5-10M kwa mwezi.
Kuishi masaki kwa sie waswahili ni mateso si kitoto, hakuna genge la nyanya, hakuna kibanda cha Mangi, hakuna kituo cha boda boda, hakuna ruti ya dala dala nk nk nk
Mbona hayo uliyoyataja yapo...mama ntilie, vigenge, boda wapo sana...

Bila kusahau barabara mbovu na madimbwi huko masaki
 
Kwa mfano maeneo yote ya Cholle Road, Sea Cliff nk nambie boda boda iko eneo lipi?
Cholle Road boda wapo bachresa pale zinapopark daladala...
See cliff boda utapata pale mwisho karibu na paparotti..tena pale paparotti kuna hadi kitua maalumu cha boda na bajaji...
Kule karibu na havoc kuna kituo cha boda
Kimsingi viko vingi..

Masaki sasa hiv ni pa hovyo...japo bado matajiri wapo sana
 
Hope wazima wakulungwa

Natamani kuishi masaki, masaki pananivutia sana lifestyle yake haina kufatiliana haina umbea yani kila mtu anaishi kivyake natamani siku moja nije kumiliki ardhi masaki, sisi watu wa madeals masaki panatufaa sana kuishi maana hatutakagi kumchomongo

Watoto wa #masakilife waje humu [emoji16]
Katoka maeneo yaliyokuwa yanaongoza kwa shida ya maji ni Masaki sijui hilo yatizo lilishamaliziika?
 
Labda masaki ya Chanika
Mkuu mara ya mwisho kutembelea masaki lini?

Sidhani kama kuna sehemu yenye barabara zenye madimbwi na viraka kama masaki..

Unabisha hakuna mama ntilie? Basi nitakuwa nabishana na MTU ambaye hajui masaki vzr

Nenda pale paparotti kuna mama ntilie kibao karibu nyumba za canaddian village tena wanauza mihogo na chakulla kabisa

Nenda pale havoc mbele karibu na shoppera...kunakuwepo mama ntilie pale

Nenda pale manzese masaki karibu na ubalozi wa namibia kuna mama ntilie

Njoo huku fitness kuna mama ntilie na boda kibao

Na maeneo mengine mengi tu
 
Huko sisi tunakwenda kutumia tu
Ngoja tukajichanganye na wastaarabu
Wenzetu

Ova
Kiranga
20231227_135351.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom