NATAKA kuingia Bongo movie ila Pakupitia sipaoni.

Story fupi kwa haraka
Katika kijiji cha Inama Inuka kulikuwa na Jama mmoja Jina lake Ndole, Jamaa Huyu alikuwa katili sana, Kwani Alikuwa anawatesa watu bila Huruma watu wasio na Hatia yoyote, Jamaa Ukimsalimia anakutusi Usipomsalimia anakupiga, (dawa yake ilikuwa ukimuona unamuepka) Mtu huyu alikuwa na Mtoto mmoja mdogo, na Mama mtoto huyo alikuwa alishaondoka kwa sababu ya Ukatili wa huyu jamaa ((nakumbuka alikuwa anakuja kwetu na kumchukua dada yetu ili akacheze na mwanaye Bila hata ridhaa ya Baba yetu)), Huyu jamaa alikuwa anaishi karibu na Barabara Ambapo walikuwa wanapita watu wengi Wengi wao walikuwa wakielekea Nchi jirani Ambapo walipokuwa wanafika pale wamechoka hivo ilikuwa inawalazim kuomba Huduma kadhaa kama Chakula,Maji,
Jamaa ukiomba Maji ya Kunywa alikuwa Anakuletea Ndoo ya Lita20 usipoyamaliza jamaa alikuwa Anakukata Kichwa, watu wengi aliwauwa kwa njia hiyo na Kuwapora mali walizokuwa nazo,
Jamaa alikuwa Na mwili pia uso wa kutisha hivo ilikuwa Vigumu kumkabiri ukiwa peke yako hata mkiwa zaidi ya mmoja ilikuwa vigumu kumkabiri.
Jamaa alikuwa Ana uwezo wa kuteka Basi akiwa peke yake na kuwapora abiria wote Mali zao.
Kwa sasa nipo tight lakini nitarudi baadae!!!

Lakini nilichotaka kukuonesha hapo ni kwamba; hapo UMESIMULIA lakini kwenye script hautakiwi kusimulia bali unatakiwa KUONESHA/KUONYESHA!!

Kwa mfano, paragraph ya kwanza niliyo-highlight with RED naweza kuiandika hiv: (sio script)

Mlango wa mbele unafunguka! Mwanaume wa makamo anatokea toka ndani huku akionekana amefura kwa hasira. Anapepesa macho kushoto na kulia kisha anafunga mlango kwa KUUBAMIZA huku akiwa amekunja ndita kwenye usoni pake.

Anatembea hatua kadhaa kabla ya kukutana na kijana wa makamo ambae anapatwa na mshituko mara anapokutana na mwanaume huyu. Huku akionekana wazi kujawa na hofu, kijana huyu anajitahidi kuongea japo kwa kitetemezi kidogo:

"Ka...ka... kaka Ndole, shika..shika...!" Kabla hajamaliza kutoa salamu yake, ghafla Ndole anarusha ngumi mzito inayotua moja kwa moja kwenye taya la kushoto la kijana huyo!

Kijana anapepesuka lakini kabla hajakaa sawasawa, anasindikizwa na teke kali la tumboni linalompeleka moja kwa moja ardhini
!

Sasa tofauti yake hapo nini; wewe hapo juu ulikuwa unasimulia kiasi kwamba huwezi kuchukua shot kwa kuandika "...jamaa huyu alikuwa katili!" Kwa sababu hata wewe na simu yako ya kamera sidhani kama unaweza ku-shoot kwa sentensi inayosema "...alikuwa katili!"

Kwenye mfano niliondika mimi kwa kutumia hiyo stori yako; sijasimulia bali NIMEONESHA na ndicho kinachofanyika kwenye uandishi wa script!

"Mlango unafunguka...! Unaweza ku-shoot tukio la mlango kufunguka
"Mwanaume wa makamo anatoka ndani...!" Pia unaweza ku-shoot hilo tukio
"Huku akionekana amefura kwa hasira...!" Unaweza ku-shoot n.k!!

Na matukio yaliyofuata yanaonesha ni namna ile kusalimiwa tu kwake imekuwa nongwa!!!

Kwahiyo hiyo ndiyo tofauti ya kwanza kabisa.... story UNAWEZA kusimulia na wengi huwa wanasimulia lakini script STRICTLY unatakiwa kuonesha na sio kusimulia ili kuwezesha shooting!!

Na kwa vitu ambavyo havionekani kama sauti kuna namna ya kuvionesha... unatumia herufi kubwa! Kwa mfano, nimeandika "...kisha anafunga mlango kwa KUUBAMIZA..." Kuubamiza nimetumia herufi kubwa kuonesha kwamba hapa palitokea sauti!!!

NOTE: 1. Nilichoandika sio script bali story manake script ina format yake ambayo ni tofauti na stori kwa 100%.
2. Punctuation kwako ni bonge la kimeo!!! Huwezi kuwa professional writer bila kuzingatia punctuation.

See ya next time when I am free!!
 
Ahsante sana, apo nmekuelewa vzuri sana.
 
Mzuri kwa Maana gani labda?
Sura au Tabia?
Kimuonekano yaani uwe na appearance ya mauzo.

Kama ni KE uwe na hips na miguu na sura ya kiana
Kama ni ME basi uwe mpaka poda na unajua kitinda nyusi.

Sasa hayo mengine ya kipaji,tabia na lugha ni kama bonasi tu hayo nililokutajia hapo juu ndio ya msingi kwa industry ya Tanzania hii.

Unaweza kudhani haya maneno ni yangu na nimeyatoa kwa kejeri, lakini kiukweli haya sio maneno yangu bali ni maneno ya Riyama wa bongo movie. Nilichoyafanyia mimi ni paraphrasing tu.
 
eliakim xavery

Kama bado una mpango wakuwa mwandishi wa screenplay, fanya mchakato uingie google tafuta kozi za script writing. Baada ya kusoma na kumaliza then anza kuandaa script kwa kuiandika, unaanza na script fupi yenye scene hata 20 ambazo zitakuwa solid kwa kulingana na ujuzi unaoupata kila siku. Baada ya hapo endelea kuandika kila siku na kuangalia maeneo gani unakwama, ukishajua kitu kinachokusumbua unaweza kurudi tena google na kujifunza zaidi.

After all hakuna mtu atakayekubeba akidhani una kipaji cha kufanya jambo fulani. Hizo script zako ziandae na kuzitunza vizuri inaweza ikawa ni sehemu za Cloud au sehemu salama unayodhani itakuwa bora kuzitunza (Hapa I hope scripts zako ziko kwenye soft copies). Baada ya hapo tumia simu yako kurekodi hiyo script ukiwa na wadau wako, mnaweza fanya for fun then unakaa na hiyo filamu yako na kuangalia mahali pakubadili namna ya uandishi na vitu vingine vya msingi. Ukiona kamera ya simu yako ni nzuri na uigizaji wako na script zako ziko vizuri anza kuzitupia mtandaoni, unaweza kuchapisha hizo video Facebook, TikTok, Instagram na YouTube. Kwakuwa unaanza kuwa makini kusoma comments za wadau zitakazokusaidia, zile za kashfa achana nazo.

Baada ya muda utajua una uwezo gani wakuandika na nguvu yako hiko kwenye genre gani. Na ikiwa bado utakuwa unaendelea kuandika na kuchapisha video zako mtandaoni (hapa andika jina lako la kwamba wewe ni script wright) wadau wanaoijua sanaa watakutafuta na kukushauri na hata kutambua kipaji chako. Then booooooom one day na wewe Series yako itakuwa inaruka pale Azam (na channel zingine za Entertainment za Bongo).

Utatoboa tu, ila si kirahisi
 
Vizuri

Back
Top Bottom