Nataka kuhamia kwenye "Kibanda" changu

zabron k

JF-Expert Member
Nov 11, 2015
923
1,058
Wakuu
Baada ya kusota sana na mshahara wa mwezi na mikopo ya masimango plus kero za wenye Nyumba, nimefanikiwa kusimamisha kibanda hadi kwenye RINTA.
Nimewaza na kuwazua nikafikiria kuhamia hivyo hivyo kwa kufunika mabat juu ya paa, milangoni na dirishani ili maisha yasonge.
Hapa nilipo kodi 100,000×6.
Mtanzania mwenzako naomba ushauri kwa suala hili, je nifanye maamuzi magumu au niendelee kuumia hapa hapa?
NB: Sina mtoto bali nina mke
 
Hamia tu then hzo 100,000 x 6 zifanye kuwa za finishing taratibu kuliko kumpa landlord.
 
paua hata vyumba viwili mkuu kama una familia kakae, unaweza kuanza na milango na madirisha used kama hela haijakaa sawa baadaye unayachomoa, kwanza kibanda kipo wapi
Nyumba ipo Mkoa wa Pwani sehemu inaitwa Vikindu ni baada ya kiwanda cha Azam Soda & Juisi
 
kakae mkuu, mimi nilikaa kwenye kibanda hapo kimara kingongo wakati huo bado hapajanganya, niligonga bati mlangoni na dirishani nikaacha nafasi kidogo ya kuingiza hewa, kwako ni kwako
 
Usalama mahali hapo upo vipi? Kuna majirani karibu? Je unawatu wa kubaki nyumbani ukitoka? Kama jibu ni ndio hapana shaka hamia la kama hakuna jipange vizuri.
 
Serikali ilifanya makosa makubwa kwenye kusimamia nyumba na makazi...ndio kisa cha watu kusumbuka hivi...serikali ilipaswa kujenga nyumba wananchi tupange humo kwa gharama nafuu kama ilivyo ulaya na marekani,finland nk sasa matokeo kila mtu anataka kua na nyumba yake jambo linalosababisha mlundikano wa vijumba vingi visivyofikia standard ya nyumba hasa wenyewe tunsita "banda"haiwezekani mtu uishi kwenye banda,hizi nyumba imekua tatizo dar hebu kama unakaribia kutua dar kwa ndege tazama chini uone msongamano wa vibanda hivi mbagala,kitunda majohe
 
Hamia tu kwako ezeka hatari nyasi!nyumba za kupanga problemoo tu
 
Serikali ilifanya makosa makubwa kwenye kusimamia nyumba na makazi...ndio kisa cha watu kusumbuka hivi...serikali ilipaswa kujenga nyumba wananchi tupange humo kwa gharama nafuu kama ilivyo ulaya na marekani,finland nk sasa matokeo kila mtu anataka kua na nyumba yake jambo linalosababisha mlundikano wa vijumba vingi visivyofikia standard ya nyumba hasa wenyewe tunsita "banda"haiwezekani mtu uishi kwenye banda,hizi nyumba imekua tatizo dar hebu kama unakaribia kutua dar kwa ndege tazama chini uone msongamano wa vibanda hivi mbagala,kitunda majohe
...hebu soma tena hiki ulichoandika halafu ujiulize kama uliishirikisha akili yako sawasawa!
...sawasawa!!??(kwa sauti ya Maalim Seif)
 
Wakuu
Baada ya kusota sana na mshahara wa mwezi na mikopo ya masimango plus kero za wenye Nyumba, nimefanikiwa kusimamisha kibanda hadi kwenye RINTA.
Nimewaza na kuwazua nikafikiria kuhamia hivyo hivyo kwa kufunika mabat juu ya paa, milangoni na dirishani ili maisha yasonge.
Hapa nilipo kodi 100,000×6.
Mtanzania mwenzako naomba ushauri kwa suala hili, je nifanye maamuzi magumu au niendelee kuumia hapa hapa?
NB: Sina mtoto bali nina mke
Sawa
 
Back
Top Bottom