Prince Nadheem
JF-Expert Member
- Feb 25, 2012
- 1,270
- 1,111
sasa mkuu wanishauri nichukue simu gani ya yenye OS ya Android ambayo ipo kwenye around laki 2.5??mkuu umetokea wap? una simu nyengine au hio galaxy chat ndo itakua main phone?
simu ni nzuri hata button zake hasimbui sana though sio classic kama za blackberry ila ni nzuri. utaweza update jelly bean na kuenjoy os mpya.
tatizo la hii simu ni processor yake 850mhz inaifanya iwe slow sana hasa pale unapokua na matumizi ya haraka haraka labda ulikua internet then hapo hapo ukataka umpigie mtu simu fasta fasta.
kuhusu kuenjoy apps kiasi flani utaenjoy app zote zinafanya kazi japo slow slow ila hvo hvo. kwa games sahau hutapata high end game hata moja nimejaribu asphalt zote zimekataa, temple run ipo slow vibaya sana.
kama una simu nyengine unatumia then unataka kuijua android tu nunua hio galaxy chat ila kama unataka hii ndo iwe simu ya kila kitu then sikushauri kuinunua
sasa mkuu wanishauri nichukue simu gani ya yenye OS ya Android ambayo ipo kwenye around laki 2.5??
Badala ya kujadili mambo ya maendeleo mnajadili simu!!!
Bure kabisa...
kwani umeambiwa hii ni jukwaa siasa ?
wewe ni mjinga (soma kamusi ya kiswahili maana ya neno hilo)Badala ya kujadili mambo ya maendeleo mnajadili simu!!!
Bure kabisa...
Nikiona kijana kutwa nzima anajadili simu, viatu na pamba huwa nasikitika sana!
wewe ni mjinga (soma kamusi ya kiswahili maana ya neno hilo)
simu kwa sisi wanateknolojia ni zaidi ya kupiga na kutuma sms, simu ni sehemu ya maisha,
hapa hatujadili simu kuwa ipi nzuri au vipi, tunajadili in terms of functionality, tunajadili simu tofauti tofauti zinawezaje kuwasaidia watu wa makundi tofauti.
mwisho usiwe na mawazo mgando, elimu haina mwisho, afu usije kwenye jukwaa kudisrespect wanajukwaa kwa kuwaita Bure
we hujui kwa nini kuna Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia
Badala ya kujadili mambo ya maendeleo mnajadili simu!!!
Bure kabisa...
yani nimecheka sana kauli yako kaka nikakumbuka mtu aliyetoa tenda atengenezewe hii website atakua kama wewe
Karibu Kwenye Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita
anyway mkuu ili nchi iendelee inabidi watu wawe na uwezo tofauti tofauti usifkiri kama nchi nzima wote tukiwa madokta na wanasheria basi ndio tutafanikiwa.
siku hizi toka tuingie karne ya 21 dunia imebadilika badala ya kutegemea viwanda sasa hv tunategemea mawasiliano. mawasiliano ndo kila kitu na sababu mawasiliano ndio kitu muhimu duniani utaonaje watu wanaozungumzia simu wapuuzi?
kwa kutumia nfc(near field technology) mcdonald (wana migahawa kila pembe ya dunia) wameweza kuwafanya watu kununua vitu kwenye migahawa bila waiter. unafika kwenye mgahawa automatic menu inatokea kwenye simu unachagua msosi unaletewa. hebu ona simu na mawasiliano vinavyoendelea na kurahisisha maisha.
ni simu zinazotuonesha saa, zinazotuamsha alarm, zinazotunza kumbukumbu zetu na kutusaidia kwenye kusoma. bado una ignore tu uzungumziwaji wake?
Kwa hyo wewe unaona kukaa alipoolewa dada yako ndio maendeleo? We bogus sana yani
Mkuu,
Kuna mtindo mpya wa jeans madukani, ushanunua?
Halafu kuna viatu vikali, toleo jipya, ushanunua?
Na simu za android samsung galaxy, kali sana, ushanunua?
Hahahahahahahahahahahaa. Watu wanawaza simu, mavazi na ngoma halafu wanafikiri maendeleo yatawafuata kibarazani!!!
unazungumzia maendeleo? Je maendeleo unayosema wewe ni yapi?
Si ndio kama hayo ya kununua simu mpya na viatu mtindo mpya.
That is very interesting! Yaani mtu kuagiza msosi kwa kutumia simu wewe unaona maendeleo!!!
Hivi hujui kuwa kwa kufanya hivyo binadamu anaanza kupoteza interpersonal skills kidogokidogo? Ndio maana vijana siku hizi hata wakienda kwenye interview wanaweza kuulizwa swali la kawaida tu kama "where do you live?" wanajikuta wanatetemeka. Wapeshapoteza uwezo wa kuwasiliana na binadamu wenzao kwa sababu wamezoea kubonyeza simu na kupata huduma.
Hizi simu mnazokesha mkizijadili zimebuniwa kuwafanya muwe consumers wa products za watu. Mkijenga tabia kila toleo la simu mntaaka kuwa nalo mnakuwa hamna tofauti na wale wanaotaka kila mtindo wa kitenge ukitoka mpaka anunue.
Utumwa unakuja kwa mitindo mbalimbali. Unaweza kuwa mtumwa bila kujijua.
we ni nani by proffesion then ntakwambia unamiss nini, manake hapa naona unafanya upondaji tu
we ni nani by proffesion then ntakwambia unamiss nini, manake hapa naona unafanya upondaji tu
Hana ajualo huyo bogus. Utapoteza muda wako bure kujibizana naye.. . Niko na swali. Je inawezekana kuchange os ya windows kwenye htc phone ikawa jelybean?