Kabla hujaondoka hapa, tafadhali wasiliana kwanza na Le Mutuz System.
Yeye ana uzoefu wa miaka 30 huko majuu na hataki kabisa kusikia habari za huko.
Lakini ushauri wangu, naomba ukomae hapa hapa nyumbani kwa sababu pana fursa kibao tu kama utajituma.
Tatizo la vijana hususan wanaomaliza chuo huwa wanakuwa na ndoto fulani za abunuwasi wanapokuwa huko, sasa wakishafika kitaa na kuona upepo tofauti, akili huwa zinawahama na kutamani kwenda majuu kwa sababu huwa wanahisi kwa hadhi ya elimu waliyonayo pamoja vyeti vyao, hawawezi kufanya kazi za huku kitaa ambazo ndio zinawatoa wengine.