Nataka kufunga mita yangu ya luku dukani nijitenge na wengine, naombeni ufafanuzi na gharama

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
3,871
8,381
Wakuu heshima kwenu.

Naombeni ufafanuzi na maelekezo ya kufata Ili kufunga MITA ya luku inayojitegemea.
Je hatua gani za kufata?

Vitu gani vinahitajika?

Gharama ya mchakato mzima ikoje??

Asanteni sana.

TANESCO
 
Wakuu heshima kwenu.

Naombeni ufafanuzi na maelekezo ya kufata Ili kufunga MITA ya luku inayojitegemea.
Je hatua gani za kufata?

Vitu gani vinahitajika?

Gharama ya mchakato mzima ikoje??

Asanteni sana.

TANESCO
Mpendwa Mteja !

Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022

Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni shilingi 320,960/=,

Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,

Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=

Aidha, gharama za kuunganisha umeme ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,

Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,

umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.

Zingatia

Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= kama ilivyoelekezwa na EWURA.

NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
 
Wakuu heshima kwenu.

Naombeni ufafanuzi na maelekezo ya kufata Ili kufunga MITA ya luku inayojitegemea.
Je hatua gani za kufata?

Vitu gani vinahitajika?

Gharama ya mchakato mzima ikoje??

Asanteni sana.

TANESCO
Ndugu mteja taratibu ni

Omba umeme kupitia

Nikonekt.tanesco.co.tz

Au

Nikonekt App

Au

Bofya *152*00#

Kisha tutakupimia na kukuona kama unakidhi vigezo na kukupatia gharama za kulipia

Ahsante
 
*MAOMBI YA MITA (T 1) KWA SASA NI TSH 320600.

*KUNA KUCHORA RAMANI NA KUGONGA MUHULI WA MKANDARASI- bajeti yake weka TSH 20000

*Mita yoyote ile ya tanesco lazima ifikie kwenye Circuit breaker alafu iende kwenye main switch kisha ndo uje kwenye matumizi.kwa iyo ukiomba mita mpya ni lazima ufunge sircuit breaker na main switch nyingine.

*Pia kuna ulinzi wa mfumo(earth protection) lazima eath road ifungwe kwa ajili ya ulinzi au usalama

Kwa iyo hapo bajeti yote pamoja na ufundi inaweza fika TSH 600,000/=
 
Back
Top Bottom