Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Usinunue kwa mtu bali ongea na wale wanaotembeza na magari utajua kiwango wanachoanza kuuza.

Au jaribu tafuta jirani anayechukua mzigo mkubwa kama itawezekana akuunganishie oda japo.

Chunguza vzri kuhusu bei huwa kuna upigaji
 
Wakuu nataka kufanya biashara ya vinywaji na kuuza jumla nina mtaji mdogo siwezi kuwa distributor kwa kufuata bidhaa kiwandani hivyo natafuta muuzaji wa kuniuzia jumla na mimi niweze kuuza jumla kwa mkoa wa Dar es salaam

Au kama kuna mtu anafahamu sehemu au namna ya kununua kwa jumla kreti ishirini za vinywaji vya Cocacola na ishirini za vinywaji vya Pepsi.

Duka litakua na vinywaji vingine kama maji na nk
Sasa mkuu hiyo biashara utaiweza kweli?, kwani creti moja ya soda faida yake ni kama tsh.500, nadhani kwenye gari unauziwa 9500, na wewe unatakiwa kuiuza 10, 000!!kuifanya biashara hii ni rahisi sana hasa ukiwa Dar, wewe watafute wale wenye magari ya pepsi/coca watakupa utaratibu wa kuwa wana kushushia kwani huwa wanasambaza mitaani.yaani carton moja ya maji faida ni kati ya 300-400!!
 
Habari zenu Wana JF.

Nahitaji kufanya biashara ya vinywaji vikali jumla na Rejareja kwa mkoa wa Shinyanga(Shinyanga mjini).

Kwa anayefahamu ni namna gani naweza kuwa wakala wa K-Vant, Konyagi, Double Kick, Shung'aa, Azam Juice na Kiwingu naomba anijuze tafadhali.
 
Hasara na faida utazikuta ukianza biashara.

Biashara ni nzuri inamzunguko ila inategemea na wateja wako ni kina nani. Biashara hii kubali mali kauli kutoa bia na kusubiri wauze wakurejee pesa yako. Kama ni stockists wateja wengi itakua ma bar Na grocery so itabidi upush zaidi ili upate order. Delivery ni msingi wa hii biashara.

Biashara hii mfano bia local nyingi price haipandi wala kushuka maana imekua regulated sana kutoka kwa wazalishaji. Atleast vinywaji wa nje unaweza price kulingana na wewe unavyotaka
 
Katika mihangaiko nimeamua kufanya biashara ya vinywaji yaani Wines na ndugu zake ila chagamoto yangu ni sijui wapi nitapata mzigo kwa bei ya chini yaani chimbo zuri kwa biashara hii.

Msaada kwa anaejua machimbo kwa DSM.
Wazoefu karbun.....
 
Katika mihangaiko nimeamua kufanya biashara ya vinywaji yaani Wines na ndugu zake ila chagamoto yangu ni sijui wapi nitapata mzigo kwa bei ya chini yaani chimbo zuri kwa biashara hii.

Msaada kwa anaejua machimbo kwa DSM.
Kuna sehem moja Mbili tatu zitakusaidia.
Ya kwanza ni pale manzese tip top kwenye maduka ya liquor store Especially pale depot ya mrina wako na bei reasonable sana,
Ya pili Ni kitumbini ukiulizia tu kule kuna maduka ya wahind pale ni maarufu sana kwa kuuza Wine,Shampen
mwisho ni k.koo mtaa wa mkunguni.

Hii biashara Nimefanya sana nilipomaliza chuo na imeniweka sana mtaani na kunipa uzoefu wa kutosha.Best of lucky Jamaa
 
Back
Top Bottom