Nataka kuezeka nyumba hii - Mrejesho

Nataka kuezeka nyumba hii - Mrejesho

Hongera Sana Mkuu Njaa umepiga hatua kubwa sana!! Nipo kwenye sehemu mbaya nikipata mda nitachangia maswali yako.
 
Last edited by a moderator:
Mimi naomba nikupongeze kwanza kwa hatua uliyofikia mkuu.
 
Hongera sana sana mkuu,hapo umefika ni pazuri sana.

Kwanza Pole sana kwa kuumizwa na ndugu yako uliempa majukum.
Hii Kitu inaitwa pesa haina ndugu,haina baba wala mama,
Nakupa mfano mdogo,mie ninamtoto wa mama yangu Mdogo yupo South Africa miaka mingi,na sio mtu wa kuja tanzania mara kwa Mara,inaweza kufika hata miaka mitano akaja mara moja.
Alipokuja akasema mama yake amtafutie Kiwanja,basi mama yake upesi ndani ya wiki tu akakipata,sasa wakati yeye anafanya mchakato wa kutuma pesa kumbe mama yake ana mipango mingine kabisaa,basi huweiz amini alitumiwa pesa na mwanae wa kumzaa,akazila zoote.Yaani utafikiria sio mwanae,wakati ile nyumba na yeye kama mama mzazi ni faida kubwa sana kwake,na pia Mwanae alimuamini sana kama mama.
Siku moja namsikia anamuambia mama kwamba kama akija atajifanya kwamba kiwanja kilikuwa na mgogoro na kesi ipo mahakamani,na kapanga kutunga kesi ya owongo.Iliniuma sana hadi leo,maana 10m sio pesa ndogo kwa maisha ya South Africa.
Sasa hilo ni somo kwamba mambo ya pesa sio kumuamini mtu moja kwa moja hata awe nani.

Kwa maelezo hapo juu,ni kwamba hata mie mifuniko hiyo sijaipenda kabisaaaa,yaani kama umeweza kupiga picha kw aumbali huu na mpaka mie naona kabisa mifuniko ileee,sipati picha aliepo karibu,na pia nawasiwasi hata hiyo mifuniko imepindapinda sana,na itakuwa ilinyooshwa kwa nyundo,wakati huwa kuna mashine maalum ya kuitengeneza.
Kuna nyumba inapigwa mifuniko wala huoni kiti utafikiria haipo.

Ile mifuniko unaweza kuitoa,maana misumari yake ipo juu juu,ila pata fundi mzuri,na pia yakunua sio kwamba sio mizuri ni mizuri ila uwe na fundi anaejua bati,maana mingine utakuta haina uwiano wa material ya bati lako,sasa mwisho wa siku rust inaanzia hapo hapo.
Hii nashauri ni bora ununue bati zako upeleke kwenye zile mashine zao za kutengeneza mifuniko kisha uitumie maana utakuwa na uhakika wa hilo.
Hii ni sawa na kujenga nyumba,ukinunua tofali za mwanzo basi hadi nyumba inaisha hakikisha unamaliza za ubora wa aina hiyo hiyo la sivyo nyumba inakatika.

Hahaha Hembu Mtaje huyo Mana JF Jirani yako? Atakuwa Kingkong huyo,maana jamaa Dar nzima yake.
Hembu namie nipe bei ya kiwanja huko niongezeke tujenge JF Member Street
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom