Nataka kuanzisha umoja wa wapangaji Dar es Salaam

Nataka kuanzisha umoja wa wapangaji Dar es Salaam

fugees

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
2,868
Reaction score
884
wadau habari ya mwaka mpya. Nombeni mawazo yenu hapa.

Ninataka kuanzisha chama cha umoja wa wapangaji Dar es Salaam(sina uhakika kama kipo kama kipo basi ni mfu na hakina malengo mathubuti). kwanini nimeamua kufanya hivi? kwa sababu zifuatazo:-
  1. manyanyaso wanayopata wapangaji toka kwa wamiliki wa nyumba.
  2. sheria za ardhi bado hazijamlinda mpangaji vya kutosha, mfano kulazimishwa kodi ya miezi sita mpaka 12
  3. utapeli wa madalali na manyanyaso yao dhidi ya wapangaji, mfano hela ya mguu unatoa harafu anakupeleka kwenye mabanda ya kuku na njiwa kuwa hizo ndio nyumba au vyumba. pia uhalali wa kodi ya mwezi mmoja kwa kuwa ni ya dalali na si kama sheria inavyosema.
  4. wenyenyumba wengi naweza aema asilimia 70 hawalipi kodi hivyo kuikosesha serikali mapato.
  5. wapangaji kutopata nyumba kwa wakati.
kutokana na sababu zangu hizo hapo juu, basi natamani sana kuwa na chama cha wapangaji mathubuti ambachokitakuwa na malengo yafuatayo:-
  1. Chama kitamtafutia nyumba mteja kwa gharama nafuu mfano ada ya 3% ya thamani ya kodi ya mwaka mzima ( au wadau watakavyopendekeza) ilimradi tu ipingane vikali na ile ya kodi ya mwezi mmoja ya dalali.
  2. Kutetea haki za wanachama (wapangaji) ikiwamo kufungu mashauri mahakamani dhidi ya vitendo dharimu vya wapangaji.
  3. kuboresha au kuhamasisha na kutoa maoni kwa selikali kuweka viwango halisi vya kodi kutokana na ubora wa nyumba ili kutoa kodi kwa serikali.
  4. kuondoa vishoka katika biashara ya udalali, dalali yeyote ni lazima awe amesajiliwa na chama cha madalali na ana EFD machine na si janja janja ya kodi ya mwezi mmoja kuwa ya dalali.
  5. chama kitashilikiana na serikali kuu na za mtaa kuandaa mfumo maalimu wa nyenye nyumba kupeleka taarifa za uwepo wa nyumba au chumba selikali za mtaa nyumba ilipo na kubandika gharama halisi na aina ya nyumba. pia selikali itapata ,mapato kwa kua kuna ghalama mpangaji atachangia mfano 0.5% ya thamani ya kodi ya mwaka pale anapopata nyumba.
  6. wamiliki wa nyumba wanaotoa taarifa ni lazima wawe wanakubali kulipa kodi (witholding tax) ambapo mpangaji atakuwa na peleka TRA
  7. iwe halamu kupangisha nyumba bila serikali ya mtaa husika ambako nyumba ilipo kujua.
  8. mwanacha atajiunga na chama cha wapangaji kwa kutoa kiasi kidogo cha uanachama na akiwa amesha jenga nyumba yake na kuhamia atatoa taarifa ya kujitoa.
  9. wanachama pia watakua wanatoa taarifa kwa chama wanapohama ili kuwapa wanachama fulsa ya kujua kunamahali kuna nyumba ila itakua lazima kupitia serikali ya mtaa husika ambapo nyumba ilipo.
Wadau naomba mawazo yenu hapa. Mimi furaha yangu ni kuona lengo linafanikiwa hii 2020 haijarishi kama mtu atafanya au achukuwe wazo hili, lengo ni kuona hili linatimia. NATANGULIZA SHUKRANI ZA DHATI KWA WACHANGIAJI.
 
Hakuna anayekuwa mpangaji,akajisahau,wengi wa wapangaji,karibia 98%,lengo ni kumiliki mjengo wake,na wengine ni wapangaji,lakini tayari na yeye anamiliki nyumba au majumba,ila amepanga karibu na kazini kwake,au kutokana na familia yake ndogo,anatafuta nyumba ya familia ndogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo zuri ila naona kama unatengeza mianya ya pesa mana toka mwanza unaizungumzia, mara serikali za mtaa, withholding tax, efd , ada ya uanachama, commission. Kama hutaka kuusisha hela hebu acha mfumo uliopo mana unapoelekea n kumbana na kumpa mzigo mpangajia na sio mwenye nyumba kama unavyofikilia
 
Back
Top Bottom