Nataka kuanzisha Msikiti binafsi

Nataka kuanzisha Msikiti binafsi

Atapataje jini la kuliweka msikitini? Maana kila Msikiti unalo jini

mnaridhika sana nyoyo zenu mnapoukashifu uislam ..sasa ww nani aliekudanganya kuwa misikitini kuna majini...uislamu unapiga vita uchawi wa aina yoyote ile na hata afanye sheikh huo uchawi hukmu yake ni mshirikina tu...karibu ktk uislam ujionee mwenyewe na uutambue uislam nakuhakikishia ukiujua uislam utasikitika sana kwa kuchelewa kuujua uislam
 
Mkuu Ngongo, navyojua Mimi mtu kutoa uwanja kwa ajili ya kujenga msikiti haimaanishi kuwa huo msikiti ni wa binafsi.

Kwa mfano mtu mwenyewe kanisa binafsi ibada yake inaendeshwa tofauti na makanisa mengine. Lakini c kwa misikiti. Ibada yake ni ile ile.

Ibada ya kiislam isipofuata utaratibu uliowekwa na Quran na suna haitakua ibada sahihi. Na ukitaka kuviepuka hivyo viwili huo ni ukafiri.
Bora ubaki hukohuko ambako mtu anaweza kuanzisha utaratibu wa ibada atakavyo bila ya muongozo sahihi.
Mf. Kuwalisha watu nyasi na mengineyo mna yoyafanya!
 
Mbona hilo lina wezekana tu mkuu,
tena misikiti mingi ni ya hivyo
Ila sipati picha kama kungekuwa na kanisa la familia ya flani tu.
 
kanisa ni mali ya Mungu ..Mungu humchagua mtu ampendaye ambaye ni mwaminifu kwake na kumpa jukumu la kulichunga/ kuliongoza kanisa ili watu wapate uponyaji wa roho na mwili (ndio maana hata waislamu utawakuta kanisani jambo ambalo ni vigumu kwa wakristo kuwakuta msikitini.)

Kwa hiyo ndo ujimilikishe Kanisa eenh????.
 
Nadhani nitakuwa nimemuelewa vizuri Mtoa mada
Yeye anachohitaji ni kuwa na kituo Ambacho atakuwa huru kuongea lolote lile lulilo kichwani Mwake
Bila ya kujali kama limefuata Misingi ya Dini (vitabu)

Kama Ambavyo leo twaona Baadhi ya Wachungaji tena wengine wakijiita Manabii wakiongea Upuuzi mbele ya Makanisa yao (Binafs) na waumini wakisikiliza na Kushangilia kwa kupewa habari za Ndoto anazoota mtumishi
Pasina kudadisi kwamba huyo Mtumishi alikuwa Ametumia nini kabla ya Kulala
Huenda alikuwa Bhange au Viroba na ndo maana akaota ndoto za Alinacha

Katika uislam Utapata tabu sana na huenda Ukaambulia Bakora kwani Waislam sio watu wa kuburutwaa tuu bila ya Dalili
Kila kitu Utachoongea Lazuima uwe na ushahidi nacho ktk VitabuVinginevyo Huo Msikiti Utasali wewe na Wanao

HUO NDO UISLAM HAUENDI ILA KWA DALILI KUTOKA VITABUNI NA SI MAWAZO BINAFS
 
Mwenyezi Mungu amesema: "Na kwa hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu".

Qur'an, 72:18

"Msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu "


Sasa mnamuabudu nan?
 
Kama ilivyo kwa makanisa binafsi. Kina kakobe, Mwingira, Gwajima na Lusekelo. Haya makanisa ni Mali yao binafsi.

Ni utaratibu gani naweza kufuata nikaanzisha Msikiti binafsi?

Mnapoteza muda kujibu mada yenye kebehi muanzisha mada si muislam ni mfuasi tu wa UKAWA anajua fika HAKUNA taratibu za kufanya msikiti kuwa ni wamtu binafsi lengo kubwa ni kuudhalilisha uislam basi.... i can't believe almost two pages comment for this nonesense.
 
Nikweli mkuu quran ishaeleza,msikiti ni wa m/mungu kinyume chake ni kupinga quran na unakuwa ukafir huo.
 
hata makanisa yote ni mali ya wakristo ila utofauti unakuja kwenye misimamo.

je, dini ya kiislam haina madhehebu? kama inayo basi hata mtu binafsi anaweza kuanzisha la kwake kwa misingi anayoiona yeye itamfaa.

Madhehebu yapo kwa mfano kuna.

Suni
Shia
Ismailia
Bohora
Konki
Ahamadiya
 
Mnapoteza muda kujibu mada yenye kebehi muanzisha mada si muislam ni mfuasi tu wa UKAWA anajua fika HAKUNA taratibu za kufanya msikiti kuwa ni wamtu binafsi lengo kubwa ni kuudhalilisha uislam basi.... i can't believe almost two pages comment for this nonesense.

Mimi nilitaka kujua utaratibu wa kumiliki msikiti. Kama mnasema misikiti yote ni ya Allah, basi hamna haja ya kulumbana. Hata hivyo nimewaelewa na ninawataka radhi pale nilipomkwaza mtu.
 
Back
Top Bottom