Hapana mkuu. Siyo makanisa yote ni Mali ya wakristu.
Kuna makanisa yanawamiliki wakristu na siyo wakristu wanamiliki makanisa. Makanisa haya yanayojiita ya kiroho yanamilikiwa na watu binafsi kabisa.
Na ile michango yote inayotolewa, sadaka,zaka na hata fungu la 10 hawa wamiliki wanachukua mzigo wooote. Tofauti kabisa na RC, na KKKT.
Hawa michango tunayotoa inaturudia tena katika huduma za kijamii kama mashule, na hospitali.
Usipotoshe mkuu!
Makanisa mainstream yanachukua mpunga vizuri sana, tena kuwazidi akina Ngwajima. Wao wana miradi vitega uchumi, ambavyo vilianzishwa kwa sadaka za waumini lakini faida yake wanaroll nayo yote, check!
Shule na Hospitali, you still buying that ----? Waliingia mkataba na Serikali, wanapokea fedha za ruzuku kutoka Serikalini,
FaizaFoxy atakuja kunieleza ni kiasi gani, na kwenye afya wameingia mikataba ya uendeshaji, Serikali inaweka watumishi na kuwalipa, na bado unachangia tozo la huduma, check!
Shule zinaendeshwa kama NGO, ada nafuu (uongo), na fedha za wahisani, wanaosapotiwa na Serikali za nje zinazotuibia, check!
Sadaka haikatwi kodi wala kufanyiwa auditing, ukitokea wizi ni kimya kimya, mfano Ujenzi wa Ukumbi wa Rugambwa, Ostabei ambao ulianza kutafutiwa fedha kwa mchango wa pili tangu Nyerere anasali pale, check!
Wana mchango wa pili kwa kila PR ya Kijamii wanayofanya, kutembelea wagonjwa, kuona yatima na kadhalika, wanaona uchungu sana kutoa sehemu ya mafungu yao kwa kazi hiyo, check!
Ni wezi, wanasisitiza maandiko yanayohamasisha sadaka, na nyimbo zake pia! Lile andiko la 'Ukikosana na nduguyo usilete sadaka yako...' huwa linakwepwa kama si kutotajwa kabisa, check!
Kimsingi yana historia ya wizi, biashara ya utumwa, kuunga mkono uvamizi na kusapotiana na wakoloni, rejea; wamisionari, check!
Hawa wanawaibia kwa mujibu wa sheria, na kwa akili ya hali ya juu, maamuma kondoo huwezi kuona, check!
Angalia uhusika wao wa moja kwa moja kwenye mambo yanayokuza ustawi, ujasiriamali, kukopesha, kusaidia mayatima, wajane, wagonjwa n.k, utagundua ni hasi au sifuri, check!
Ni matajiri kuliko makampuni mengi, wewe hujui hilo, check!