Nataka kuanzisha kampuni ya uchapishaji..!

Nataka kuanzisha kampuni ya uchapishaji..!

IHOLOMELA

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
1,807
Reaction score
1,677
Wana wa jamvi naomba ushauri wenu kuhusu hili. Toka nikiwa mdogo ndoto zangu ni kumiliki kampuni ya uchapishaji, hasa katika kuchapa maandishi na picha kwenye fulana. Nilianza zamani sana nikiwa shule ya msingi kuchonga maandishi katika makaratasi ya x-ray na kuweka nembo ktk fulana na mashati yangu. Kutokana na kupenda shughuli hiyo, sasa napamba fulana zangu kwa kutumia Transer papers. Ila nimeona niingie rasmi katika soko hilo kwa aidha kununua fulana na kuziweka picha na maandishi na kuziuza au kuwachapishia watakaoleta fulana zao. Tatizo sijui wapi pa kupata mitambo na gharama zake na kama ntaweza kumudu gharama za uendeshaji. Mtaji nilionao mpaka sasa ni tsh. Milioni tatu. Mwenye idea na fani hii naomba maelekezo.!
 
Tuendelee kuwasiliana, nipo sehemu naweza kutafuta muda nikakuchekia hiyo mitambo, Ila kwa sasa niko busy mno!
 
Back
Top Bottom