Nataka kuagiza gari hii, itanigharimu vipi?

Homeboi unajua bei ya bajaj now?.........for your information.....is not less than 4mil!

Dah Bajaj ya miguu 3 sasa ni kama 4.5mil na pikipiki Bajaj ni kuanzia 1.6mil CT100 na 125xcd ni kama 2.1mil hapa bado hujasajili.
 
Fisadi J,

Kwa haraka haraka hii kitu inaweza kukucost kitu kama US$2200 (CIF)...Kutoka hapo, TRA watakula kama US$ 1595 so jumla itakuwa US$ 3,750*1350 =TSHS 5,123,250

Hapo itakuwa bado gharama za agent, registration na TRA, Road licence, insurance na gharama za bandarini which can cost you up to Tshs 500,000! So total kitu mpaka kipo barabarani will cost you estimated cost of Tshs 5,623,250!

BWT: Nimemwona Dullymo kajaa tele hapa ni mzoefu zaidi kny hizi issues so anaweza kukupa ushauri zaidi pia unaweza check na captain Kitomai!

Kweli NL ni mzee wa details... uliniahca hoi ya Tanga l
 
Kweli NL ni mzee wa details... uliniahca hoi ya Tanga l

Aaahaaaaa...mzee wa ''DOCEBIT VOS OMNIA'' ...Huja toa updates...ile tour yako kule kunani iliendaji mzee....vipi ulienjoy or ulipata disappointments?
 
Nshukurusa sana kwa wazee wa kukokotoa, mnatoa mwanga sana. Inabidi TRA wawalipe, maana lazima wana-budget ya kutoa elimu ila sijui inaendaga wapi.

Matumaini yangu yakujikomboa na hii adha yanarudi, ila naomba wakuu mnikosoe. Na pengine hii inaweza kuwasaidia wengine kama mimi.

Nimeona kuna hivi vigari vidogovidogo (Nissan March, Toyota Duet, etc) vya mwaka 2001, vya cc 1,000, nimeona vinauzwa FOB $600 mpaka $800. Hivi vinapunguza kodi sana kwa kuondoa dumping fee na excise duty. Tukichukulia CIF ni $2000, pengine mtu anaweza kutoka maana nikikokotoa fasta napata 3,345,300/= bila kumhonga mtu.

Je, maana yake nikipata pa kukopa hiyo 500,000 nikaongezea kwa vi M3 vyangu naweza nikapata moja ya hivi vidude?

Kwa mfano:
http://www.tradecarview.com/used_car/japan car/nissan/march/820691/
http://www.tradecarview.com/used_car/japan car/toyota/duet/900408/

Sijali kina nini, mi ilimradi kitembee tu na kiweze ku-overtake daladala basi ... tehe tehe.

Naomba mawazo wakuu.
 
Fisadi.jones itabidi ubadili moniker uwe "Kafulia.Jones"
Hivi Fisadi gani hata kamkokoteni cha 5 million kinasumbua? ha ha haa

Mkuu nimecheka mpaka basi lol , majirani zangu ndio wananitania hivyo hivyo.

Waliponipa jina haya mambo ya ufisadi yalikuwa hayajaanza mkuu. Mimi hata kuzipata za kuweka mfukoni sijazipata, ntafulia vipi?

Bado nalipenda jina langu lakini lol
 
...mimi naomba kuuliza;

Watanzania-wakazi wa Uingereza bado wanahitajika kupata certificate za MOT toka kampuni ya WTM Utility Services 32 Norfolk Road DAGENHAM RM10 8EX...??? :)
 
...mimi naomba kuuliza;

Watanzania-wakazi wa Uingereza bado wanahitajika kupata certificate za MOT toka kampuni ya WTM Utility Services 32 Norfolk Road DAGENHAM RM10 8EX...??? :)

Jibu "no" alau kwa sasa given unayo valid DVLA M.O.T certificate.
 
Mkuu achana na gari nunua pikipiki tu. Gari utanunua baadae.

Ninapenda sana wazo la pikipiki, lakini pikipiki naiogopa sana, balance siko mzuri. Baskeli yenyewe napata shida kuendesha, na ilishawahi kuniadhiri vibaya mkuu.

Kwa hiyo ninaikimbia pikipiki sababu ya hofu tu mkuu.
 
Mbona watu hawanipi jibu kuhusu hivyo vidude vidogo dogo?

Au ndio wameshaenda kuniwahi na kuviagiza wao? lol
 
Mkuu Fisadi mimi ninakushauri hivi kweli unaweza ukapata gari from Japan kwa hela uliyonayo il vitu vya kufikiri:
Uimara wa gari, jee inamiliki mikiki ya barabara za Bongo? waweza nunua gari isidumu hata miezi 6.
Kwa ushauri wangu bora zidundulize alau zifike millioni 5 waweza kupata usafiri wa maana tena hapohapo Bongo.
Ama kama una mtu UK muagizie Suzuki Vitara, hazina bei, ni imara na ukibahatika kwa millioni 5 waweza kusukuma huu mkweche Dar. Naongea kwa uhakika kwa vile kuna jamaa yangu ameshawahi kuleta hio gari na ilimgharimu millioni 5.
mfano hii hapa:

http://cgi.ebay.co.uk/1997-SUZUKI-V...s_UK?hash=item439a4c6a23&_trksid=p3286.c0.m14

Kwa pesa ya madafu utaipata kwa mill 1.8 maximum. ila waingereza ni watu wa kusikiliza best offer kama unampa huyu bwana £750 sawa na sh. mill 1.5 anakuachia mkweche. Freight mpaka Dar mill 1.5. kwa hio mill 3 kitu iko bongo, mazagaa mengine ya ushuru n.k
weka mpaka mill 2.5 jumla millioni 5.5 gari iko mitaani.
 
Asante sana mkubwa kwa ushauri wako.

Barabara za bongo ntakazozitumia mimi ni lamu tupu. Mimi nataka gari ya kwenda na kurudi kazini basi.

Inavyoonekana itabidi nichukue hivyo vidude vidogodogo vya japani, au nikaze buti kidogo. Ila kwa vimishahara vyetu hivi sijui nitafika lini huko kwenye 5.5M. Ila natumanini nikishafika huko shilingi itakuwa haijashuka thamani sana, maana hukawii kuambiwa inabid nijivute vute tena nifike hata 7M hivi.
 
...pikipiki wakati wa ajali 'body' ni mwili wako...! yanini kugeuzwa sambusa bure?

Mkuu mbona hata gari mwili unakuwa sambusa ajali ni ajali hata ukiwa una jog toka Mbezi mpaka Posta unaweza geuzwa sambusa vile vile.
Cha muhimu aangalie miundo mbinu ya bongo ovyo ovyo sana anunue pikipiki itamsaidia kuwahi kazini na nyumbani pia maana foleni ya Bongo bana mpaka inakera.
 
...haya bana,

vile vile sipendelei mamsapu akikaa mkao wa ~kuji express~ kwenye hizo 'tuk-tuk'... akheri ya kule Unguja na zile Vespa zetu, mikao ya 'chai maharage'.
 
vile vile sipendelei mamsapu akikaa mkao wa ~kuji express~ kwenye hizo 'tuk-tuk'... akheri ya kule Unguja na zile Vespa zetu, mikao ya 'chai maharage'.

Hahahaha usiombee awe na maumbile makubwa nyuma alafu umpakie dah s nchezo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom