Samahani kwa nitakaye mkwaza kwa hili.
Kuacha kazi kuna pande mbili,,
1. Kufanikiwa na kuishukuru akili iliyokutuma kufanya hivo na
2. Kushindwa na kujutia hasa kwa kuilaumu akili iliyokutuma kufanya hivo
Ikumbukwe hakuna asiye bisha kua ukiajiriwa ujue unafanya kazi kwa aliyejiajiri kataa ukubali na ukifuatulia chenye gharama hua ni bora
Kujiajiri ni bora na kuna gharama yake kwani unapoajoriwa na mtu inaonekana kabisa ujuzi ulio nao umeahindwa kuutumia na ukakubali akili ya mtu aliyejiajiri kuutumia,, hapo mi nasema ni mgando wa fikra na kutafuta unafuu wa maisha pasipo ku-u- weka uhalisia wa maisha
Naamini watanzania wengi hasa vijana tunaishi maisha ya maigizo sana na hicho hutufanya sisi kushindwa kufanya maamuzi kwani tumeshindwa kujitoa katika dimbwi la kutegemea akili zetu, yaani tumekua tegemezi kwa kila kitu,,
Kingene sisi ni wavivu sanaa na ndio tunapenda kutumikishwa na mtu aliyefanya juhudi akaukana uvivu wa kufikiri na kutenda, kwa mfano mpaka hapo yawezekana hauna katiba ya maisha yako ndio maana unashindwa kuamua.
Cha kukushauri sasa ni hiki,,
Kama unataka kuacha kazi jiandae katika kila nyanja
Kisaikolojia
Kiakili
Kiuchumi( matumizi)
Na vilevile unapaswa uandike project ya maisha yako inje ya kazi ili itumike kukuongoza utakapo kua inje ya kituo
Ukumbuke kabisa kua ukijiari usitegemee kukosolewa kwa utendaji m bovu utakao ufanya na hapo ndio itakua kifoa cha fikra kitakukumba,, ujuzi uliokua unaufanyia kazi kule uzidishe mara dufu ili kuongeza uzalishaji wako hapo jipe mda fuatilia jeee uko ndani ya chaki ya mipango yako??
Ongeza juhudi katika kazi utakayoichagua ipe muda zaidi ya ule wa kazi ya kuajiriwa tune your mind epuka mawazo finyu ya kuwaza kummilikisha ujuzi mtu mwingine. Jitume na amua kwa juhudi.
Yafuatayo yazingatie kwa manufaa yako
1. Andaa mchanganuo wa kazi unayotaka kujiajiri kisha ufanyie utafiti
2. Anza sasa baada ya kumaliza mchanganua lakini hakikisha umeuchambua vizuri kama unavofanya hapo offisini kwa muhindi
3. Muandae mkeo awe wa kukutia moyo na kukushika mkono kwani ikumbukwe unaingia katika mapambano
4. Punguza matumizi kwako kwa kila namna mpak mshahala wako unaojilipa baada ya kazi mf.starehe, burudani n.k
4. Acha wizi ndani mwako na hasa tabia ya udokozi, hapa namanisha unachukua kijisent hata kidogo halafu hata hukiandikii kinapotea tuu hivihivi bila ya kujua ukifanya hivo mwisho wa siku utashindwa kujua gharama halisi ya maisha yako kwa kipindi unachojifanyia kazi
Hayo ni baadhi tu ya ushauri wangu wa bure
IPE AKILI NAFASI YA KUPAMBANA KWA MANUFAAA YA NAFSI YAKE NA SI KWA MANUFAA YA MUHINDI
IKUMBUKWE KUA NAFSI YALO INAUMIA KUONA AKILI YAKO INATESEKA KWA AJIRI YA MUHINDI