Mkuu,ushauri wangu usiache kazi ghafla kabla hujasuka mikakati ya shughuli utakayoifanya baada ya kuacha kazi,kujiajiri ni jambo la busara sana japo lina changamoto kubwa ya ubunifu na ili ufanikiwe katika hii sekta inabidi uishinde hii changamoto ya "ubunifu" kuepuka kufanya anachofanya mwingine kwa level ileile,kaa chini Fanya utafiti wa kutosha juu ya unachotaka kufanya kisha anza kuendesha huo mradi wako ukiwa kazini na utapoona mradi wako umekakamaa unaweza kusimama kwa miguu yote miwili hapo nakushauri acha kazi rasmi jikite kwenye miradi yako,ila kubwa kuliko yote mtangulize MUNGU katika kila unalotaka kulifanya uombe hekima na busara zake zikuongoze
Suala la pesa ya muhindi kuwa haifanyi jambo la msingi nafananisha na ule usemi wa pesa ya boom la chuo huwezi fanyia jambo la maana zaidi ya kununua nguo na subwoofer, mkuu hilo suala lipo kiimani sana na ukweli ni kwamba tunasahau kwamba 10% ya mapato yetu kila siku ni Mali ya MUNGU hivo yapasa tumrejeshee yeye mwenyewe,mkuu nakuhakikishia hakuna ulinzi mzuri wa mapato yako zaidi ya kumtolea BWANA fungu la kumi pesa zako utaziona utamu wake na utaztumia as ulivopanga bila ufujaji wa nia ovu ya shetani.