Nilibahatika kuajiriwa katika moja ya kampuni ya wahindi miaka mitatu na nusu iliyopita baada ya kukaa nyumbani bila kazi kwa mwaka mmoja na nusu tangu kuhitimu chuo kikuu.
Nilianza na mshahara wa laki tano (net salary) lakini kwa sasa nakaribia milioni moja (net salary).Kampuni hiyo ni ya kifamilia zaidi,wakati naajiriwa kulikuwa na Managing Director mwanaume ambaye pia ndiye mwanzilishi wa Kampuni hiyo.Kwa bahati mbaya,mwanzoni mwa mwaka jana MD huyo alifariki dunia (R.I.P) na sasa kampuni inaongozwa na mke wake.
Kwa kweli kwa kipindi cha huyo MD wa kwanza mambo yalikuwa poa sana,wafanyakazi tulikuwa tunaheshimika,tunajaliwa na kusaidiwa kwa kila namna ilivyowezekana,lakini baada ya kiti kukaliwa na huyu mama,mambo yamebadilika,dharau,manyanyaso na kila sura ya kihindi unayoijua wewe sisi tunaiona live
lakini jambo la pili,kwa muda wote huo najiona kama sifanyi kitu chochote,hela unaipata hujui inaishaje,wafanyakazi niliowakuta(hata wenye mishahara mizuri) bado wapo ktk lindi la umaskini wa kutupwa kila kukicha najiona kama vile bado sijapata kazi (Kuna kalugha nakasikia mtaani kwamba pesa ya mhindi huwezi kuifanyia chochote).
Baada ya kutafakari hayo yote na mengine mengine sasa nafikiria kuacha kazi hapa.Nafikiria japo kuchukua akiba yangu iliyopo huko kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii ili nijiajiri mwenyewe maana mtaani napo kila siku kilio ni ukosefu wa ajira.
Je,wadau mawazo yangu ni mwafaka?
Naombeni ushauri wenu.