Nataka kuacha kazi serikalini Tanzania bara

bidam90

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2013
Posts
273
Reaction score
203
Natumaini mu wazima wa afya!Nipo njia panda nahitaji ushauri

Kwasasa nimeajiriwa chuo cha serikali Tanzania bara.Niliamua kuomba nafasi kutokana na changamoto ya ajira ya fani niliosomea.Nimepata nafasi ya kazi mamlaka ya uthibiti wa nishati na mafuta Zanzibar ambayo ni taasisi ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.Nafikiria kuacha kazi ya kufundisha chuo na kwenda Zanzibar ila napata wakati mgumu. Je taratibu za kuacha kazi zipoje serikalini?na vp haitaniletea shida baadae kwani tayari jina langu lipo utumishi na check number pia!!Zanzibar wana wizara yao ya ajira na tume ya utumishi ambayo haihusiani na huku bara.

Naamini kuna watu wazoefu na wenye kujua au walishawahi kuacha kazi serikali Tanzania bara na kwenda Zanzibar. Naombeni ushauri wana jf wenzangu
 
Unapata wakati mgumu kuwaacha watoto wa kutafuna bure baada ya kuwapa test na quiz ngumu
 
Hapo Mkuu unaacha tu kama unaenda kukojoa hiyo ndio mazima hurudi tena!
 
Natumaini mu wazima wa afya!Nipo njia panda nahitaji ushauri

Kwasasa nimeajiriwa kama Tutorial Assistant chuo cha serikali Tanzania bara.Niliamua kuomba nafasi kutokana na changamoto ya ajira ya fani niliosomea.Nimepata nafasi ya kazi mamlaka ya uthibiti wa nishati na mafuta Zanzibar ambayo ni taasisi ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.Nafikiria kuacha kazi ya kufundisha chuo na kwenda Zanzibar ila napata wakati mgumu. Je taratibu za kuacha kazi zipoje serikalini?na vp haitaniletea shida baadae kwani tayari jina langu lipo utumishi na check number pia!!Zanzibar wana wizara yao ya ajira na tume ya utumishi ambayo haihusiani na huku bara.

Naamini kuna watu wazoefu na wenye kujua au walishawahi kuacha kazi serikali Tanzania bara na kwenda Zanzibar. Naombeni ushauri wana jf wenzangu
Sikushauri uje Zanzibar utajuta....ni watu wanafiki, wavivu na hawapendi wabara kuja kufanya kazi huku pia kimaendeleo kupo nyuma.

Mishahara yao pia iko chini sana kuliko bara hivyo fikiria mara mbili mbili
 
Mkuu mie ni mzanzibar ndo mana nimepata kazi huko!!Na navyojua taasisi za udhibiti kama EWURA,ZURA kidogo mishahara yao ipo vizuri na posho ni nyingi kwani wanajitegemea mishahara yao hawatumii salary scale za utumishi
 
Andika barua ya kuacha kazi ndani ya saa 24. Nenda kale bata huko
 
Natumaini mu wazima wa afya!Nipo njia panda nahitaji ushauri

Kwasasa nimeajiriwa kama Tutorial Assistant chuo cha serikali Tanzania bara.Niliamua kuomba nafasi kutokana na changamoto ya ajira ya fani niliosomea.Nimepata nafasi ya kazi mamlaka ya uthibiti wa nishati na mafuta Zanzibar ambayo ni taasisi ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.Nafikiria kuacha kazi ya kufundisha chuo na kwenda Zanzibar ila napata wakati mgumu. Je taratibu za kuacha kazi zipoje serikalini?na vp haitaniletea shida baadae kwani tayari jina langu lipo utumishi na check number pia!!Zanzibar wana wizara yao ya ajira na tume ya utumishi ambayo haihusiani na huku bara.

Naamini kuna watu wazoefu na wenye kujua au walishawahi kuacha kazi serikali Tanzania bara na kwenda Zanzibar. Naombeni ushauri wana jf wenzangu
Nilijua hili ni bandiko la kuacha ajira na kwenda kujiajili.Du nimepoteza muda wangu bure.
 
Zenji mishahara midogo sana,
Mwalom bachelor anaanza na laki nne km basic salary
 
takwimu zinaonyesha kuwa zanzibar kuna kiwango kidogo cha vvu,kale raha mzee unachelewa.
 
Mkuu andika barua weka sababu zajo za msingi za kuacha kazi.
 
Back
Top Bottom