Nataka kuacha chuo nijihusishe na shughuli za ujasiriamali

slow_learner

Senior Member
Nov 24, 2016
139
110
Habari ndugu wana JF
Mimi kutokana na maisha kuwa magumu nafikiria kuacha chuo ili nijihusishe na uzalishaji Mali.
Nazungumza haya kutokana na kauli ama ushauri wa POLEPOLE kwa wanachuo waliokosa mkopo.

Nimefikia uamuzi huu ila sijajua nianze kufanya shughuli gani.
Duh! Itanibidi niitekeleze kauli mbiu ya mheshimiwa sana.
 
mkuu hao watu uliowataja ukitekeleza(ukifuatilia) wanayoyasema hautakaa uonje ladha ya mafanikio maana wao wenyewe hawajielewi wanataka/fanya nini hasa huyo slow slow
 
Kwa kauli hii nakushauri umalize kwanza chuo.
 
mkuu hao watu uliowataja ukitekeleza(ukifuatilia) wanayoyasema hautakaa uonje ladha ya mafanikio maana wao wenyewe hawajielewi wanataka/fanya nini hasa huyo slow slow
Mie nahisi anawasilisha ujumbe kutoka juu.
Anashaur tuachane na chuo then tutafute ada na tukipata ndo turudi chuo.
Mie japokuwa nimefikia chuo naona kama napoteza muda bora niachane na chuo mazima na nikipata hela nitasoma hata open university.
 
Anza hata kushona viatu kwa mtaji wa 50,000/- tena ufanyie karibu na chuo ambapo unazika vitabu na kuanza kusaka pesa ili marafiki zako ndo wawe wateja. si mbaya pia ukawauzia unga wale wapenda dona wanaoishi maghetoni unafuata tu kwa wakulima
 
Nadhani hapo anataka akachakarike mtaani hata vibarua vidogo apate kianzio kama kamtaji, sasa huo muda anaochakarika mtaani apate hiko kidogo na masomo yanampita.

sasa sina uhakika kama anayo hela cash ya kuendelea na chuo.
Kwa sasa sina hiyo pesa cash ya kuendelea na chuo ndo Maana nikasema niachane na chuo sababu upepo wa mbele hausomeki na maisha ya Dar es salaam ni magumu sana
 
Nasuport hoja. Ila uko unakoelekea hakikisha unamtaji. Kama mtaji unao hutajutia
 
Back
Top Bottom