Kijana Style
Member
- Apr 3, 2014
- 37
- 10
Nimeweka modem router nyumbani,ninailipia kila mwezi kwa shirika la simu nchini,Modem router yenyewe ni aina ya TP Link,150 Mbps,Wireless N ADSL2+, Model No.TD-W8951ND,tatizo langu kila nikimpatia mtu anitilie password ili watu nje wasiweze kutumia internet yangu, nashangazwa kuona hata wiki haifiki nakuta nje ya nyumba yangu vijana wanachat kwa kutumia net yangu ambayo imeshafunguka au imeshafunguliwa na wenye ujuzi wa kufungua passwords,naomba kwa yeyote mwenye ujuzi wa kuifunga modem router yangu anifundishe njia ya kuweka password,nitakuwa kila mara nabadili password ili wasiweze kui-hack.Nina komputa ya kawaida natumia windows xp profesional. Asanteni