Kuhusu matumizi ya data modem za Zantel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhusu matumizi ya data modem za Zantel

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by alsaidy, Feb 16, 2012.

 1. alsaidy

  alsaidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wakuu,

  Naomba kuwakilisha kama ifuatavyo:-

  Tunatumia modem ya zantel katika kupata internet katika office iliyo na wafanyakazi watatu nikiwepo mimi mwenyewe. Tumenunua wireless router za mwanzo zilizouzwa na zantel ambazo unaplug modem yako katika hiyo router then ndio inatupa wireless na sehemu ya cable kwa user 1.

  Hivi karibuni tuliweka 2Gb mida ya 1 usiku kufika saa 7 mchana siku ya pili ngoma imekwisha. Kila tukipiga hesabu ni almost impossible kwa kipindi chini ya 24hrs kumaliza 2Gb. Kumbuka wireless tumeweka password kwa kutumia WEP ili mtu wa nje asipate access.

  Nilivyokwenda office za Zantel walinitolea matumizi yangu kitu ambacho sielewi wala sijui zimetafunwa vipi.

  Msaada kwenu wana JF kwa mambo matatu:-

  1. Kuna mtumiaji yoyote anaetumia modem ya zantel ambae matumizi yake hayalingani na matumizi halisi na modem inavyokata?
  2. Kuna software yoyote ambayo ninaweza ku install ambayo ita govern matumizi yangu ya internet ili nipate ku compare na data za zantel?
  3. Je mitandao mengine iko kama hii au?

  Kitu ambacho nimekipenda sana zantel ambacho kinachonivutia sana ni speed ya internet it is just superb!!!

  Ki ukweli nahisi zantel wanatuchakachua lakini nataka kupata ushahidi wa kutosha katika hili.
   
 2. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,231
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  ni ukweli mkuu ZANTEL is the fatest internet kwa sasa! but one of the main problem of zantel in gharama

  ni ukweli BUNDLE za hawa jamaa hazilingani na uhalisia wa bunde, ukiweka 500mb, just downloding two articles UNAAMBIWA IMEISHA, mimi now nimeachana nao, huwa natumia SASATEL. SASATEL wao gharama zao ni very cheap, but SPEED yao, hasa
  wakati wa usiku balaaa!! unaezalia,

  pia nimewahi jaribu kuweka bundle sawasawa ya 1.5gb katika zantel na katika sasatel amini nakuambia kwa matumizi yanayolingana hapa ofsn katika pc 2, baada ya siku 3 nikacheck balance, ZANTEL nikakuta ina 370mb while SASATEL Ikiwa na 967mb. so kuwa makini sana na zantel

  pia kitu kingine, zantel ukimbaliza bundle kabla muda wa kuexpire hujaisha, huweze tena kuweka bunde hata ukiweka watakukata malipo ya kawaida, otherwize uweke bundle kubwa ya iliyoisha, tofauti na sasatel ambapo ikiisha bundle hata kama expire period bado unauwezo wa kuomba bundle nyengine.

  kwa mawasiliano ni PM
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  2Gb sio nyingi kwa watu watatu ni kama 600MB each, mtakuwa mmemaliza tu. Nadhani unapata hisia kuwa imeisha haraka kwa sababu ina spidi nzuri, kitu ambacho kingechukua masaa kudownload kwenye network nyingine kinashuka ndani ya dakika chache, pia spidi ikiongezeka matumizi yako nayo yanabadilika ukiwa na net slow unakuwa huna hamu ya kufungua baadhi ya site.

  Install NetWorx kwenye kila PC kuona matumizi. Bandwidth monitor, bandwidth speed test, bandwidth and traffic monitoring tool for Windows
   
 4. j

  junior05 Senior Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu umepata majibu mazuri ila kwa kuongezea kumbuka kunaweza kukawa na hidden activities kwenye hzo PC husika,mfano windows update,security softwares(untviruses) bila ya ww kuwa aware,I can assure u sometime a virus is enough to take care of u r valuable bandwith wothout u r knowledge
   
 5. alsaidy

  alsaidy JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Asante mkuu kwa majibu yako mazuri. Ni kweli unachozungumza nilichokifanya windows update zote nime disable then sasa hivi na install hiyo software aliyenipa mkuu hapo juu.

  Nafikiri baada ya kiunstall hii software nina imani nitapata majibu mazuri.
   
 6. alsaidy

  alsaidy JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu nashkuru kwa msaada wako wa melezo pamoja na hii software. Nina imani itanisaidia
   
 7. alsaidy

  alsaidy JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Asante mkuu kwa ushirikiano na maelezo mazuri......
   
Loading...