Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
.... Zilipendwa origino -kati ya miaka 1975-1995 naomba awasiliane nami kwa PM...
Jamani mwenye Zilipendwa origino kati ya miaka 1975-1995 naomba awasiliane nami kwa PM.
Hususan natafuta Nuta.Juwata/Ottu, Mlimani Park, Vijana Jazz, Marquis, Mzee Makassy, OSS, Kyauri Voice, King Kiki, Biashara Jazz, Kimulimuli, Mwenge Jazz, Dar Jazz, Bima Jazz, Tshimanga Assosa na Mambo Bado, Nk.
mchUngaji wa kondooo wa BWANA....
heee umefikwa na nini mwenzetu,unataka niymbo???mie nilifikiria wachungaji hawasikilizaji nyimbo.heshima yako,mie ninazo za taarab kama za NADI IKHWAN SWAFAA na CULTURE MUSICAL CLUB jee zitakufaa??
mchUngaji wa kondooo wa BWANA....
heee umefikwa na nini mwenzetu,unataka niymbo???mie nilifikiria wachungaji hawasikilizaji nyimbo.heshima yako,mie ninazo za taarab kama za NADI IKHWAN SWAFAA na CULTURE MUSICAL CLUB jee zitakufaa??
Mfalme Daudi alipiga zumari na kucheza muziki, alokwambia kusikiliza mziki ni dhambi nani?
Je unazo za Bi. Shakila na yule Mzee alikuwa ana madongo makali? je wakumbuka bunduki risasi hewa? pochi?
Kama unazo naomba nichomee, halafu tuwasiliane jinsi ya kutumiana!
mchungaji.....
wakati ninapoongelea zilipendwa za tarab za znz,akina shakila na wengine walikuwa bado wanacheza TANCUT ALMASI,MAQUIZ,VIJANA JAZZ n.k,kwa maana hiyo mie hao nimeanza kuwajua majuzi tu.lakini kuna nina vigongo vya TAARAB ASILIA kama za MOHD ILYASI,FAUZIA,RUKIYA RAMADHAN, n.k hizo ndio nyimbo zetu yakhe sio za siku hizi akina khadija kopa na wezake TAARAB DANSA.
kwa hiyo mchungaji kama wataka hizo naweza kukuchomea na kukufikishia kunakohusika.
endelea kuwachunga KONDOO WA BWANA.muombee sana ANDREW CHENGE mola amsamehe madhambi yake.amin.
Kama unazo naomba nichomee, halafu tuwasiliane jinsi ya kutumiana!
Mhandisi,
Nimekuuliza kuhusu Bi. Shakila si kuhusu Khadija Kopa bwana. Ama humfahamu Bi. Shakila weye...!
Je Issa Matona unaye? na yule bibie malkia wa Afrika Kulthum wa Misri wamfahamu?
piracy? kama sio naomba msinipige mawe pls. Halafu Mchungaji si umesema unataka origino?
ZITAPATIKANA CD 15