jmapunda
JF-Expert Member
- Jul 9, 2015
- 731
- 2,923
Wakuu,ingawa mimi bado kijana mdogo tu nimekuwa nikivutiwa na muziki wa dansi ule wa zamani uliokuwa ukiporomoshwa na bendi kama Mlimani park, OSS, Juwata,Marquis,Matimila, Bima, Tuncut nk.
Muziki huu ulikuwa ni mzuri sana kwani vyombo na sauti za waimbaji zilipangiliwa kwa ustadi wa hali ya juu.Ulionyesha ni jinsi gani binadamu anaweza kuchezea sauti kadiri alivyopenda ama wapiga ala walivyoweza kuchezea ala zao kwa umahiri wa hali ya juu bila msaada wa nyenzo kama computer!
Live show ilikuwa live kweli tofauti ya sasa ambapo huwa ni kelele tu na kuwataka mashabiki wapige kelele au washangilie...muziki wa zamani utashangilia bila kuombwa!
Enzi hizo unaweza kuahirisha hata kula kama utabahatika kuingia kwenye shoo za wanamuziki kama Maneti,Marijani,Bitchuka,Zahir Ali,King Kiki,Moshi,Kasongo Mpinda,Kasaloo na Kyanga nk.
Nini kifanyike kuuokoa muziki huu?Radio nyingi za binafsi ziupe nafasi hewani.Tatizo kubwa mapresenta wengi ni vijana wao wanajua bongo fleva tu.Wizara husika iangalie namna ya kuuokoa muziki huu. Naamini kuna watu wengi tu wanaovutiwa na muziki huu.Ukiwezeshwa ni ajira tosha. Kama unaniunga mkono...taja wimbo mmoja wa zamani na bendi au mwanamziki aliyeshiriki.
Nawasilisha.