Natafuta wimbo wa Rafael alikuwepo by Fred Saganda

mkuu figganigga marehemu Mr. Abel alikuwa anaimba RnB kama za Mr. Paul. Saganda namkubali sana kwani baada ya yeye kutoa hiyo ngoma yake ndipo ulipojitokeza utitiri wa wasanii wakirap kwa kutumia idea yake. Sijui kwa nini jamaa hakusikika tena.
Mkuu jamaa aliingia kwenye mambo ya kutayarisha nyimbo. mia
 
Last edited by a moderator:
Ni jinsi gani??ni namna gani tutaishi duniani paka siku tunasema buriani,jamaa anaimba kwa lafudhi ya kichaga Hiv,MASAWE alikuepo,kimaro alikuepo,mushi alikuepo kawataja wengi sanaa!!
 
mkuu figganigga marehemu Mr. Abel alikuwa anaimba RnB kama za Mr. Paul. Saganda namkubali sana kwani baada ya yeye kutoa hiyo ngoma yake ndipo ulipojitokeza utitiri wa wasanii wakirap kwa kutumia idea yake. Sijui kwa nini jamaa hakusikika tena.


Enzi zile hakukuwa na kiki za instagram
 
Kama ni namna gani utawini maishani tafuta kazi ya kuwasifu watu...utapata cheo fasta.
 
Hahahha!! umenikumbusha mbali sana mwenye thread hii,huyo jamaa anaitwa Fred Saganda aka SAGANDA,alikuwa anasoma zamani kaole kule bagamoyo baadae akawa lecturer pale pale kaole,ni producer wa music na mtengeneza film,na anatengeneza pia hizi short film mfano za ukimwi zinazozaminiwa na mashirika ya nje,kwa kweli kipaji anacho,mi namjua vizuri sana mana nilisoma nae pale mlimani na hata wakati tukitengeneza nyimbo zetu enzi hizo tulikuwa tunamwita aje atoe ushauri wake alikuwa peace sana.kwa sasa anafanya maigiz kwenye stesheni ya STAR TV,kwenye kipindi cha PICKABOMB!!,kile watu wamevaa kama masnamu halafu wanaigiza rafudhi ya kichaga na kipemba, we tazama star tv utamwona tu yeye ni yule jamaa anayeigiza kwa kichaga.Jamaa kwao alikuwa mambo supa sana mana dingi alikuwa ni profesa na yeye alikulia mule ndani chuoni ndipo baba yake anapokaa,inasemekana dingi yake alikuwa hataki kabisa jamaa asomee maswala ya muziki ila jamaa muziki ulikuwa kwenye damu ikabidi dingi mwenyewe asarende.
Kwa kifupi hawa ni watoto wa kishua wa maprofesa yeye pamoja na wengine akina HASHIMU DOGO,wote hawa wamekulia ndani mule udsm watoto wa maprofesa.
Mara ya mwisho nilikutana naye mwenge kituo ch mabasi miaka mingi sana nyuma,alikuwa anatoka bagamoyo kaole nafikiri,siku zote alikuwa anatembea na gitaa lake,anaimba rap lakini ni mwimbaji mzuri wa reggae pia sema kutokana na uzushi wa ma-DJs wa bongo watu wengi wenye vipaji waliamua kusarenda akiwemo saganda kuepuka manyanyaso yao mana walikua wanajifanya miungu-watu hasa hasa CLOUDS wale jamaa ni mashetani wakubwa sana siwapendi kabisa ndio walioua mziki wa bongo.
natamani sana kujua namna ya kuzipata zile filamu zake zilikuwa zina mafundisho sana. zilikuwa zinahusu athari za madawa ya kulevya na bangi. hebu tuambie namna ya kuzipata maana vijana wetu wanapotea hakuna mafundisho yoyote ya maana wanayopata kupitia hizi Bongo movie za sasa.
 
Kuna msanii simkumbuki jina aliimba wambo wa rafael. baadhi ya mistari ninayo kumbuka ni;
"ninamna gani, ni jinsi gani tutawin maishani mpaka siku tunasema buriani, ni jinsi gani yesu wangu.
tulikua tumekaa pale bar rafael akaja akatuangalia machoni akatudharau akaingiza mkono mfukoni akaagiza walete kama tulivyo. mariam alikuwepo, joshua alikuwepo na yule kijana anaye kaa pale kona nani? chua eeh! eti chua nae alikuwepo". hayo ni baadhi ya maneno ninayo yakumbuka. mwenye huo wimbo nauomba. thanx. mia

====


Nilibahatika kusikiliza Album ya huyo jamaa yenye huo wimbo ni balaa sana. Ana ngoma yake humo inaitwa "Makota Mapilau" ni shidaa. Saganda ana kipaji sana sema kagoma kuwa commercial hadi leo anafanya underground
 
mkuu figganigga marehemu Mr. Abel alikuwa anaimba RnB kama za Mr. Paul. Saganda namkubali sana kwani baada ya yeye kutoa hiyo ngoma yake ndipo ulipojitokeza utitiri wa wasanii wakirap kwa kutumia idea yake. Sijui kwa nini jamaa hakusikika tena.
Aliacha kuimba. Anafanya production. Lakini pia ndie anayetengeneza zile audio za katuni za Ubongo Kids. Yuko njema sana jamaa, na anaendeleza rap zake za kichagga kwenye hizo hizo katuni
 
Ni namna gani tutawin maishani
yesu wangu,ni namna gani
yereuuuwiiii,Kidogo tu huyooo
Rafael na motakaa,,Hahahaha!!Mala
ya kwanza kuuskia
ni Mwaka jana
Kwenye kipindi
cha Shujaaz cha
DJ Tee,Niliuelewa
sana Aisee
 
Massawe alikuepo,Kimaro alikuepo,
Mangi alikuepo,
Urassa alikuepo,
Lema alikuepo,
Urio alikuepo,
Na huyu mtoto
wa jirani nani uyu?
Chua,eeh et chua
nae alikuepo!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom