Natafuta shule ya kujitolea kufundisha masomo ya Hesabu na Fizikia, cha msingi nipate sehemu ya kulala na kula tu

Feb 24, 2021
14
22
Habari zenu jamani, hakika Dunia tambalabovu niukweli kwamba maisha yamenipiga nimepigika nipo chapachapa. Hivyo ninaomba kwaanaeweza kunisaidia Nipate shule yoyote ya kujitolea sitaki kulipwa hata sent chamsingi nipate chakula cha mchana tu jioni nitapiga pasi ndefu.

Mimi nimuhitimu wa chuo cha kati chuo cha ualimu tabora nimesomea ngazi ya stashahada masomo ya physics na mathematics.

Kwa yeyote mwenye mchongo anisaidie imefika wakati natembea njiani huku naongea pekee angu kwa msongo wa mawazo, na njaa inavyonitandika. Asante
 
Dah pole dadangu hakika ajira imekuwa janga Sasa shule hazna walimu siasa zmekuwa nyingi.

Mungu akupe hitaji lako dada JF n sehemu pana utafanikiwa tu.
 
Habari zenu jamani, hakika Dunia tambalabovu niukweli kwamba maisha yamenipiga nimepigika nipo chapachapa. Hivyo ninaomba kwaanaeweza kunisaidia Nipate shule yoyote ya kujitolea sitaki kulipwa hata sent chamsingi Nipate chakula cha mchana tu jioni nitapiga pasi ndefu...
Uko wapi?

I can feel what you're going through.

Mimi ninewahi kwenda kwa waosha magari kuwaomba niwe nawasaidia kuosha ila wawe wananipa buku tu🤣 ya kula. Wakati huo 2017 nimetoka chuo.
 
Pole sana! hakika duniani ni changamoto sana

Masomo uliyoyataja kiukweli yanachangamoto kwenye kupatikana walimu, hivyo binafsi naona ni advantage kwako.

Nafikiri shida kubwa haujaexpose proposal yako kwa wahitaji. Jaribu tembelea shule zilizonje ya miji, sio za mjini.

Binafsi nilipokuwa nasoma form six- nilikuwa natamani kupata kazi temporally ya kufundisha nikishamaliza shule na kweli nilipomaliza tu, kwa kuwa nilisoma PCM nilipotembelea shule ya kwanza tu kuitembelea nilipewa kazi
 
Kama ni mdada kama jina lako lilivyo daah pole sana... ungekuwa mwanaume ningekwambia kabebe mizigo upate hela. Japo waalimu wa physics na chem wanatafutwa sana mbona nini shida yani?
 
pole sana! hakika duniani ni changamoto sana

masomo uliyoyataja kiukweli yanachangamoto kwenye kupatikana walimu, hivyo binafsi naona ni advantage kwako....
Shule gani nije maana jana nimeenda shule takribani nne, mburahati secondary, nikaenda kibasila secondary, tambaza na jangwani secondary zote wananiambia hawana accommodation wala msosi hivyo wakanishauri niendelee kutafuta nisichoke
 
pole sana! hakika duniani ni changamoto sana

masomo uliyoyataja kiukweli yanachangamoto kwenye kupatikana walimu, hivyo binafsi naona ni advantage kwako..
Hata mimi nimefundisha sana miaka ya 2012-2014 ila alivyoingia Shetani na mbwembwe zake za elimu bure zikavuruga kila kitu.

Sasa Hivi shule havina pesa ya kulipa walimu wa kujitolea na wakuu wa shule wanaogopa kuwaambia wazazi wachangie, wakihofia kufukuzwa kazi.
 
Kama ni mdada kama jina lako lilivyo daah pole sana... ungekuwa mwanaume ningekwambia kabebe mizigo upate hela. Japo waalimu wa physics na chem wanatafutwa sana mbona nini shida yani??

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
Shida ni kwamba kila shule nikienda wananiambia hawana uwezo wakunipatia chakula tena cha mchana tu sitaki chai wala dina
 
Habari zenu jamani, hakika Dunia tambalabovu niukweli kwamba maisha yamenipiga nimepigika nipo chapachapa. Hivyo ninaomba kwaanaeweza kunisaidia Nipate shule yoyote ya kujitolea sitaki kulipwa hata sent chamsingi Nipate chakula cha mchana tu jioni nitapiga pasi ndefu. Mimi nimuhitimu wa chuo cha kati chuo cha ualimu tabora nimesomea ngazi ya stashahada masomo ya physics na mathematics. Kwayeyote mwenye mchongo anisaidie imefika wakati natembea njiani huku naongea pekee angu kwa msongo wa mawazo, na njaa inavyonitandika. Asante
Sina shule, ila pa wewe kula, kulala na mitoko kibao papo. Karibu home kwangu
 
Back
Top Bottom