Anaandika Mwl. Asiyekuwa na Darasa wala Shule

Joined
Jul 23, 2018
Posts
46
Reaction score
66
NATUMIA SIKU HII YA MAADHIMISHO YA WALIMU, KUZUNGUMZA NA WATANZANIA WENZANGU NA SERIKALI.

Usichoke kusoma!! Soma, Soma, Soma ujumbe wangu Mimi Mwalimu nisiye na Darasa la kufundisha, Vyeti vyangu vya Kuhitimu Chuo Kikuu vimekoswa kazi kwenye begi!!

Mimi ni Kijana wa Kitanzania, ambaye nimetimiza miaka 30 sasa. Naitwa Josephat.
Nimeona niandike ujumbe wangu huu siku hii ya leo ili kwa yeyote atakaefanikiwa kuusoma, aone jinsi ya kunisaidia ama kusaidia wengine walio na mazingira kama yangu.

Kwa taaluma Mimi ni Mwalimu. Nimehitimu mwaka 2017.

Nikiwa kidato cha tatu Mwaka 2010, nilifukuzwa Shule na Mwalimu wangu Mkuu kwa kukoswa Ada ya kulipia Mwaka.
Wakati huo Baba yangu (miaka 86 kwa wakati huo) alikuwa ameanza kuugua, japo akiwa bado hajachoka. Baba akatoa kauli kwamb Ardhi iliyopo kidogo pale Kijijini kwetu iuzwe ili niendelee na Masomo (Japo wakati naingia kidato cha kwanza Ardhi pia iliuzwa nikafanikiwa kuingia).
Tuliuza Ardhi nyingine kwa Mara ya pili, nikapata fedha nikarudi shule.
Mwaka 2011 nimehitimu Kidato cha Nne. Natakiwa kwenda Advance, sina hela tena.
Ikabidi Baba auze tena kauwanja ambako kalikuwa kamebaki (Ninavyoandika hapa, nyumbani hakuna Ardhi ya kuweza kulima, kuna uwanja wa mahali zilipo nyumba zetu za kuishi tu).
Baba yangu aliamini nikisoma basi nitapata kazi nzuri na kurejesha vyote hivyo vilivyopotea. Hapa sijaelezea juhudi za Mama yangu alivyokuwa anatoka kwenda kufanya vibarua na kuniletea pesa ili kulipa shuleni, lengo nisome. Asante Mama yangu.
Mipango ya MUNGU mwanadamu hawezi kuzuia. Mwaka 2012 nimeingia tu kidato cha Tano, nikajulishwa kuwa Baba yangu amefariki!! So sad!!. Tena alifariki kwa kukoswa pesa ya matibabu (alifia nyumbani).
Nilitamani niende kumzika Baba, lakini sikuwa na nauli ya kurudi nyumbani kumzika Baba. Nikapiga moyo konde!!
Baba yangu akatangulia, nikabaki na Mama yangu!!

Mwaka 2014 nimehitimu Kidato cha Sita, nikajiunga Chuo Kikuu mwaka wa Kwanza.
Nikasoma kwa taabu sana mwanzoni kwa kukoswa Mkopo Mwaka wa kwanza, (nikachangiwa na watu, maana kwenye ukoo na Familia nimesoma Mimi tu), MUNGU saidia mwaka wa pili nikapata Mkopo wa Serikali hadi mwaka wa Tatu.

Nimemaliza mwaka 2017 nimerudi nyumbani, nikitazamia Ajira Serikalini.
Nimetuma maombi Serikalini tangu mwaka 2018 hadi leo Mwaka 2021 sijawahi kuchukuliwa na Serikali ili kwenda kufanya kazi niliyosomea, na ninaipenda sana.
Kwakweli nilikata tamaa. Mama yangu ananiuliza kila siku, "mbona huajiriwi Serikalini, au hukumaliza Masomo?" Namwambia hapana Mama, nilimaliza nasubiri Serikali iniajiri, labda bahati yangu bado.
Mama yangu kwakuwa hakusoma, anachoka na anakata tamaa kila akiniona.
Sina kazi na sina fedha za kumsaidia yeye pamoja na mimi mwenyewe.
Walionisaidia kunichangia wakati nasoma wanasikitika, yaani inafika hatua sasa sitaki hata kukutana nao.

Serikali yangu!! Naomba mniondolee aibu hii. Naomba mniajiri jamani.

Nimetafuta Kazi za kufundisha kwenye Shule Binafsi na kwenye Makampuni sijapata. Matangazo ya kazi yanatoka nikituma maombi, hata kwenye usahili tu siitwi.
Nikiwa nauliza watu tatizo ni nini jamani sipati kazi. Naambiwa "huna mtu wa kukushika mkono, tafuta mtu akusaidie". Hapa ndio nachoka zaidi.
Maana kwenye Familia yetu tupo watoto Sita (6) na Kati ya hao wanne wa kike walishaolewa (walimaliza darasa la Saba tu) mmoja ni Kaka yangu, alimaliza la Saba tu. Mimi pekee ndiye nimefanikiwa kufikia hatua ya Chuo Kikuu. Sasa najiuliza ni nani wa kunishika mkono hapa? Nagundua sina mtu.

Basi nasema, nipate hata mfadhili anifadhili mtaji nianzishe Biashara zangu huku nikisubiri ili nipate pa kujikimu bado kumpata mtu ni kitendawili.
Naishi kwa Taabu sana.

Hivi sasa nipo tu nyumbani Mkoa wa Mwanza.
Naomba kwa yeyote atayesoma ujumbe huu awe Kiongozi wa Serikali, Mtu binafsi mwenye kazi zake binafsi, mfanyabiashara au Kampuni ajue kuwa ninaomba mambo haya yafuatayo na nipo tayari kufanya wakati wowote:

1. Natafuta kazi yoyote ya kufanya iwe kwenye Kampuni au kwa mtu binafsi ilimradi iwe halali na nipate jinsi ya kujikimu.

2. Nipo tayari kujitolea kufundisha katika shule yoyote Masomo yangu ni (ENGLISH LANGUAGE & HISTORY).

3. Kama kuna mtu anaweza kunisaidia mtaji wa biashara kwa makubaliano ambayo ni nafuu, naomba anisaidie. Nipo tayari.

4. Naomba Serikali iniajiri ili nitumikie Taifa langu la Tanzania.

5. Nipo tayari kwenda Mkoa wowote ili kufanya kazi katika Ofisi yoyote ilimradi nipate pesa ya kujikimu Mimi na Mama yangu.

Maandiko Matakatifu yanasema, Nayaweza yote katika yeye yule (MUNGU) anitiae nguvu.
Ninaishi kwa uwezo wake MUNGU.
Natamani nifanye kazi, maana imeagizwa hivyo!!

Nimeona ni vyema kutoa ujumbe wangu kwa kutumia mitandao ya kijamii kupitia simu ya mtu ninaemfahamu kwakuwa ninaamini kuwa siku hizi Serikali na watu Binafsi wanatumia sana mitandao hii.

Mawasiliano yangu ni;

0746407415
Kama ukiwa na jambo lolote kwangu au unataka kunitia moyo kwa namna unayoona inafaa tafadhali tuwasiliane kwa namba hiyo.

SAMBAZA UJUMBE HUU ILI KUMSAIDIA HUYU KIJANA WA KITANZANIA.
 
Pole Sana dogo naamini kabisa utafanikiwa

Usijione mnyonge Ni wengi Sana wanapitia mapito Kama yako.

Me nashangaa kwanini serikali inawatelekeza watu wengi waliosoma elimu kiwango Cha shahada na kuwapa mashavu wenye certificate na diploma.

Kiukweli watu wenye degree by 2010- 2020 wanasota Sana mtaani halafu ajira zinakuja na masharti ya umri na Mambo mengine .

Vijana wanaumia Sana Sana sio Siri serikali ijaribu kufanya research ya wahitimu wenye mahitaji ya ajira kulingana na familia zao maana wengine wanao uwezo wa kupata mitaji ila wengine hawana uwezo kutokana na family background.
Nashauri walimu waajiriwe maana kuna upungufu mkubwa Sana wa walimu.
 
Nyumbani kwangu ninao wa aina yako watatu wa aina yako. Na wa nne anahitimu mwakani. Wote hawana ajira. Inaniuma sana vijana kurudi na kukuuliza Baba sasa tufanyeJe !! Nabaki na chukia

Awamu ya tano ilileta majanga na ujenzi wa madaraja wakasahau kila kitu ktk mahitaji ya kila siku ya mwananchi.
 
NATUMIA SIKU HII YA MAADHIMISHO YA WALIMU, KUZUNGUMZA NA WATANZANIA WENZANGU NA SERIKALI.

Usichoke kusoma!! Soma, Soma, Soma ujumbe wangu Mimi Mwalimu nisiye na Darasa la kufundisha, Vyeti vyangu vya Kuhitimu Chuo Kikuu vimekoswa kazi kwenye begi!!

Mimi ni Kijana wa Kitanzania, ambaye nimetimiza miaka 30 sasa. Naitwa Josephat.
Nimeona niandike ujumbe wangu huu siku hii ya leo ili kwa yeyote atakaefanikiwa kuusoma, aone jinsi ya kunisaidia ama kusaidia wengine walio na mazingira kama yangu.

Kwa taaluma Mimi ni Mwalimu. Nimehitimu mwaka 2017.

Nikiwa kidato cha tatu Mwaka 2010, nilifukuzwa Shule na Mwalimu wangu Mkuu kwa kukoswa Ada ya kulipia Mwaka.
Wakati huo Baba yangu (miaka 86 kwa wakati huo) alikuwa ameanza kuugua, japo akiwa bado hajachoka. Baba akatoa kauli kwamb Ardhi iliyopo kidogo pale Kijijini kwetu iuzwe ili niendelee na Masomo (Japo wakati naingia kidato cha kwanza Ardhi pia iliuzwa nikafanikiwa kuingia).
Tuliuza Ardhi nyingine kwa Mara ya pili, nikapata fedha nikarudi shule.
Mwaka 2011 nimehitimu Kidato cha Nne. Natakiwa kwenda Advance, sina hela tena.
Ikabidi Baba auze tena kauwanja ambako kalikuwa kamebaki (Ninavyoandika hapa, nyumbani hakuna Ardhi ya kuweza kulima, kuna uwanja wa mahali zilipo nyumba zetu za kuishi tu).
Baba yangu aliamini nikisoma basi nitapata kazi nzuri na kurejesha vyote hivyo vilivyopotea. Hapa sijaelezea juhudi za Mama yangu alivyokuwa anatoka kwenda kufanya vibarua na kuniletea pesa ili kulipa shuleni, lengo nisome. Asante Mama yangu.
Mipango ya MUNGU mwanadamu hawezi kuzuia. Mwaka 2012 nimeingia tu kidato cha Tano, nikajulishwa kuwa Baba yangu amefariki!! So sad!!. Tena alifariki kwa kukoswa pesa ya matibabu (alifia nyumbani).
Nilitamani niende kumzika Baba, lakini sikuwa na nauli ya kurudi nyumbani kumzika Baba. Nikapiga moyo konde!!
Baba yangu akatangulia, nikabaki na Mama yangu!!

Mwaka 2014 nimehitimu Kidato cha Sita, nikajiunga Chuo Kikuu mwaka wa Kwanza.
Nikasoma kwa taabu sana mwanzoni kwa kukoswa Mkopo Mwaka wa kwanza, (nikachangiwa na watu, maana kwenye ukoo na Familia nimesoma Mimi tu), MUNGU saidia mwaka wa pili nikapata Mkopo wa Serikali hadi mwaka wa Tatu.

Nimemaliza mwaka 2017 nimerudi nyumbani, nikitazamia Ajira Serikalini.
Nimetuma maombi Serikalini tangu mwaka 2018 hadi leo Mwaka 2021 sijawahi kuchukuliwa na Serikali ili kwenda kufanya kazi niliyosomea, na ninaipenda sana.
Kwakweli nilikata tamaa. Mama yangu ananiuliza kila siku, "mbona huajiriwi Serikalini, au hukumaliza Masomo?" Namwambia hapana Mama, nilimaliza nasubiri Serikali iniajiri, labda bahati yangu bado.
Mama yangu kwakuwa hakusoma, anachoka na anakata tamaa kila akiniona.
Sina kazi na sina fedha za kumsaidia yeye pamoja na mimi mwenyewe.
Walionisaidia kunichangia wakati nasoma wanasikitika, yaani inafika hatua sasa sitaki hata kukutana nao.

Serikali yangu!! Naomba mniondolee aibu hii. Naomba mniajiri jamani.

Nimetafuta Kazi za kufundisha kwenye Shule Binafsi na kwenye Makampuni sijapata. Matangazo ya kazi yanatoka nikituma maombi, hata kwenye usahili tu siitwi.
Nikiwa nauliza watu tatizo ni nini jamani sipati kazi. Naambiwa "huna mtu wa kukushika mkono, tafuta mtu akusaidie". Hapa ndio nachoka zaidi.
Maana kwenye Familia yetu tupo watoto Sita (6) na Kati ya hao wanne wa kike walishaolewa (walimaliza darasa la Saba tu) mmoja ni Kaka yangu, alimaliza la Saba tu. Mimi pekee ndiye nimefanikiwa kufikia hatua ya Chuo Kikuu. Sasa najiuliza ni nani wa kunishika mkono hapa? Nagundua sina mtu.

Basi nasema, nipate hata mfadhili anifadhili mtaji nianzishe Biashara zangu huku nikisubiri ili nipate pa kujikimu bado kumpata mtu ni kitendawili.
Naishi kwa Taabu sana.

Hivi sasa nipo tu nyumbani Mkoa wa Mwanza.
Naomba kwa yeyote atayesoma ujumbe huu awe Kiongozi wa Serikali, Mtu binafsi mwenye kazi zake binafsi, mfanyabiashara au Kampuni ajue kuwa ninaomba mambo haya yafuatayo na nipo tayari kufanya wakati wowote:

1. Natafuta kazi yoyote ya kufanya iwe kwenye Kampuni au kwa mtu binafsi ilimradi iwe halali na nipate jinsi ya kujikimu.

2. Nipo tayari kujitolea kufundisha katika shule yoyote Masomo yangu ni (ENGLISH LANGUAGE & HISTORY).

3. Kama kuna mtu anaweza kunisaidia mtaji wa biashara kwa makubaliano ambayo ni nafuu, naomba anisaidie. Nipo tayari.

4. Naomba Serikali iniajiri ili nitumikie Taifa langu la Tanzania.

5. Nipo tayari kwenda Mkoa wowote ili kufanya kazi katika Ofisi yoyote ilimradi nipate pesa ya kujikimu Mimi na Mama yangu.

Maandiko Matakatifu yanasema, Nayaweza yote katika yeye yule (MUNGU) anitiae nguvu.
Ninaishi kwa uwezo wake MUNGU.
Natamani nifanye kazi, maana imeagizwa hivyo!!

Nimeona ni vyema kutoa ujumbe wangu kwa kutumia mitandao ya kijamii kupitia simu ya mtu ninaemfahamu kwakuwa ninaamini kuwa siku hizi Serikali na watu Binafsi wanatumia sana mitandao hii.

Mawasiliano yangu ni;

0746407415
Kama ukiwa na jambo lolote kwangu au unataka kunitia moyo kwa namna unayoona inafaa tafadhali tuwasiliane kwa namba hiyo.

SAMBAZA UJUMBE HUU ILI KUMSAIDIA HUYU KIJANA WA KITANZANIA.
Pole sana!

Andiko linawakilisha wengi, lakini pia ni andiko lenye fasihi pana na nzito ya "Riwaya ya Mwalimu asiye Mwalimu".

Ni ujumbe mzito unaoonyesha mahangaiko ya Vijana wengi Watanzania. Hao wenye mashahada wanahangaika, wamachinga wanahangaika, walio makazini nao wanahangaika.......... tujiandae hii hali ina mwisho wake, tena si muda mrefu tuliowengi tutashuhudia........

Wale wenzetu wenye bahati ya kula na kusaza....wasaidieni hawa ndugu....... siku za kuzaliwa wote tulikuwa tunafanana, hakuna aliyekuja amevikwa.......na siku ya kuondoka wote tutafukiwa tu ardhini, hakuna atakayehifadhiwa kwa Freezer.

Ahsante kwa bandiko lenye fasihi nzito yenye tafakuri nzito kabisa.
 
Ubarikiwe sana
 
Nyumbani kwangu ninao wa aina yako watatu wa aina yako. Na wa nne anahitimu mwakani. Wote hawana ajira. Inaniuma sana vijana kurudi na kukuuliza Baba sasa tufanyeJe !! Nabaki na chukia

Awamu ya tano ilileta majanga na ujenzi wa madaraja wakasahau kila kitu ktk mahitaji ya kila siku ya mwananchi.
Aisee!!
 
Acha kulialia mwalimu. Tayari ushaelimika. Tumia elimu yako kujiajiri. Fungua hata tuition center ya kufundishia watoto/vijana.

Shughuli za kufanya zipo nyingi. Hata kulima huku mikoani mashamba yapo mengi tu. Mje. Acheni kuzurura na bahasha mikononi.
Tumia elimu yako, ikusaidie kupambana na hali halisi huku field.
Kulialia hakutakusaidia.
 
Ndugu yangu kuongea ni rahis Sana Tena sana ,kwa maelezo aliyoyatoa huyu ndugu sidhan km ungepata hata hiyo nguvu ya kuongea hayo.

Kwanza nikuulize anafungua twisheni center kwa mtaji upi? Au unafungua tu Kama kamba za viatu. Tuition center inahitaji mtaji kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, sehemu yakufundishia.

Kwa maelezo aliyoyatoa huyo ndugu mwalimu unamwona Ana viashiria vya uvivu wa kutofanya kazi hata ya tuition?

Siku nyingine km huna Cha kuchangia Bora ukae kimya ,sisi wenye ndugu na jamaa wa dizain hii tunajua wanavyohangaika na hata kutaka kazi ya kulipwa 150k na wanakosa .

Pia hakuna mhitimu wa ngazi ya degree ambae angependa kudharirika kitaa ingawa wengi mna kauli et badil elimu kuwa mtaji ,swal unabadir vipi wakat hujui pakuanzia na elimu yetu haifundishi ujasiriamal au elimu ya kujitegemea.

Mpe pakuanzia alafu akishindwa uje umlaumu hapa ,yaan mpe msaada hata wachumba Cha kufundishia hiyo tuition plus vifaa ,wateja atapambana yeye kwa kuwapata.

Narudia Tena ni rahis Sana kuongea pia usiombe upitie Hali ya huyu jamaa ,maana naamin anatamani hata apate kibarua Cha kulipwa kwa siku elfu tatu na hicho kibarua hakipo.
Alafu et aje hata mkoani alime, hivi unaamin mikoan Kuna ardhi ya bure ? Na vipi Kuna kilimo bila mtaji? Je wote Wana mashamba huko mikoani?
 
Wako watu walemavu,wamepoteza wazazi kwasasa,hawana elimu na wanapambana!
Muhimu tafuta ajira private omba kujitolea kwanza bure pigs kazi badae uyapewa chochote. Chamuhimu pambana usitiishe huruma
 
Ungekuw dar nngekuomba tuonane nkushauri jambo.
 
Sasa ulitaka wote tumwonee huruma! Lugha za hivi zinamfanya mtu ajiongeze. Sasa ajira hamna, wewe unategemea aendelee kutembea na bahasha kitaa anatafuta kazi?

Huku kitaa wapo draduate kibao. Wengine mabodaboda wengine mafundi simu wasanii, wengine wakulima nk.
 
Pole Mungu akutangulie ila na nature ya masomo ungekuwa umesoma eg Maths,Physics,Bios au chem ungekuw umepata...ila History
 
Ndugu yangu kuongea ni rahis Sana Tena sana ,kwa maelezo aliyoyatoa huyu ndugu sidhan km ungepata hata hiyo nguvu ya kuongea hayo.

Kwanza nikuulize anafungua twisheni center kwa mtaji upi? Au unafungua tu Kama kamba za viatu. Tuition center inahitaji mtaji kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, sehemu yakufundishia.

Kwa maelezo aliyoyatoa huyo ndugu mwalimu unamwona Ana viashiria vya uvivu wa kutofanya kazi hata ya tuition?

Siku nyingine km huna Cha kuchangia Bora ukae kimya ,sisi wenye ndugu na jamaa wa dizain hii tunajua wanavyohangaika na hata kutaka kazi ya kulipwa 150k na wanakosa .

Pia hakuna mhitimu wa ngazi ya degree ambae angependa kudharirika kitaa ingawa wengi mna kauli et badil elimu kuwa mtaji ,swal unabadir vipi wakat hujui pakuanzia na elimu yetu haifundishi ujasiriamal au elimu ya kujitegemea.

Mpe pakuanzia alafu akishindwa uje umlaumu hapa ,yaan mpe msaada hata wachumba Cha kufundishia hiyo tuition plus vifaa ,wateja atapambana yeye kwa kuwapata.

Narudia Tena ni rahis Sana kuongea pia usiombe upitie Hali ya huyu jamaa ,maana naamin anatamani hata apate kibarua Cha kulipwa kwa siku elfu tatu na hicho kibarua hakipo.
Alafu et aje hata mkoani alime, hivi unaamin mikoan Kuna ardhi ya bure ? Na vipi Kuna kilimo bila mtaji? Je wote Wana mashamba huko mikoani?
Andiko lako nimelielewa sana ndugu, umevaa viatu vya ndugu yetu kwa usahihi. Asante sana ndugu, maana wengine humu wanaandika kama wamekatwa vichwa.
 
Back
Top Bottom