Natafuta shule ya kufanyia Teaching Practice

Apparent

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
220
110
Habari ndugu zangu.
Naomba anaefahamu wapi kuna shule ya serikali(Kidato cha kwanza hadi cha sita) ambayo ipo karibu kabisa na maeneo yafuatayo(karibu na barabara ya lami yenye daladala za moja kwa moja hadi Ubungo).

1.Ubungo hadi Mbezi mwisho
2.Ubungo hadi Tabata Segerea
3.Ubungo hadi Tegeta Nyuki
4.Ubungo hadi Makumbusho na Morocco
5.Ubungo hadi Kariakoo

Mimi naishi Chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) hivyo natafuta sehemu ambayo nitaweza kufika kwa urahisi.

Msaada wenu ni mhimu sana kwangu.
Mimi ni Mwalimu wa Form 1-6
Ordinary level and Advanced level.
 
kumbe unataka dar?? juzi zilitoka nafasi kwa wanaotaka kwenda lindi meals & accommodation pamoja na allowance ni free
nitafute kama uko gud nipo UDSM pia
 
Siwezi kwenda tofauti na maeneo tajwa hapo juu.
kumbe unataka dar?? juzi zilitoka nafasi kwa wanaotaka kwenda lindi meals & accommodation pamoja na allowance ni free
nitafute kama uko gud nipo UDSM pia
 
Nenda pale stand ya mawasiliano kwa mbele kuna shule inaitwa Mugabe sec. School govt ni ordinary level
 
Jaza yusuph makamba sec mkuu..... Ipo hapa unakatshia external hii njia ya TFDA Jaza hii mkuu hata kuwahi kutoka unawahi saana afu kuko poa kabisa mkuu
 
Jaza yusuph makamba sec mkuu..... Ipo hapa unakatshia external hii njia ya TFDA Jaza hii mkuu hata kuwahi kutoka unawahi saana afu kuko poa kabisa mkuu
Asante mkuu.
Nimefika hadi pale shule nimepakubali.
Changamoto ni usafiri itabidi nitafute chumba nipange kwa miezi mitatu.
 
Back
Top Bottom