Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,582
- 28,734
Wakuu natafuta shamba la kununua lenye ukubwa usiopungua hekari 30, kwa ajili ya project yangu ya kilimo mwaka ujao ninayotegemea kuifanya nje kidogo ya jiji la Dar es Salam, shamba hilo naomba liwe na sifa zifuataazo:
- Liwe na ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo hususani mahindi
- Liwe eneo lenye water-table iliyo karibu, eneo ambalo nikichimmba kisima cha ku-drill nitapata uhakika wa maji kuanzia lita 5,000 kwa siku, na iwe ni kwa mwaka mzima.
- Liwe pembezoni mwa mji lakini umbali usizidi km 50 kutoka Dar es Salaam.
- Liwe linafikika kwa urahisi kwa gari kwa ajili ya kusafirisha mazao yangu kutoka shambani
- Uwepo wa umeme japo si muhimu sana
Kwa mwenye kuwa nalo au yeyote mwenye kuuza naomba tuwasiliane hapa au kwa PM hususani kwa mambo kama bei, vibali na location.
Natanguliza shukrani
Maeneo ya hivyo ni lazima yawe huko Mlandizi,Kibaha,Kisarawe,na Mkuranga. Ila kama una ubavu nenda Bagamoyo maeneo baada ya kupita Kiwangwa kama unakwenda Msata, ile ardhi inamea mahindi vizuri sana, tatizo iko nje ya umbali unaotaka ww. Umeme upo, ndio unapita sasa, na maji ndio wanatawanya sasa hivi ya bomba.
Au jaribu Kidugalo, kuna ardhi nzuri sana ya mahindi,ila maji mtihani,umeme bado. Ni km 100 hivi toka Dar kwenda kule. Gwata ni km 115 toka Buguruni kwenda kule, tatizo la Gwata ni mifugo,ila ardhi ipo kubwa.
Wakuu natafuta shamba la kununua lenye ukubwa usiopungua hekari 30, kwa ajili ya project yangu ya kilimo mwaka ujao ninayotegemea kuifanya nje kidogo ya jiji la Dar es Salam, shamba hilo naomba liwe na sifa zifuataazo:
- Liwe na ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo hususani mahindi
- Liwe eneo lenye water-table iliyo karibu, eneo ambalo nikichimmba kisima cha ku-drill nitapata uhakika wa maji kuanzia lita 5,000 kwa siku, na iwe ni kwa mwaka mzima.
- Liwe pembezoni mwa mji lakini umbali usizidi km 50 kutoka Dar es Salaam.
- Liwe linafikika kwa urahisi kwa gari kwa ajili ya kusafirisha mazao yangu kutoka shambani
- Uwepo wa umeme japo si muhimu sana
Kwa mwenye kuwa nalo au yeyote mwenye kuuza naomba tuwasiliane hapa au kwa PM hususani kwa mambo kama bei, vibali na location.
Natanguliza shukrani
Malila kila siku unanipa kibwagizo kipya , Gwata ni wapi huko?
Zipo Gwata mbili, mimi nazungumzia Gwata ya Kisarawe. Kama ukifika Mzenga, kuna njia inakwenda Mafizi kupitia Mwanamsekwa, Nyani hadi Gwata. Gwata pana watu wengi sana,wakulima na wafugaji,usafiri wa bus kuja Buguruni upo kila siku, usafiri wa tren upo. Ardhi ipo nzuri sana kando ya mto Ruvu. Lipo gulio kubwa kwa siku nne mfululizo,la mifugo zaidi. Biashara ya nyumba za wageni inalipa sana kuanzia alhamisi mpaka jumapili.
H/shauri ya Kisarawe wanataka kujenga mnada wa kisasa pale,viwanja vimepanda bei vibaya baada ya plan hiyo kuwekwa peupe. Mimi nilifuata ardhi ya kuotesha cocoa. Jamaa zetu Waarabu wamekomba mapande ya ardhi kinoma. Sijasikia ugomvi wa ardhi kule. Maji ni mto Ruvu, ni nguvu yako. Na migomba inamea pia.
Gwata ya pili iko Migindu huko Chalinze,
Swali lingine kaka!!!!!!!

Hebu siku moja tufanye tuonane tufunge safari tukatembelee hiyo mitaa maana kwangu ni sehemu ngeni kabisa.
Ardhi ya huko bei zikoje?
Kwa eka moja ilikuwa Tsh 50,000/ kwa eka, juzi nilisikia imepanda mpaka 80,000/ kwa eka. Naamini baada ya hawa jamaa kutoka mashariki ya kati kuvamia itakuwa inacheza kwenye laki moja hivi.
Nikirudi Dar mwisho wa mwaka tutafutane tukatembee mitaa ya kule.
Thnx kwa info,kiongozi vp khs Nguvu kz! Tractor zinapatikanaje huko?
Kwa eka moja ilikuwa Tsh 50,000/ kwa eka, juzi nilisikia imepanda mpaka 80,000/ kwa eka. Naamini baada ya hawa jamaa kutoka mashariki ya kati kuvamia itakuwa inacheza kwenye laki moja hivi.
Nikirudi Dar mwisho wa mwaka tutafutane tukatembee mitaa ya kule.
Bei yake ni kiasi gani kwa hekari mkuu??Kuna shamba kisalawe lina hekali24 lina sifa zote ila lipo km,60 kutoka dar
Shukrani sana mkuu naona ulipo hakiharibiki kitu mkuu...Zipo Gwata mbili, mimi nazungumzia Gwata ya Kisarawe. Kama ukifika Mzenga, kuna njia inakwenda Mafizi kupitia Mwanamsekwa, Nyani hadi Gwata. Gwata pana watu wengi sana,wakulima na wafugaji,usafiri wa bus kuja Buguruni upo kila siku, usafiri wa tren upo. Ardhi ipo nzuri sana kando ya mto Ruvu. Lipo gulio kubwa kwa siku nne mfululizo,la mifugo zaidi. Biashara ya nyumba za wageni inalipa sana kuanzia alhamisi mpaka jumapili.
H/shauri ya Kisarawe wanataka kujenga mnada wa kisasa pale,viwanja vimepanda bei vibaya baada ya plan hiyo kuwekwa peupe. Mimi nilifuata ardhi ya kuotesha cocoa. Jamaa zetu Waarabu wamekomba mapande ya ardhi kinoma. Sijasikia ugomvi wa ardhi kule. Maji ni mto Ruvu, ni nguvu yako. Na migomba inamea pia.
Gwata ya pili iko Migindu huko Chalinze,
Swali lingine kaka!!!!!!!
Shukrani sana mkuuMkuu samahani kwa kuingilia uzi, kwa swali lako la kuotesha majani ya mifugo wengi kwenye eneo dogo, technology inayotumiwa kenya kwa manufaa makubwa ni hydroponic fodder hii ni technologia ya kukuza mimea bola udongo na kwa majani ya mifugo wanatimia zaidi barley kiswahili chake sijui. Ndani ya siku saba unakwa umeshapata majani mabichi kwa mifugo yako. Ni technology ngeni kidogo lakini naona wemzetu wemufaika . Kwa maelezo jinsi ya kupata technologia hii google hyroponics kenya. Kuna bwana ambaye anauza technologia hii na siyo gharama kubwa sana.
Mkuu nimefuatilia hii kitu imenistusha sana aiseeeKaribu mkuu, naamini mtanzania akipata technologia hii itakuwa rahisi na wengine pia kupata kwa urahisi.